ملة الإسلام

السورة 75 · 40 آية · Ali Muhsin Al Barwani

سورة القيامة باللغة السواحلية

السورة بالعربية مع التفسير استمع إلى سورة القيامة (1,389 قارئاً)
مكيةسورة القيامة٤٠ آية

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

لَآ أُقۡسِمُ بِيَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ ١Ninaapa kwa Siku ya Kiyama وَلَآ أُقۡسِمُ بِٱلنَّفۡسِ ٱللَّوَّامَةِ ٢Na ninaapa kwa nafsi inayo jilaumu أَيَحۡسَبُ ٱلۡإِنسَٰنُ أَلَّن نَّجۡمَعَ عِظَامَهُۥ ٣Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake بَلَىٰ قَٰدِرِينَ عَلَىٰٓ أَن نُّسَوِّيَ بَنَانَهُۥ ٤Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake بَلۡ يُرِيدُ ٱلۡإِنسَٰنُ لِيَفۡجُرَ أَمَامَهُۥ ٥Lakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilioko mbele yake يَسۡـَٔلُ أَيَّانَ يَوۡمُ ٱلۡقِيَٰمَةِ ٦Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama فَإِذَا بَرِقَ ٱلۡبَصَرُ ٧Basi jicho litapo dawaa وَخَسَفَ ٱلۡقَمَرُ ٨Na mwezi utapo patwa وَجُمِعَ ٱلشَّمۡسُ وَٱلۡقَمَرُ ٩Na likakusanywa jua na mwezi يَقُولُ ٱلۡإِنسَٰنُ يَوۡمَئِذٍ أَيۡنَ ٱلۡمَفَرُّ ١٠Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio كـَلَّا لَا وَزَرَ ١١La! Hapana pa kukimbilia إِلَىٰ رَبِّكَ يَوۡمَئِذٍ ٱلۡمُسۡتَقَرُّ ١٢Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu يُنَبَّؤُاْ ٱلۡإِنسَٰنُ يَوۡمَئِذِۭ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ ١٣Siku hiyo ataambiwa aliyo yatanguliza na aliyo yaakhirisha بَلِ ٱلۡإِنسَٰنُ عَلَىٰ نَفۡسِهِۦ بَصِيرَةٌ ١٤Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake وَلَوۡ أَلۡقَىٰ مَعَاذِيرَهُۥ ١٥Na ingawa atatoa chungu ya udhuru لَا تُحَرِّكۡ بِهِۦ لِسَانَكَ لِتَعۡجَلَ بِهِۦٓ ١٦Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka إِنَّ عَلَيۡنَا جَمۡعَهُۥ وَقُرۡءَانَهُۥ ١٧Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha فَإِذَا قَرَأۡنَٰهُ فَٱتَّبِعۡ قُرۡءَانَهُۥ ١٨Tunapo usoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake ثُمَّ إِنَّ عَلَيۡنَا بَيَانَهُۥ ١٩Kisha ni juu yetu kuubainisha كـَلَّا بَلۡ تُحِبُّونَ ٱلۡعَاجِلَةَ ٢٠Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani وَتَذَرُونَ ٱلۡأٓخِرَةَ ٢١Na mnaacha maisha ya Akhera وُجُوهٌ يَوۡمَئِذٍ نَّاضِرَةٌ ٢٢Zipo nyuso siku hiyo zitao ng'ara إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌ ٢٣Zinamwangallia Mola wao Mlezi وَوُجُوهٌ يَوۡمَئِذِۭ بَاسِرَةٌ ٢٤Na zipo nyuso siku hiyo zitakao kunjana تَظُنُّ أَن يُفۡعَلَ بِهَا فَاقِرَةٌ ٢٥Zitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo كـَلَّآ إِذَا بَلَغَتِ ٱلتَّرَاقِيَ ٢٦La, hasha! (Roho) itakapo fikia kwenye mafupa ya koo وَقِيلَ مَنۡۜ رَاقٍ ٢٧Na pakasemwa: Nani wa kumganga وَظَنَّ أَنَّهُ ٱلۡفِرَاقُ ٢٨Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko kufariki وَٱلۡتَفَّتِ ٱلسَّاقُ بِٱلسَّاقِ ٢٩Na utapo ambatishwa muundi kwa muundi إِلَىٰ رَبِّكَ يَوۡمَئِذٍ ٱلۡمَسَاقُ ٣٠Siku hiyo ndiyo kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako Mlezi فَلَا صَدَّقَ وَلَا صَلَّىٰ ٣١Kwa sababu hakusadiki, wala hakusali وَلَٰكِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ ٣٢Bali alikanusha, na akageuka ثُمَّ ذَهَبَ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ يَتَمَطَّىٰٓ ٣٣Kisha akenda kwa ahali zake kwa matao أَوۡلَىٰ لَكَ فَأَوۡلَىٰ ٣٤Ole wako, ole wako ثُمَّ أَوۡلَىٰ لَكَ فَأَوۡلَىٰٓ ٣٥Kisha Ole wako, ole wako أَيَحۡسَبُ ٱلۡإِنسَٰنُ أَن يُتۡرَكَ سُدًى ٣٦Ati anadhani binaadamu kuwa ataachwa bure أَلَمۡ يَكُ نُطۡفَةً مِّن مَّنِيٍّ يُمۡنَىٰ ٣٧Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa ثُمَّ كَانَ عَلَقَةً فَخَلَقَ فَسَوَّىٰ ٣٨Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo فَجَعَلَ مِنۡهُ ٱلزَّوۡجَيۡنِ ٱلذَّكَرَ وَٱلۡأُنثَىٰٓ ٣٩Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke أَلَيۡسَ ذَٰلِكَ بِقَٰدِرٍ عَلَىٰٓ أَن يُحۡـِۧيَ ٱلۡمَوۡتَىٰ ٤٠Je! Huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu

الترجمة: Ali Muhsin Al Barwani.