Millat al-Islam

Chapter 84 · 25 verses · Ali Muhsin Al Barwani

Surah Al-Inshiqaq in Swahili

Arabic with tafsir Listen to Surah Al-Inshiqaq (1262 reciters)

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنشَقَّتۡ ١Itapo chanika mbingu وَأَذِنَتۡ لِرَبِّهَا وَحُقَّتۡ ٢Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza وَإِذَا ٱلۡأَرۡضُ مُدَّتۡ ٣Na ardhi itakapo tanuliwa وَأَلۡقَتۡ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتۡ ٤Na kuvitoa vilivyo kuwa ndani yake, ikawa tupu وَأَذِنَتۡ لِرَبِّهَا وَحُقَّتۡ ٥Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡإِنسَٰنُ إِنَّكَ كَادِحٌ إِلَىٰ رَبِّكَ كَدۡحًا فَمُلَٰقِيهِ ٦Ewe mtu! Hakika wewe unajikusuru kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta فَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ ٧Ama atakaye pewa daftari lake kwa mkono wa kulia فَسَوۡفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا ٨Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi وَيَنقَلِبُ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ مَسۡرُورًا ٩Na arudi kwa ahali zake na furaha وَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ وَرَآءَ ظَهۡرِهِۦ ١٠Na ama atakaye pewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake فَسَوۡفَ يَدۡعُواْ ثُبُورًا ١١Basi huyo ataomba kuteketea وَيَصۡلَىٰ سَعِيرًا ١٢Na ataingia Motoni إِنَّهُۥ كَانَ فِيٓ أَهۡلِهِۦ مَسۡرُورًا ١٣Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake إِنَّهُۥ ظَنَّ أَن لَّن يَحُورَ ١٤Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena بَلَىٰٓۚ إِنَّ رَبَّهُۥ كَانَ بِهِۦ بَصِيرًا ١٥Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona فَلَآ أُقۡسِمُ بِٱلشَّفَقِ ١٦Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapo kuchwa وَٱلَّيۡلِ وَمَا وَسَقَ ١٧Na kwa usiku na unavyo vikusanya وَٱلۡقَمَرِ إِذَا ٱتَّسَقَ ١٨Na kwa mwezi unapo pevuka لَتَرۡكَبُنَّ طَبَقًا عَن طَبَقٍ ١٩Lazima mtapanda t'abaka kwa t'abaka فَمَا لَهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ ٢٠Basi wana nini hawaamini وَإِذَا قُرِئَ عَلَيۡهِمُ ٱلۡقُرۡءَانُ لَا يَسۡجُدُونَۤ ۩ ٢١Na wanapo somewa Qur'ani hawasujudu بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يُكَذِّبُونَ ٢٢Bali walio kufuru wanakanusha tu وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا يُوعُونَ ٢٣Na Mwenyezi Mungu anajua wanayo yadhamiria فَبَشِّرۡهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ٢٤Basi wabashirie adhabu chungu إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَهُمۡ أَجۡرٌ غَيۡرُ مَمۡنُونِۭ ٢٥Isipo kuwa wale walio amini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usio malizika

Translation: Ali Muhsin Al Barwani.