بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
أَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي يُكَذِّبُ بِٱلدِّينِ ١Je, waiona hali ya yule ambaye akanusha kufufuliwa na kulipwa فَذَٰلِكَ ٱلَّذِي يَدُعُّ ٱلۡيَتِيمَ ٢Huyo ndiye yule anayemkaripia yatima kwa nguvu akimnyima haki yake kwa sababu ya ususuavu wa moyo wake وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ ٣Na wala hawahimizi wengine kulisha masikini. Vipi yeye mwenyewe atamlisha فَوَيۡلٌ لِّلۡمُصَلِّينَ ٤Basi adhabu kali itawafikia wenye kusali ٱلَّذِينَ هُمۡ عَن صَلَاتِهِمۡ سَاهُونَ ٥ambao wameghafilika na Swala zao: hawazisimamishi kama ipasavyo wala hawazisali kwa nyakati zake ٱلَّذِينَ هُمۡ يُرَآءُونَ ٦Ambao huonyesha watu amali zao za kheri kwa njia ya ria وَيَمۡنَعُونَ ٱلۡمَاعُونَ ٧Na wanakataa kuwaazima watu vitu ambavyo hawadhuriki kwa kuviazima, kama vyombo vya kutumia na vinginevyo. Wao hawakujifanyia wema nafsi zao kumuabudu Mola wao wala hawakuwafanyia wema viumbe Vyake