Millat al-Islam

Chapter 89 · 30 verses · Ali Muhsin Al Barwani

Surah Al-Fajr in Swahili

Arabic with tafsir Listen to Surah Al-Fajr (1331 reciters)
Meccanسورة الفجر30 verses

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلۡفَجۡرِ ١Naapa kwa alfajiri وَلَيَالٍ عَشۡرٍ ٢Na kwa masiku kumi وَٱلشَّفۡعِ وَٱلۡوَتۡرِ ٣Na kwa viwili viwili na kimoja kimoja وَٱلَّيۡلِ إِذَا يَسۡرِ ٤Na kwa usiku unapo pita هَلۡ فِي ذَٰلِكَ قَسَمٌ لِّذِي حِجۡرٍ ٥Je! Hapana katika haya kiapo kwa mwenye akili أَلَمۡ تَرَ كَيۡفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِعَادٍ ٦Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo wafanya kina A'di إِرَمَ ذَاتِ ٱلۡعِمَادِ ٧Wa Iram, wenye majumba marefu ٱلَّتِي لَمۡ يُخۡلَقۡ مِثۡلُهَا فِي ٱلۡبِلَٰدِ ٨Ambao haukuumbwa mfano wake katika nchi وَثَمُودَ ٱلَّذِينَ جَابُواْ ٱلصَّخۡرَ بِٱلۡوَادِ ٩Na Thamudi walio chonga majabali huko bondeni وَفِرۡعَوۡنَ ذِي ٱلۡأَوۡتَادِ ١٠Na Firauni mwenye vigingi ٱلَّذِينَ طَغَوۡاْ فِي ٱلۡبِلَٰدِ ١١Ambao walifanya jeuri katika nchi فَأَكۡثَرُواْ فِيهَا ٱلۡفَسَادَ ١٢Wakakithirisha humo ufisadi فَصَبَّ عَلَيۡهِمۡ رَبُّكَ سَوۡطَ عَذَابٍ ١٣Basi Mola wako Mlezi aliwapiga mjeledi wa adhabu إِنَّ رَبَّكَ لَبِٱلۡمِرۡصَادِ ١٤Hakika Mola wako Mlezi yupo kwenye mavizio anawavizia فَأَمَّا ٱلۡإِنسَٰنُ إِذَا مَا ٱبۡتَلَىٰهُ رَبُّهُۥ فَأَكۡرَمَهُۥ وَنَعَّمَهُۥ فَيَقُولُ رَبِّيٓ أَكۡرَمَنِ ١٥Ama mtu anapo jaribiwa na Mola wake Mlezi, akamkirimu na akamneemesha, husema: Mola wangu Mlezi amenikirimu وَأَمَّآ إِذَا مَا ٱبۡتَلَىٰهُ فَقَدَرَ عَلَيۡهِ رِزۡقَهُۥ فَيَقُولُ رَبِّيٓ أَهَٰنَنِ ١٦Na ama anapo mjaribu akampunguzia riziki yake, husema: Mola wangu Mlezi amenitia unyonge كـَلَّاۖ بَل لَّا تُكۡرِمُونَ ٱلۡيَتِيمَ ١٧Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima وَلَا تَحَٰٓضُّونَ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ ١٨Wala hamhimizani kulisha masikini وَتَأۡكُلُونَ ٱلتُّرَاثَ أَكۡلًا لَّمًّا ١٩Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa وَتُحِبُّونَ ٱلۡمَالَ حُبًّا جَمًّا ٢٠Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi كـَلَّآۖ إِذَا دُكَّتِ ٱلۡأَرۡضُ دَكًّا دَكًّا ٢١Sivyo hivyo! Itakapo vunjwa ardhi vipande vipande وَجَآءَ رَبُّكَ وَٱلۡمَلَكُ صَفًّا صَفًّا ٢٢Na akaja Mola wako Mlezi na Malaika safu safu وَجِاْيٓءَ يَوۡمَئِذِۭ بِجَهَنَّمَۚ يَوۡمَئِذٍ يَتَذَكَّرُ ٱلۡإِنسَٰنُ وَأَنَّىٰ لَهُ ٱلذِّكۡرَىٰ ٢٣Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo, siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini يَقُولُ يَٰلَيۡتَنِي قَدَّمۡتُ لِحَيَاتِي ٢٤Atasema: Laiti ningeli jitangulizia kwa uhai wangu فَيَوۡمَئِذٍ لَّا يُعَذِّبُ عَذَابَهُۥٓ أَحَدٌ ٢٥Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu kwake وَلَا يُوثِقُ وَثَاقَهُۥٓ أَحَدٌ ٢٦Wala hatafunga yeyote kama kufunga kwake يَٰٓأَيَّتُهَا ٱلنَّفۡسُ ٱلۡمُطۡمَئِنَّةُ ٢٧Ewe nafsi iliyo tua ٱرۡجِعِيٓ إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةً مَّرۡضِيَّةً ٢٨Rejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika, na umemridhisha فَٱدۡخُلِي فِي عِبَٰدِي ٢٩Basi ingia miongoni mwa waja wangu وَٱدۡخُلِي جَنَّتِي ٣٠Na ingia katika Pepo yangu

Translation: Ali Muhsin Al Barwani.