بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
وَٱلنَّجۡمِ إِذَا هَوَىٰ ١Naapa kwa nyota inapo tua مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمۡ وَمَا غَوَىٰ ٢Mwenzenu huyu hakupotea, wala hakukosea وَمَا يَنطِقُ عَنِ ٱلۡهَوَىٰٓ ٣Wala hatamki kwa matamanio إِنۡ هُوَ إِلَّا وَحۡيٌ يُوحَىٰ ٤Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa عَلَّمَهُۥ شَدِيدُ ٱلۡقُوَىٰ ٥Amemfundisha aliye mwingi wa nguvu ذُو مِرَّةٍ فَٱسۡتَوَىٰ ٦Mwenye kutua, akatulia وَهُوَ بِٱلۡأُفُقِ ٱلۡأَعۡلَىٰ ٧Naye yuko juu kabisa upeo wa macho ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّىٰ ٨Kisha akakaribia na akateremka فَكَانَ قَابَ قَوۡسَيۡنِ أَوۡ أَدۡنَىٰ ٩Akawa ni kama baina ya mipinde miwili, au karibu zaidi فَأَوۡحَىٰٓ إِلَىٰ عَبۡدِهِۦ مَآ أَوۡحَىٰ ١٠Akamfunulia mja wake (Mwenyezi Mungu) alicho mfunulia مَا كَذَبَ ٱلۡفُؤَادُ مَا رَأَىٰٓ ١١Moyo haukusema uwongo uliyo yaona أَفَتُمَٰرُونَهُۥ عَلَىٰ مَا يَرَىٰ ١٢Je! Mnabishana naye kwa aliyo yaona وَلَقَدۡ رَءَاهُ نَزۡلَةً أُخۡرَىٰ ١٣Na akamwona mara nyingine عِندَ سِدۡرَةِ ٱلۡمُنتَهَىٰ ١٤Penye Mkunazi wa mwisho عِندَهَا جَنَّةُ ٱلۡمَأۡوَىٰٓ ١٥Karibu yake ndiyo ipo Bustani inayo kaliwa إِذۡ يَغۡشَى ٱلسِّدۡرَةَ مَا يَغۡشَىٰ ١٦Kilipo ufunika huo Mkunazi hicho kilicho ufunuika مَا زَاغَ ٱلۡبَصَرُ وَمَا طَغَىٰ ١٧Jicho halikuhangaika wala halikuruka mpaka لَقَدۡ رَأَىٰ مِنۡ ءَايَٰتِ رَبِّهِ ٱلۡكُبۡرَىٰٓ ١٨Kwa yakini aliona katika Ishara kubwa kabisa za Mola wake Mlezi أَفَرَءَيۡتُمُ ٱللَّٰتَ وَٱلۡعُزَّىٰ ١٩Je! Mmemuona Lata na Uzza وَمَنَوٰةَ ٱلثَّالِثَةَ ٱلۡأُخۡرَىٰٓ ٢٠Na Manaat, mwingine wa tatu أَلَكُمُ ٱلذَّكَرُ وَلَهُ ٱلۡأُنثَىٰ ٢١Je! Nyinyi mnao wana wanaume na Yeye ndio awe na wanawake تِلۡكَ إِذًا قِسۡمَةٌ ضِيزَىٰٓ ٢٢Huo ni mgawanyo wa dhulma إِنۡ هِيَ إِلَّآ أَسۡمَآءٌ سَمَّيۡتُمُوهَآ أَنتُمۡ وَءَابَآؤُكُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بِهَا مِن سُلۡطَٰنٍۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَمَا تَهۡوَى ٱلۡأَنفُسُۖ وَلَقَدۡ جَآءَهُم مِّن رَّبِّهِمُ ٱلۡهُدَىٰٓ ٢٣Hayo hayakuwa ila ni majina mliyo wapa nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuleta uthibitisho wowote juu ya hayo. Hawafuati ila dhana tu na kipendacho nafsi. Na kwa yakini uwongofu ulikwisha wafikia kutoka kwa Mola wao Mlezi أَمۡ لِلۡإِنسَٰنِ مَا تَمَنَّىٰ ٢٤Ati mtu anakipata kila anacho kitamani فَلِلَّهِ ٱلۡأٓخِرَةُ وَٱلۡأُولَىٰ ٢٥Mwenyezi Mungu tu ndiye Mwenye dunia na Akhera ۞ وَكَم مِّن مَّلَكٍ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ لَا تُغۡنِي شَفَٰعَتُهُمۡ شَيۡـًٔا إِلَّا مِنۢ بَعۡدِ أَن يَأۡذَنَ ٱللَّهُ لِمَن يَشَآءُ وَيَرۡضَىٰٓ ٢٦Na wako Malaika wangapi mbinguni, ambao uombezi wao hautafaa chochote isipo kuwa baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na kumridhia إِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ لَيُسَمُّونَ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ تَسۡمِيَةَ ٱلۡأُنثَىٰ ٢٧Hakika wasio amini Akhera bila ya shaka wao ndio wanawaita Malaika kwa majina ya kike وَمَا لَهُم بِهِۦ مِنۡ عِلۡمٍۖ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّۖ وَإِنَّ ٱلظَّنَّ لَا يُغۡنِي مِنَ ٱلۡحَقِّ شَيۡـًٔا ٢٨Nao hawana ujuzi wowote kwa hayo isipo kuwa wanafuata dhana tu. Na dhana haisaidii chochote mbele ya haki فَأَعۡرِضۡ عَن مَّن تَوَلَّىٰ عَن ذِكۡرِنَا وَلَمۡ يُرِدۡ إِلَّا ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا ٢٩Basi mwachilie mbali anaye upa kisogo ukumbusho wetu, na wala hataki ila maisha ya dunia ذَٰلِكَ مَبۡلَغُهُم مِّنَ ٱلۡعِلۡمِۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِمَنِ ٱهۡتَدَىٰ ٣٠Huo ndio mwisho wao wa ujuzi. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuipotea njia yake, na Yeye ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuongoka وَلِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ لِيَجۡزِيَ ٱلَّذِينَ أَسَٰٓـُٔواْ بِمَا عَمِلُواْ وَيَجۡزِيَ ٱلَّذِينَ أَحۡسَنُواْ بِٱلۡحُسۡنَى ٣١Ni vya Mwenyezi Mungu vyote viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi, ili awalipe walio tenda ubaya kwa waliyo yatenda, na walio tenda mema awalipe mema ٱلَّذِينَ يَجۡتَنِبُونَ كَبَٰٓئِرَ ٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡفَوَٰحِشَ إِلَّا ٱللَّمَمَۚ إِنَّ رَبَّكَ وَٰسِعُ ٱلۡمَغۡفِرَةِۚ هُوَ أَعۡلَمُ بِكُمۡ إِذۡ أَنشَأَكُم مِّنَ ٱلۡأَرۡضِ وَإِذۡ أَنتُمۡ أَجِنَّةٌ فِي بُطُونِ أُمَّهَٰتِكُمۡۖ فَلَا تُزَكُّوٓاْ أَنفُسَكُمۡۖ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَنِ ٱتَّقَىٰٓ ٣٢Ambao wanajiepusha na madhambi makuu na vitendo vichafu, isipo kuwa makosa khafifu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mkunjufu wa maghfira, naye anakujueni sana tangu alipo kuumbeni kutoka kwenye ardhi, na mlipo kuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msijisifu usafi. Yeye anamjua sana mwenye kujikinga na maovu أَفَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي تَوَلَّىٰ ٣٣Je! Umemwona yule aliye geuka وَأَعۡطَىٰ قَلِيلًا وَأَكۡدَىٰٓ ٣٤Na akatoa kidogo, kisha akajizuia أَعِندَهُۥ عِلۡمُ ٱلۡغَيۡبِ فَهُوَ يَرَىٰٓ ٣٥Je! Anayo huyo ilimu ya ghaibu, basi ndio anaona أَمۡ لَمۡ يُنَبَّأۡ بِمَا فِي صُحُفِ مُوسَىٰ ٣٦Au hakuambiwa yaliyomo katika Vitabu vya Musa وَإِبۡرَٰهِيمَ ٱلَّذِي وَفَّىٰٓ ٣٧Na vya Ibrahimu aliye timiza ahadi أَلَّا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزۡرَ أُخۡرَىٰ ٣٨Ya kwamba hakika nafsi iliyo beba madhambi haibebi madhambi ya mwengine وَأَن لَّيۡسَ لِلۡإِنسَٰنِ إِلَّا مَا سَعَىٰ ٣٩Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyo yafanya mwenyewe وَأَنَّ سَعۡيَهُۥ سَوۡفَ يُرَىٰ ٤٠Na kwamba vitendo vyake vitaonekana ثُمَّ يُجۡزَىٰهُ ٱلۡجَزَآءَ ٱلۡأَوۡفَىٰ ٤١Kisha ndio atalipwa malipo yake kwa ukamilifu وَأَنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلۡمُنتَهَىٰ ٤٢Na kwamba kwao Mola wako Mlezi ndio mwisho وَأَنَّهُۥ هُوَ أَضۡحَكَ وَأَبۡكَىٰ ٤٣Na kwamba Yeye ndiye anaye leta kicheko na kilio وَأَنَّهُۥ هُوَ أَمَاتَ وَأَحۡيَا ٤٤Na kwamba Yeye ndiye anaye fisha na kuhuisha وَأَنَّهُۥ خَلَقَ ٱلزَّوۡجَيۡنِ ٱلذَّكَرَ وَٱلۡأُنثَىٰ ٤٥Na kwamba Yeye ndiye aliye umba jozi, dume na jike مِن نُّطۡفَةٍ إِذَا تُمۡنَىٰ ٤٦Kutokana na mbegu ya uzazi inapo miminwa وَأَنَّ عَلَيۡهِ ٱلنَّشۡأَةَ ٱلۡأُخۡرَىٰ ٤٧Na kwamba ni juu yake ufufuo mwengine وَأَنَّهُۥ هُوَ أَغۡنَىٰ وَأَقۡنَىٰ ٤٨Na kwamba ni Yeye ndiye anaye tosheleza na kukinaisha وَأَنَّهُۥ هُوَ رَبُّ ٱلشِّعۡرَىٰ ٤٩Na kwamba hakika Yeye ndiye Mola Mlezi wa nyota ya Shii'ra وَأَنَّهُۥٓ أَهۡلَكَ عَادًا ٱلۡأُولَىٰ ٥٠Na kwamba Yeye ndiye aliye waangamiza A'di wa kwanza وَثَمُودَاْ فَمَآ أَبۡقَىٰ ٥١Na Thamudi hakuwabakisha وَقَوۡمَ نُوحٍ مِّن قَبۡلُۖ إِنَّهُمۡ كَانُواْ هُمۡ أَظۡلَمَ وَأَطۡغَىٰ ٥٢Na kabla yao kaumu ya Nuhu. Na hao hakika walikuwa ni madhaalimu zaidi, na waovu zaidi وَٱلۡمُؤۡتَفِكَةَ أَهۡوَىٰ ٥٣Na miji iliyo pinduliwa, ni Yeye aliye ipindua فَغَشَّىٰهَا مَا غَشَّىٰ ٥٤Vikaifunika vilivyo funika فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكَ تَتَمَارَىٰ ٥٥Basi neema gani ya Mola wako Mlezi unayo ifanyia shaka هَٰذَا نَذِيرٌ مِّنَ ٱلنُّذُرِ ٱلۡأُولَىٰٓ ٥٦Hili ni Onyo katika maonyo yale yale ya zamani أَزِفَتِ ٱلۡأٓزِفَةُ ٥٧Kiyama kimekaribia لَيۡسَ لَهَا مِن دُونِ ٱللَّهِ كَاشِفَةٌ ٥٨Hapana wa kukifichua isipo kuwa Mwenyezi Mungu أَفَمِنۡ هَٰذَا ٱلۡحَدِيثِ تَعۡجَبُونَ ٥٩Je! Mnayastaajabia maneno haya وَتَضۡحَكُونَ وَلَا تَبۡكُونَ ٦٠Na mnacheka, wala hamlii وَأَنتُمۡ سَٰمِدُونَ ٦١Nanyi mmeghafilika فَٱسۡجُدُواْۤ لِلَّهِۤ وَٱعۡبُدُواْ ۩ ٦٢Basi msujudieni Mwenyezi Mungu, na mumuabudu