ملة الإسلام

السورة 93 · 11 آية · Abdullah Muhammad Abu Bakr

سورة الضحى باللغة السواحلية

السورة بالعربية مع التفسير استمع إلى سورة الضحى (1,350 قارئاً)
مكيةسورة الضحى١١ آية

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلضُّحَىٰ ١Mwenyezi Mungu Anaapa kwa wakati wa dhuha, na uliokusudiwa ni wakati wa mchana mzima وَٱلَّيۡلِ إِذَا سَجَىٰ ٢Na kwa usiku utuliapo na viumbe na likashadidi giza lake. Mwenyezi Mungu Huapa kwa Atakacho katika viumbe vyake. Ama kiumbe, hafai kuapa kwa asiyekuwa Muumba wake. Kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni ushirikina مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ ٣Hakukuwacha Mola wako, ewe Mtume, wala Hakukuchukia kwa kuchelewesha kukuteremshiaWahyi وَلَلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٌ لَّكَ مِنَ ٱلۡأُولَىٰ ٤Na Nyumba ya Akhera ni bora kwako kuliko nyumba ya ulimwengu وَلَسَوۡفَ يُعۡطِيكَ رَبُّكَ فَتَرۡضَىٰٓ ٥Na Atakupa Mola wako, ewe Mtume, neema ya kila sampuli uridhike أَلَمۡ يَجِدۡكَ يَتِيمًا فَـَٔاوَىٰ ٦Kwani Hakukupata, kabla ya hapo, kuwa ni yatima Akakukusanya na kukutunza وَوَجَدَكَ ضَآلًّا فَهَدَىٰ ٧Na Akakupata hujui Kitabu wala Imani, Akakufundisha yale amabayo ulikuwa huyajui na akakuafikia kufanya amali bora وَوَجَدَكَ عَآئِلًا فَأَغۡنَىٰ ٨Na Akakupata masikini, Akakuletea riziki yako na Akakutajirisha kwa kutosheka na kusubiri فَأَمَّا ٱلۡيَتِيمَ فَلَا تَقۡهَرۡ ٩Basi yatima usimtende ubaya وَأَمَّا ٱلسَّآئِلَ فَلَا تَنۡهَرۡ ١٠Na muombaji usimkaripie, bali mlishe na umtimizie haja yake وَأَمَّا بِنِعۡمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثۡ ١١Na ama neema ya Mola wako Aliyokuneemesha nayo izungumze

الترجمة: Abdullah Muhammad Abu Bakr.