ملة الإسلام

السورة 44 · 59 آية · Ali Muhsin Al Barwani

سورة الدخان باللغة السواحلية

السورة بالعربية مع التفسير استمع إلى سورة الدخان (1,230 قارئاً)
مكيةسورة الدخان٥٩ آية

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

حمٓ ١H'a Mim وَٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡمُبِينِ ٢Naapa kwa Kitabu kinacho bainisha إِنَّآ أَنزَلۡنَٰهُ فِي لَيۡلَةٍ مُّبَٰرَكَةٍۚ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ ٣Hakika tumekiteremsha katika usiku ulio barikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji فِيهَا يُفۡرَقُ كُلُّ أَمۡرٍ حَكِيمٍ ٤Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hikima أَمۡرًا مِّنۡ عِندِنَآۚ إِنَّا كُنَّا مُرۡسِلِينَ ٥Jambo litokalo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma رَحۡمَةً مِّن رَّبِّكَۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ ٦Ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia Mwenye kujua رَبِّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَآۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ ٧Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, ikiwa nyinyi mna yakini لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۖ رَبُّكُمۡ وَرَبُّ ءَابَآئِكُمُ ٱلۡأَوَّلِينَ ٨Hakuna mungu ila Yeye; anahuisha na anafisha- Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa mwanzo بَلۡ هُمۡ فِي شَكٍّ يَلۡعَبُونَ ٩Lakini wao wanacheza katika shaka فَٱرۡتَقِبۡ يَوۡمَ تَأۡتِي ٱلسَّمَآءُ بِدُخَانٍ مُّبِينٍ ١٠Basi ingoje siku ambayo mbingu zitakapo leta moshi ulio dhaahiri يَغۡشَى ٱلنَّاسَۖ هَٰذَا عَذَابٌ أَلِيمٌ ١١Utakao wafunika watu: Hii ni adhabu chungu رَّبَّنَا ٱكۡشِفۡ عَنَّا ٱلۡعَذَابَ إِنَّا مُؤۡمِنُونَ ١٢Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini أَنَّىٰ لَهُمُ ٱلذِّكۡرَىٰ وَقَدۡ جَآءَهُمۡ رَسُولٌ مُّبِينٌ ١٣Nini faida ya kukumbuka kwao? Na alikwisha wafikia Mtume mwenye kubainisha ثُمَّ تَوَلَّوۡاْ عَنۡهُ وَقَالُواْ مُعَلَّمٌ مَّجۡنُونٌ ١٤Na wao wakamgeuzia uso, na wakasema: Huyu amefunzwa, naye ni mwendawazimu إِنَّا كَاشِفُواْ ٱلۡعَذَابِ قَلِيلًاۚ إِنَّكُمۡ عَآئِدُونَ ١٥Hakika sisi tutaiondoa adhabu kidogo, lakini nyinyi kwa yakini mtarejea vile vile يَوۡمَ نَبۡطِشُ ٱلۡبَطۡشَةَ ٱلۡكُبۡرَىٰٓ إِنَّا مُنتَقِمُونَ ١٦Siku tutayo yashambulia mashambulio makubwa, bila ya shaka Sisi ni wenye kutesa ۞ وَلَقَدۡ فَتَنَّا قَبۡلَهُمۡ قَوۡمَ فِرۡعَوۡنَ وَجَآءَهُمۡ رَسُولٌ كَرِيمٌ ١٧Na hakika kabla ya hawa tuliwafanyia mtihani watu wa Firauni, na aliwafikia Mtume Mtukufu أَنۡ أَدُّوٓاْ إِلَيَّ عِبَادَ ٱللَّهِۖ إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٌ ١٨Akasema: Nipeni waja wa Mwenyezi Mungu; kwa hakika mimi kwenu ni Mtume Muaminifu وَأَن لَّا تَعۡلُواْ عَلَى ٱللَّهِۖ إِنِّيٓ ءَاتِيكُم بِسُلۡطَٰنٍ مُّبِينٍ ١٩Na msimfanyie kiburi Mwenyezi Mungu; hakika mimi nitakuleteeni uthibitisho ulio wazi وَإِنِّي عُذۡتُ بِرَبِّي وَرَبِّكُمۡ أَن تَرۡجُمُونِ ٢٠Nami najikinga kwa Mola wangu Mlezi na ndiye Mola wenu Mlezi pia, ili msinipige mawe وَإِن لَّمۡ تُؤۡمِنُواْ لِي فَٱعۡتَزِلُونِ ٢١Na ikiwa hamniamini, basi jitengeni nami فَدَعَا رَبَّهُۥٓ أَنَّ هَٰٓؤُلَآءِ قَوۡمٌ مُّجۡرِمُونَ ٢٢Ndipo akamwomba Mola wake Mlezi: Hakika watu hawa ni wakosefu فَأَسۡرِ بِعِبَادِي لَيۡلًا إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ ٢٣Mwenyezi Mungu akasema: Basi nenda na waja wangu usiku. Kwa yakini mtafuatwa وَٱتۡرُكِ ٱلۡبَحۡرَ رَهۡوًاۖ إِنَّهُمۡ جُندٌ مُّغۡرَقُونَ ٢٤Na iache bahari vivyo hivyo imeachana, hakika wao hao ni jeshi litakalo zamishwa كَمۡ تَرَكُواْ مِن جَنَّٰتٍ وَعُيُونٍ ٢٥Mabustani mangapi, na chemchem ngapi waliziacha وَزُرُوعٍ وَمَقَامٍ كَرِيمٍ ٢٦Na mimea na vyeo vitukufu وَنَعۡمَةٍ كَانُواْ فِيهَا فَٰكِهِينَ ٢٧Na neema walizo kuwa wakijistareheshea كَذَٰلِكَۖ وَأَوۡرَثۡنَٰهَا قَوۡمًا ءَاخَرِينَ ٢٨Ndio hivyo! Na tukawarithisha haya watu wenginewe فَمَا بَكَتۡ عَلَيۡهِمُ ٱلسَّمَآءُ وَٱلۡأَرۡضُ وَمَا كَانُواْ مُنظَرِينَ ٢٩La mbingu wala ardhi hazikuwalilia, wala hawakupewa muhula وَلَقَدۡ نَجَّيۡنَا بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ مِنَ ٱلۡعَذَابِ ٱلۡمُهِينِ ٣٠Na bila ya shaka tuliwaokoa Wana wa Israili katika adhabu ya kuwadhalilisha مِن فِرۡعَوۡنَۚ إِنَّهُۥ كَانَ عَالِيًا مِّنَ ٱلۡمُسۡرِفِينَ ٣١Ya Firauni. Hakika yeye alikuwa jeuri katika wenye kupindukia mipaka وَلَقَدِ ٱخۡتَرۡنَٰهُمۡ عَلَىٰ عِلۡمٍ عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ ٣٢Na tuliwakhiari kwa ujuzi wetu kuliko walimwengu wenginewe وَءَاتَيۡنَٰهُم مِّنَ ٱلۡأٓيَٰتِ مَا فِيهِ بَلَٰٓؤٌاْ مُّبِينٌ ٣٣Na tukawapa katika ishara zenye majaribio yaliyo wazi إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ لَيَقُولُونَ ٣٤Hakika hawa wanasema إِنۡ هِيَ إِلَّا مَوۡتَتُنَا ٱلۡأُولَىٰ وَمَا نَحۡنُ بِمُنشَرِينَ ٣٥Hapana ila kufa kwetu mara ya kwanza tu, wala sisi hatufufuliwi فَأۡتُواْ بِـَٔابَآئِنَآ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ ٣٦Basi warudisheni baba zetu, ikiwa nyinyi mnasema kweli أَهُمۡ خَيۡرٌ أَمۡ قَوۡمُ تُبَّعٍ وَٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ أَهۡلَكۡنَٰهُمۡۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ مُجۡرِمِينَ ٣٧Je! Ni wao bora au watu wa Tubbaa' na walio kuwa kabla yao? Tuliwaangamiza. Hakika hao walikuwa wakosefu وَمَا خَلَقۡنَا ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَا لَٰعِبِينَ ٣٨Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo baina yake kwa mchezo مَا خَلَقۡنَٰهُمَآ إِلَّا بِٱلۡحَقِّ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ ٣٩Hatukuviumba hivyo ila kwa Haki, lakini wengi wao hawajui إِنَّ يَوۡمَ ٱلۡفَصۡلِ مِيقَٰتُهُمۡ أَجۡمَعِينَ ٤٠Hakika siku ya Uamuzi ni wakati ulio wekwa kwa wao wote يَوۡمَ لَا يُغۡنِي مَوۡلًى عَن مَّوۡلًى شَيۡـًٔا وَلَا هُمۡ يُنصَرُونَ ٤١Siku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote, wala hawatanusuriwa إِلَّا مَن رَّحِمَ ٱللَّهُۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ ٤٢Isipo kuwa atakaye mrehemu Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu إِنَّ شَجَرَتَ ٱلزَّقُّومِ ٤٣Hakika Mti wa Zaqqum طَعَامُ ٱلۡأَثِيمِ ٤٤Ni chakula cha mwenye dhambi كَٱلۡمُهۡلِ يَغۡلِي فِي ٱلۡبُطُونِ ٤٥Kama shaba iliyo yayushwa, hutokota matumboni كَغَلۡيِ ٱلۡحَمِيمِ ٤٦Kama kutokota kwa maji ya moto خُذُوهُ فَٱعۡتِلُوهُ إِلَىٰ سَوَآءِ ٱلۡجَحِيمِ ٤٧(Itasemwa:) Mkamateni na mtupeni katikati ya Jahannamu ثُمَّ صُبُّواْ فَوۡقَ رَأۡسِهِۦ مِنۡ عَذَابِ ٱلۡحَمِيمِ ٤٨Kisha mmwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji yanayo chemka ذُقۡ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡكَرِيمُ ٤٩Onja! Ati wewe ndiye mwenye nguvu, mtukufu إِنَّ هَٰذَا مَا كُنتُم بِهِۦ تَمۡتَرُونَ ٥٠Hakika haya ndiyo mliyo kuwa mkiyatilia shaka إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي مَقَامٍ أَمِينٍ ٥١Hakika wachamngu watakuwa katika mahali pa amani فِي جَنَّٰتٍ وَعُيُونٍ ٥٢Katika mabustani na chemchem يَلۡبَسُونَ مِن سُندُسٍ وَإِسۡتَبۡرَقٍ مُّتَقَٰبِلِينَ ٥٣Watavaa hariri nyepesi na hariri nzito wakikabiliana كَذَٰلِكَ وَزَوَّجۡنَٰهُم بِحُورٍ عِينٍ ٥٤Hivi ndivyo itakavyo kuwa, na tutawaoza mahurilaini يَدۡعُونَ فِيهَا بِكُلِّ فَٰكِهَةٍ ءَامِنِينَ ٥٥Humo watataka kila aina ya matunda, na wakae kwa amani لَا يَذُوقُونَ فِيهَا ٱلۡمَوۡتَ إِلَّا ٱلۡمَوۡتَةَ ٱلۡأُولَىٰۖ وَوَقَىٰهُمۡ عَذَابَ ٱلۡجَحِيمِ ٥٦Humo hawataonja mauti ila mauti yale ya kwanza, na (Mwenyezi Mungu) atawalinda na adhabu ya Jahannamu فَضۡلًا مِّن رَّبِّكَۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ ٥٧Kuwa ni fadhila zitokazo kwa Mola wako Mlezi. Huko ndiko kufuzu kukubwa فَإِنَّمَا يَسَّرۡنَٰهُ بِلِسَانِكَ لَعَلَّهُمۡ يَتَذَكَّرُونَ ٥٨Basi tumeifanya nyepesi hii Qur'ani kwa ulimi wako, ili wapate kukumbuka فَٱرۡتَقِبۡ إِنَّهُم مُّرۡتَقِبُونَ ٥٩Ngoja tu, na wao wangoje pia

الترجمة: Ali Muhsin Al Barwani.