بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡمُدَّثِّرُ ١Ewe uliojifinika nguo zako قُمۡ فَأَنذِرۡ ٢Inuka kutoka kwenye malazi yako owaonye watu adhabu ya Menyezi Mungu وَرَبَّكَ فَكَبِّرۡ ٣Na umkusudie Mola wako, Peke Yake, kwa kumtukuza, kumpwekesha na kumuabudu وَثِيَابَكَ فَطَهِّرۡ ٤Na usafishe nguo zako kutokana na najisi, kwani usafi wa nje ni katika kutimia usafi wa ndani وَٱلرُّجۡزَ فَٱهۡجُرۡ ٥Na uendelee daima kuyaepuka masanamu na mizimu, na matendo ya ushirikina yote usiyakaribie وَلَا تَمۡنُن تَسۡتَكۡثِرُ ٦Na usitoe kitu kumpa mtu kwa lengo la kupata zaidi ya hiko. Na kwa ajili ya kupata radhi ya Mwenyezi Mungu وَلِرَبِّكَ فَٱصۡبِرۡ ٧vumilia juu ya maamrisho na makatazo فَإِذَا نُقِرَ فِي ٱلنَّاقُورِ ٨Pindi patakapopulizwa kwenye barugumu mpulizo wa Ufufuzi na Uenezaji فَذَٰلِكَ يَوۡمَئِذٍ يَوۡمٌ عَسِيرٌ ٩wakati huo ni wakati ambao ni mgumu kwa makafiri عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ غَيۡرُ يَسِيرٍ ١٠si rahisi kwao kusalimika na yale walionayo ya kujadiliwa hesabu zao na vituko vingine vikubwa ذَرۡنِي وَمَنۡ خَلَقۡتُ وَحِيدًا ١١Niache mimi, ewe Mtume, na huyu niliyemuumba ndani ya tumbo la mamake akiwa peke yake, hana mali wala watoto وَجَعَلۡتُ لَهُۥ مَالًا مَّمۡدُودًا ١٢Nikamfanya awe na mali mengi yenye kuenea na watoto waliyoko na yeye hapo Makkah hawamuondokei. Na وَبَنِينَ شُهُودًا ١٣nikamsahilishia kwa kumrahisishia njia za maisha. Kisha yeye anatarajia, baada ya vitu hivi alivyopewa وَمَهَّدتُّ لَهُۥ تَمۡهِيدًا ١٤nimuongezee kwenye mali yake na watoto wake na huku yeye amenikanusha. Mambo sivyo kama anavyodai huyu mwenye kuasi, mtenda dhambi ثُمَّ يَطۡمَعُ أَنۡ أَزِيدَ ١٥Simuongezei zaidi ya hiko nilichompa كـَلَّآۖ إِنَّهُۥ كَانَ لِأٓيَٰتِنَا عَنِيدًا ١٦kwa kuwa yeye alikuwa mshindani mkanushaji wa Qur’ani na hoja za Mwenyezi Mungu kwa viumbe Wake سَأُرۡهِقُهُۥ صَعُودًا ١٧Nitambebesha mateso magumu na usumbufu usio na mapumziko. Anayekusudiwa hapa ni Al-Walid mwana wa Al-Mughi rah aliyekuwa akishindana na haki na akijitokeza kupigana vita na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Haya ndiyo malipo ya kila mwenye kushindana na haki na kuipiga vita إِنَّهُۥ فَكَّرَ وَقَدَّرَ ١٨Kwa kweli yeye aliwaza ndani ya nafsi yake akatayarisha la kusema kumtukana Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na Qur’ani فَقُتِلَ كَيۡفَ قَدَّرَ ١٩Hivyo basi akalaaniwa na akastahili, kwa hilo, maangamivu: alijiandaa vipi ndani ya nafsi yake kwa hayo matukano ثُمَّ قُتِلَ كَيۡفَ قَدَّرَ ٢٠Kisha pia akalaaniwa ثُمَّ نَظَرَ ٢١Kisha yeye alifikiria kuhusu kile alichokipanga na kukitayarisha cha kuitia dosari Qur’ani ثُمَّ عَبَسَ وَبَسَرَ ٢٢Kisha akafinya uso wake na akazidi katika hali ile ya ukunjaji uso kwa kukosa hila za kufanya na kutopata ila yoyote ya kuitia dosari Qur’ani ثُمَّ أَدۡبَرَ وَٱسۡتَكۡبَرَ ٢٣Kisha akarudi kuipa mgongo haki na akajiona ni mkubwa wa kutofaa kuikubali فَقَالَ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا سِحۡرٌ يُؤۡثَرُ ٢٤hapo akasema kuhusu Qur’ani, «Haya anayoyasema Muhammad si chochote isipokuwa ni uchawi uliopokewa kutoka kwa watu wa mwanzo waliopita إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا قَوۡلُ ٱلۡبَشَرِ ٢٥Haikuwa hi Qur’ani isipokuwa ni maneno ya viumbe ambayo Muhammad amejifunza kutoka kwao kisha akadai kuwa yanatoka kwa Mwenyezi Mungu.» سَأُصۡلِيهِ سَقَرَ ٢٦Basi nitamuingiza kwenye moto wa Jahanamu ili alionje joto lake na achomeke kwa moto wake وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا سَقَرُ ٢٧Na ni lipi lililokujulisha wewe ni kitu gani hiyo Jahanamu لَا تُبۡقِي وَلَا تَذَرُ ٢٨Haibakishi nyama wala haiachi mfupa isipokuwa huvichoma لَوَّاحَةٌ لِّلۡبَشَرِ ٢٩Unageuza ngozi ya mwili, unazifanya ngozi kuwa nyeusi na unazichoma عَلَيۡهَا تِسۡعَةَ عَشَرَ ٣٠Wanasimamia mambo yake na kushikilia kazi ya kuwatesa watu wake Malaika kumi na tisa katika washika zamu wa Motoni wenye nguvu وَمَا جَعَلۡنَآ أَصۡحَٰبَ ٱلنَّارِ إِلَّا مَلَٰٓئِكَةًۖ وَمَا جَعَلۡنَا عِدَّتَهُمۡ إِلَّا فِتۡنَةً لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ لِيَسۡتَيۡقِنَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ وَيَزۡدَادَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِيمَٰنًا وَلَا يَرۡتَابَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَ وَلِيَقُولَ ٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ وَٱلۡكَٰفِرُونَ مَاذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِهَٰذَا مَثَلًاۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ ٱللَّهُ مَن يَشَآءُ وَيَهۡدِي مَن يَشَآءُۚ وَمَا يَعۡلَمُ جُنُودَ رَبِّكَ إِلَّا هُوَۚ وَمَا هِيَ إِلَّا ذِكۡرَىٰ لِلۡبَشَرِ ٣١Na hatukuwafanya washika hazina wa Motoni isipokuwa miongoni mwa Malaika washupavu. Na hatukuiweka idadi hiyo isipokuwa kuwatahini wale waliomkufuru Mwenyezi Mungu, na ili imani ya yakini ipatikane kwa wale Mayahudi na Wanaswara waliopewa Vitabu kwamba yaliyokuja ndani ya Qur’ani juu ya washika hazina wa Motoni ni ukweli utokao kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, kwani hayo yanaafikiana na vitabu vyao, na ili Waumini wazidi kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na waifuate Sheria Yake kivitendo, na ili wasilifanyie shaka hilo wale Mayahudi na Wanaswara waliopewa Vitabu wala wale wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na ili wapate kusema wale wenye unafiki ndani ya nyoyo zao na makafiri, «Ni lipi alilolikusudia Mwenyezi Mungu kwa idadi hii ya ajabu?» Kwa mfano wa hayo yaliyotajwa, Mwenyezi Mungu Anampoteza Anayetaka kumpoteza na Anamuongoza Anayetaka kumuongoza. Na hakuna ajuwaye idadi ya askari wa Mola wako, na miongoni mwao ni Malaika, isipokuwa Mwenyezi Mungu Peke Yake. Na haukuwa huu Moto isipokuwa ni ukumbusho na mazingatio kwa watu كـَلَّا وَٱلۡقَمَرِ ٣٢Mambo sivyo kama walivyotaja ya ukanushaji Mtume katika yale aliyokuja nayo! Anaapa Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu, kwa mwezi وَٱلَّيۡلِ إِذۡ أَدۡبَرَ ٣٣na kwa usiku unapogeuka kwenda zake وَٱلصُّبۡحِ إِذَآ أَسۡفَرَ ٣٤na kwa asubuhi inapotoa mwangaza na kufunuka إِنَّهَا لَإِحۡدَى ٱلۡكُبَرِ ٣٥hakika Moto ni mojawapo ya mambo makubwa نَذِيرًا لِّلۡبَشَرِ ٣٦kwa ajili ya kuwaonya na kuwatisha watu لِمَن شَآءَ مِنكُمۡ أَن يَتَقَدَّمَ أَوۡ يَتَأَخَّرَ ٣٧kwa anayetaka miongoni mwenu kujiweka karibu na Mola wake kwa kufanya matendo ya utiifu, au kujikalisha nyuma kwa kufanya matendo ya uasi كُلُّ نَفۡسِۭ بِمَا كَسَبَتۡ رَهِينَةٌ ٣٨Kila nafsi imefungwa na kuwekwa rahani kwa ilichokitenda, miongoni mwa matendo mema au mabaya, kwa kukichuma. Haifunguliwi mpaka itekeleze haki zilizo juu ya lazima yake na ipatiwe mateso yanayostahili kupatiwa إِلَّآ أَصۡحَٰبَ ٱلۡيَمِينِ ٣٩Isipokuwa Waislamu waliotakaswa, watu wa upande wa kulia waliojikomboa shingo zao kwa utiifu فِي جَنَّٰتٍ يَتَسَآءَلُونَ ٤٠Wao watakuwa kwenye mabustani ya Peponi ambayo sifa zake hazifikiwi ukomo. Watakuwa wakiulizana wao kwa wao عَنِ ٱلۡمُجۡرِمِينَ ٤١kuhusu makafiri waliojikosea nafsi zao مَا سَلَكَكُمۡ فِي سَقَرَ ٤٢«Ni lipi lililowaingiza kwenye moto wa Jahanamu na likawafanya قَالُواْ لَمۡ نَكُ مِنَ ٱلۡمُصَلِّينَ ٤٣mlionje joto lake lililo kali sana?» Wahalifu waseme , «Hatukuwa ni miongoni mwa wanaoswali duniani وَلَمۡ نَكُ نُطۡعِمُ ٱلۡمِسۡكِينَ ٤٤na hatukuwa tukitoa sadaka na kuwafanyia wema wahitaji na maskini وَكُنَّا نَخُوضُ مَعَ ٱلۡخَآئِضِينَ ٤٥na tulikuwa tukizungumza maneno ya ubatilifu na watu wa upotofu na upotevu وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوۡمِ ٱلدِّينِ ٤٦na tulikuwa tukiikanusha Siku ya kuhesabiwa na kulipwa حَتَّىٰٓ أَتَىٰنَا ٱلۡيَقِينُ ٤٧mpaka kifo kikatujia na hali sisi tuko kwenye mambo hayo mabaya ya upotevu فَمَا تَنفَعُهُمۡ شَفَٰعَةُ ٱلشَّٰفِعِينَ ٤٨Basi hayatawafalia neno maombezi ya wenye kuombea wote, miongoni mwa Malaika, Manabii na wengineo, kwa kuwa aombewaye ni yule aliyechaguliwa na Mwenyezi Mungu na akamuidhinisha mwenye kumuombea فَمَا لَهُمۡ عَنِ ٱلتَّذۡكِرَةِ مُعۡرِضِينَ ٤٩Basi wana nini hawa washirikina wamejiepusha na Qur’ani na كَأَنَّهُمۡ حُمُرٌ مُّسۡتَنفِرَةٌ ٥٠mawaidha yaliyomo ndani yake? Kama kwamba wao ni pundamilia wanaobabaika فَرَّتۡ مِن قَسۡوَرَةِۭ ٥١wanaomkimbia simba mshambulizi بَلۡ يُرِيدُ كُلُّ ٱمۡرِيٍٕ مِّنۡهُمۡ أَن يُؤۡتَىٰ صُحُفًا مُّنَشَّرَةً ٥٢Lakini kila mmoja, miongoni mwa hawa washirikina, ana matumaini ateremshiwe kitabu kutoka mbinguni kilichokunjuliwa kama kile kilichoteremshiwa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie كـَلَّاۖ بَل لَّا يَخَافُونَ ٱلۡأٓخِرَةَ ٥٣Mambo si hivyo kama wanavyodai. Ukweli ni kwamba wao hawaiogopi Akhera wala hawaamini kuwa kuna kufufuliwa na kulipwa كـَلَّآ إِنَّهُۥ تَذۡكِرَةٌ ٥٤Ni kweli kwamba Qur’ani ni mawaidha yenye ufasaha, yanayotosha kuwafanya wao wawaidhike فَمَن شَآءَ ذَكَرَهُۥ ٥٥Anayetaka kuwaidhika, basi na awaidhike kwa yaliyomo ndani yake na anufaike na uongofu wake وَمَا يَذۡكُرُونَ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُۚ هُوَ أَهۡلُ ٱلتَّقۡوَىٰ وَأَهۡلُ ٱلۡمَغۡفِرَةِ ٥٦Na hawawaidhiki kwayo isipokuwa iwapo Mwenyezi Mungu Amewatakia kuongoka. Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Anayestahiki kuogopewa na kutiiwa, na Ndiye Anayestahiki kumsamehe anayemuamini Yeye na kumtii