Millat al-Islam

Chapter 94 · 8 verses · Abdullah Muhammad Abu Bakr

Surah Al-Inshirah in Swahili

Arabic with tafsir Listen to Surah Al-Inshirah (1282 reciters)
Meccanسورة الشرح8 verses

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

أَلَمۡ نَشۡرَحۡ لَكَ صَدۡرَكَ ١Kwani Hatukukunjulia, ewe Mtume, kifua chako kwa sheria za Dini, kulingania watu kwa Mwenyezi Mungu na kujipamba kwa tabia nzuri وَوَضَعۡنَا عَنكَ وِزۡرَكَ ٢Tukakuondolea mazito yako yaliyoemea mgongo wako ٱلَّذِيٓ أَنقَضَ ظَهۡرَكَ ٣na Tukakuweka, kwa matukufu Tuliyokuneemesha وَرَفَعۡنَا لَكَ ذِكۡرَكَ ٤kwenye cheo cha juu فَإِنَّ مَعَ ٱلۡعُسۡرِ يُسۡرًا ٥Usirudi nyuma katika kueneza ujumbe uliotumwa nao kwa makero ya maadui zako. Kwani kwenye dhiki kuna faraji إِنَّ مَعَ ٱلۡعُسۡرِ يُسۡرًا ٦Hakika kwenye dhiki kuna faraji فَإِذَا فَرَغۡتَ فَٱنصَبۡ ٧Basi utakapomaliza mambo ya kidunia na shughuli zake jipinde kwa kufanya ibada وَإِلَىٰ رَبِّكَ فَٱرۡغَب ٨Na kwa Mola wako Peke Yake weka matumaini yako

Translation: Abdullah Muhammad Abu Bakr.