Millat al-Islam

Chapter 79 · 46 verses · Abdullah Muhammad Abu Bakr

Surah An-Naziat in Swahili

Arabic with tafsir Listen to Surah An-Naziat (1339 reciters)

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلنَّٰزِعَٰتِ غَرۡقًا ١Anaapa Mwenyezi Mungu kwa Malaika ambao huzing’oa roho za makafiri mng’oo mkali وَٱلنَّٰشِطَٰتِ نَشۡطًا ٢Na kwa Malaika ambao huzitukua roho za Waumini kwa uchangamfu na upole وَٱلسَّٰبِحَٰتِ سَبۡحًا ٣Na kwa Malaika wanaoogelea katika kushuka kwao kutoka mbinguni na kupaa kwao kwenda mbinguni فَٱلسَّٰبِقَٰتِ سَبۡقًا ٤Na kwa Mlaika ambao wanakimbilia kutekeleza amri za Mwenyezi Mungu فَٱلۡمُدَبِّرَٰتِ أَمۡرًا ٥Na kwa Malaika wanaopitisha amri za Mola wao katika mambo ya ulimwengu waliowakilishwa kuyafanya na kuyasimamia, - Wala haifai kwa kiumbe kukiapia chochote kile, bali yapasa kiapo chake kiwe ni kwa jina la Mola wake Muumba au sifa Zake. Na lau ataapa kwa asiye Muumba wake, basi huyo amekuwa mshirikina - Watafufuliwa viumbe bila shaka na watahesabiwa يَوۡمَ تَرۡجُفُ ٱلرَّاجِفَةُ ٦Siku ambayo ardhi itatetemeka kwa mvuvuo wa kwanza تَتۡبَعُهَا ٱلرَّادِفَةُ ٧mvuvio wa kufisha, ukifuatiwa na mvuvio mwingine wa kuhuisha قُلُوبٌ يَوۡمَئِذٍ وَاجِفَةٌ ٨Nyoyo za makafiri, Siku hiyo, zitakuwa na papatiko kwa kicho kikubwa أَبۡصَٰرُهَا خَٰشِعَةٌ ٩Macho ya makafiri hao yatakuwa madhalilifu kwa kitisho watakachokiona يَقُولُونَ أَءِنَّا لَمَرۡدُودُونَ فِي ٱلۡحَافِرَةِ ١٠Wanasema hawa wakanushao kufufuliwa أَءِذَا كُنَّا عِظَٰمًا نَّخِرَةً ١١«Je, tutarudishwa baada ya kufa kwetu kwenye yale tuliyokuwa nayo katika ardhi? Je, tutarudishwa na hali tushakuwa mifupa iliochakaa?» قَالُواْ تِلۡكَ إِذًا كَرَّةٌ خَاسِرَةٌ ١٢Wakasema: «Kurejea kwetu huko kutakuwa kutupu kusikokuwa kweli.’ فَإِنَّمَا هِيَ زَجۡرَةٌ وَٰحِدَةٌ ١٣Hakika tukio hilo litakuwa kwa mvivio mmoja tu فَإِذَا هُم بِٱلسَّاهِرَةِ ١٤Wakitahamaki wao wako hai juu ya ardhi baada ya kuwa walikuwa ndani yake هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ مُوسَىٰٓ ١٥Je imekujilia, ewe Mtume, habari ya Mūsā إِذۡ نَادَىٰهُ رَبُّهُۥ بِٱلۡوَادِ ٱلۡمُقَدَّسِ طُوًى ١٦Pindi Mola wake Alipomwita katika bonde lililotakaswa na kubarikiwa, la Ṭuwā. Akamwambia ٱذۡهَبۡ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ إِنَّهُۥ طَغَىٰ ١٧«Enda kwa Firauni. Hakika yeye amekiuka mno katika kuasi فَقُلۡ هَل لَّكَ إِلَىٰٓ أَن تَزَكَّىٰ ١٨Ukamwambie, ‘Je, unapendelea kuitakasa nafsi yako na upungufu na kuipamba na imani وَأَهۡدِيَكَ إِلَىٰ رَبِّكَ فَتَخۡشَىٰ ١٩Na nikuelekeze njia ya kumtii Mola wako, upate kumcha na kumuogopa?’» فَأَرَىٰهُ ٱلۡأٓيَةَ ٱلۡكُبۡرَىٰ ٢٠Mūsā alimuonyesha Firauni alama kubwa: fimbo na mkono فَكَذَّبَ وَعَصَىٰ ٢١Hapo Firauni alimkanusha Nabii wa Mwenyezi Mungu , naye ni Mtume Mūsā, amani imshukie, na alimuasi Mola wake Aliyetukuka ثُمَّ أَدۡبَرَ يَسۡعَىٰ ٢٢Kisha alikengeuka hali ya kuipa mgongo Imani na kufanya bidii katika kumpinga Mūsā فَحَشَرَ فَنَادَىٰ ٢٣Hapo aliwakusanya raia wa utawala wake na akawaita kwa فَقَالَ أَنَا۠ رَبُّكُمُ ٱلۡأَعۡلَىٰ ٢٤kuwaambia,»Mimi ndiye mola wenu ambaye hakuna mola mwengine aliye juu yake.» فَأَخَذَهُ ٱللَّهُ نَكَالَ ٱلۡأٓخِرَةِ وَٱلۡأُولَىٰٓ ٢٥Hapo Mwenyezi Mungu Alimtesa kwa adhabu ya duniani na ya Akhera إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبۡرَةً لِّمَن يَخۡشَىٰٓ ٢٦Na Akaifanya adhabu hiyo iwe ni mazingatio na ni onyo kwa watu mfano wake kati ya wale waasi. Hakika Firauni na kile kilichompata cha adhabu ni mawaidha kwa mwenye kuwaidhika na kutishika ءَأَنتُمۡ أَشَدُّ خَلۡقًا أَمِ ٱلسَّمَآءُۚ بَنَىٰهَا ٢٧Je, kufufuliwa kwenu, enyi watu, baada ya kufa ni kugumu zaidi, katika vipimo vyenu, au ni kuumbwa kwa mbingu رَفَعَ سَمۡكَهَا فَسَوَّىٰهَا ٢٨Amezipanga juu yenu kama jengo. Na Ameinua sakafu yake angani, haina tofauti wala nyufa وَأَغۡطَشَ لَيۡلَهَا وَأَخۡرَجَ ضُحَىٰهَا ٢٩Na Ameutia giza usiku wake kwa kutwa kwa jua lake. Na Ameweka wazi mchana wake kwa kuchomoza kwake وَٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ ذَٰلِكَ دَحَىٰهَآ ٣٠Na ardhi baada ya kuumba mbingu Ameitandaza. Na Ameweka humo manufaa yake أَخۡرَجَ مِنۡهَا مَآءَهَا وَمَرۡعَىٰهَا ٣١Na Ametumbua humo chemchemu za maji. Na Ameotesha humo mimea inayolishwa وَٱلۡجِبَالَ أَرۡسَىٰهَا ٣٢Na Ameyakita humo majabali yakiwa ni vigingi vyake. Ameumba, Aliyetakasika na kila upungufu مَتَٰعًا لَّكُمۡ وَلِأَنۡعَٰمِكُمۡ ٣٣neema zote hizi zikiwa ni manufaa kwenu na kwa wanyama wenu. (Hakika kurudisha kuumbwa kwenu, Siku ya Kiyama, ni sahali kwa Mwenyezi Mungu kushinda kuumba viumbe hivyo vyingine. Na vyote hivyo, kwa Mwenyezi Mungu, ni rahisi na ni vipesi) فَإِذَا جَآءَتِ ٱلطَّآمَّةُ ٱلۡكُبۡرَىٰ ٣٤Pindi kitakapokuja Kiyama Kikubwa na balaa nzito, nao ni Mvuvio wa pili. Kipindi hicho zitaoneshwa kwa binadamu vitendo vyake vyote, za kheri na za shari يَوۡمَ يَتَذَكَّرُ ٱلۡإِنسَٰنُ مَا سَعَىٰ ٣٥Hapo atazikumbuka na kuzitambua وَبُرِّزَتِ ٱلۡجَحِيمُ لِمَن يَرَىٰ ٣٦Na utaoneshwa Moto wa Jahanamu kwa kila aonaye, uwe waonekana waziwazi فَأَمَّا مَن طَغَىٰ ٣٧Ama yule atakayekiuka amri ya Mwenyezi Mungu وَءَاثَرَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا ٣٨na akapendelea maisha ya ulimwenguni kuliko ya Akhera فَإِنَّ ٱلۡجَحِيمَ هِيَ ٱلۡمَأۡوَىٰ ٣٩basi kwa kweli marejeo yake ni Motoni وَأَمَّا مَنۡ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِۦ وَنَهَى ٱلنَّفۡسَ عَنِ ٱلۡهَوَىٰ ٤٠Na ama yule atakayeogopa kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu kuhesabiwa na akaikanya nafsi yake na matamanio mapotofu فَإِنَّ ٱلۡجَنَّةَ هِيَ ٱلۡمَأۡوَىٰ ٤١basi Peponi ndiko makazi yake يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلسَّاعَةِ أَيَّانَ مُرۡسَىٰهَا ٤٢Wanakuuliza washirikina, ewe Mtume, kwa madharau, kuhusu wakati wa kuanzia Kiyama unachowaonya فِيمَ أَنتَ مِن ذِكۡرَىٰهَآ ٤٣Wewe huna kamwe ujuzi nacho إِلَىٰ رَبِّكَ مُنتَهَىٰهَآ ٤٤Bali mambo ya ujuzi huo yarejeshwe kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye Sifa Tukufu إِنَّمَآ أَنتَ مُنذِرُ مَن يَخۡشَىٰهَا ٤٥Wewe linalokuhusu katika habari zake ni kumuonya nacho yule anayekiogopa كَأَنَّهُمۡ يَوۡمَ يَرَوۡنَهَا لَمۡ يَلۡبَثُوٓاْ إِلَّا عَشِيَّةً أَوۡ ضُحَىٰهَا ٤٦Kama kwamba wao siku watakapouona Kiyama kimesimama, watakuwa hawakukaa katika maisha yao ya duniani, kwa vituko vya hiko Kiyama, isipokuwa ni kama kwamba wamkaa kati ya adhuhuri mpaka kutwa juwa, au ni kama kati ya kuchomoza jua mpaka nusu ya mchana

Translation: Abdullah Muhammad Abu Bakr.