بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
إِذَا ٱلشَّمۡسُ كُوِّرَتۡ ١Pindi jua litakapokunjwa, na mwangaza wake ukaondoka وَإِذَا ٱلنُّجُومُ ٱنكَدَرَتۡ ٢Na pindi nyota zitakapopuputika na nuru yake ikafutika وَإِذَا ٱلۡجِبَالُ سُيِّرَتۡ ٣Na pindi majabali yatakapoondoshawa kwenye uso wa ardhi yakawa ni vumbi linaloenea وَإِذَا ٱلۡعِشَارُ عُطِّلَتۡ ٤Na pindi ngamia wenye mimba watakapoachwa na kupuuzwa وَإِذَا ٱلۡوُحُوشُ حُشِرَتۡ ٥Na pindi wanyama mwitu watakapokusanywa na kutangamanishwa, ili Mwenyezi Mungu Awape nafasi ya kulipizana wao kwa wao وَإِذَا ٱلۡبِحَارُ سُجِّرَتۡ ٦Na pindi bahari zitakapowashwa moto zikawa ni moto unaowaka وَإِذَا ٱلنُّفُوسُ زُوِّجَتۡ ٧Na pindi nafsi zitakapokutanishwa na mfano wake na sampuli yake وَإِذَا ٱلۡمَوۡءُۥدَةُ سُئِلَتۡ ٨Na pindi mtoto wa kike aliyezikwa akiwa hai atakapoulizwa, Siku ya Kiyama, suala la kumbembeleza na kumkejeli aliyemzika بِأَيِّ ذَنۢبٍ قُتِلَتۡ ٩ni kwa dhambi gani ilikuwa kuzikwa kwake وَإِذَا ٱلصُّحُفُ نُشِرَتۡ ١٠Na pindi kurasa za matendo zitakapoonyeshwa وَإِذَا ٱلسَّمَآءُ كُشِطَتۡ ١١Na pindi mbingu zitakapong’olewa na kuondoshwa zilipokuwa وَإِذَا ٱلۡجَحِيمُ سُعِّرَتۡ ١٢Na pindi Moto utakapowashwa na ukawaka وَإِذَا ٱلۡجَنَّةُ أُزۡلِفَتۡ ١٣Na pindi Pepo , Nyumba ya Neema, itakaposongezewa watu wake wachamungu عَلِمَتۡ نَفۡسٌ مَّآ أَحۡضَرَتۡ ١٤Litakapotokea hilo, itayakinisha kila nafsi na kujua kile ilichokitanguliza cha kheri au shari فَلَآ أُقۡسِمُ بِٱلۡخُنَّسِ ١٥Anaapa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa nyota zinazofichika nuru yake mchana ٱلۡجَوَارِ ٱلۡكُنَّسِ ١٦zinazotembea na zinazoghibu katika anga zake وَٱلَّيۡلِ إِذَا عَسۡعَسَ ١٧Na Anaapa kwa usiku unapojitokeza na giza lake وَٱلصُّبۡحِ إِذَا تَنَفَّسَ ١٨Na kwa asubuhi unapojitokeza mwangaza wake إِنَّهُۥ لَقَوۡلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ ١٩Hakika Qur’ani ni ujumbe wa mjumbe mtukufu , naye ni Jibrili, amani imshukike ذِي قُوَّةٍ عِندَ ذِي ٱلۡعَرۡشِ مَكِينٍ ٢٠Mwenye nguvu katika kuyapitisha yale anayoamrishwa. Mwenye cheo cha juu kwa Mwenyezi Mungu. Anayesikilizwa na Malaika مُّطَاعٍ ثَمَّ أَمِينٍ ٢١Anayeaminiwa juu ya Wahyi anaoteremka nao وَمَا صَاحِبُكُم بِمَجۡنُونٍ ٢٢Hakuwa Muhammad mnayemjua ni mwendawazimu وَلَقَدۡ رَءَاهُ بِٱلۡأُفُقِ ٱلۡمُبِينِ ٢٣Na kwa hakika Muhammad alimuona Jibrili anayemjia na utume katika pambizo kubwa وَمَا هُوَ عَلَى ٱلۡغَيۡبِ بِضَنِينٍ ٢٤Wala yeye hafanyi ubakhili katika kufikisha Wahyi وَمَا هُوَ بِقَوۡلِ شَيۡطَٰنٍ رَّجِيمٍ ٢٥Wala haikuwa hii Qur’ani ni neno la Shetani aliyefukuzwa na kutolewa kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu. Lakini Qur’ani hii ni maneno ya Mwenyezi Mungu na ni Wahyi wake فَأَيۡنَ تَذۡهَبُونَ ٢٦Akili zenu zawapeleka wapi katika kukanusha baada ya hoja hizi zilizo wazi na zenye nguvu إِنۡ هُوَ إِلَّا ذِكۡرٌ لِّلۡعَٰلَمِينَ ٢٧Hayakuwa haya isipokuwa ni mawaidha kutoka kwa Mwenyezi Mungu yanapewa watu wote لِمَن شَآءَ مِنكُمۡ أَن يَسۡتَقِيمَ ٢٨Kwa atakaye, kati yenu, kulingana juu ya haki na Imani وَمَا تَشَآءُونَ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ رَبُّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ٢٩Wala nyinyi hamtotaka isipokuwa kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe wote