ملة الإسلام

السورة 37 · 182 آية · Ali Muhsin Al Barwani

سورة الصافات باللغة السواحلية

السورة بالعربية مع التفسير استمع إلى سورة الصافات (1,203 قارئاً)
مكيةسورة الصافات١٨٢ آية

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلصَّٰٓفَّٰتِ صَفًّا ١Naapa kwa wanao jipanga kwa safu فَٱلزَّٰجِرَٰتِ زَجۡرًا ٢Na kwa wenye kukataza mabaya فَٱلتَّٰلِيَٰتِ ذِكۡرًا ٣Na kwa wenye kusoma Ukumbusho إِنَّ إِلَٰهَكُمۡ لَوَٰحِدٌ ٤Hakika Mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja رَّبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا وَرَبُّ ٱلۡمَشَٰرِقِ ٥Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na yaliyomo kati yao, na ni Mola Mlezi wa mashariki zote إِنَّا زَيَّنَّا ٱلسَّمَآءَ ٱلدُّنۡيَا بِزِينَةٍ ٱلۡكَوَاكِبِ ٦Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota وَحِفۡظًا مِّن كُلِّ شَيۡطَٰنٍ مَّارِدٍ ٧Na kulinda na kila shet'ani a'si لَّا يَسَّمَّعُونَ إِلَى ٱلۡمَلَإِ ٱلۡأَعۡلَىٰ وَيُقۡذَفُونَ مِن كُلِّ جَانِبٍ ٨Wasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu. Na wanafukuzwa huko kila upande دُحُورًاۖ وَلَهُمۡ عَذَابٌ وَاصِبٌ ٩Wakifurushwa. Na wanayo adhabu ya kudumu إِلَّا مَنۡ خَطِفَ ٱلۡخَطۡفَةَ فَأَتۡبَعَهُۥ شِهَابٌ ثَاقِبٌ ١٠Isipo kuwa anaye nyakua kitu kidogo, na mara humfwatia kimondo kinacho ng'ara فَٱسۡتَفۡتِهِمۡ أَهُمۡ أَشَدُّ خَلۡقًا أَم مَّنۡ خَلَقۡنَآۚ إِنَّا خَلَقۡنَٰهُم مِّن طِينٍ لَّازِبِۭ ١١Hebu waulize: Je! Wao ni wenye umbo gumu zaidi au hao wengine tulio waumba. Hakika Sisi tuliwaumba wao kwa udongo unao nata بَلۡ عَجِبۡتَ وَيَسۡخَرُونَ ١٢Bali unastaajabu, na wao wanafanya maskhara وَإِذَا ذُكِّرُواْ لَا يَذۡكُرُونَ ١٣Na wanapo kumbushwa hawakumbuki وَإِذَا رَأَوۡاْ ءَايَةً يَسۡتَسۡخِرُونَ ١٤Na wanapo ona Ishara, wanafanya maskhara وَقَالُوٓاْ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا سِحۡرٌ مُّبِينٌ ١٥Na husema: Haya si chochote ila ni uchawi tu ulio dhaahiri أَءِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَٰمًا أَءِنَّا لَمَبۡعُوثُونَ ١٦Ati tukisha kufa na tukawa udongo na mifupa ndio kweli tutafufuliwa أَوَءَابَآؤُنَا ٱلۡأَوَّلُونَ ١٧Hata baba zetu wa zamani قُلۡ نَعَمۡ وَأَنتُمۡ دَٰخِرُونَ ١٨Sema: Naam! Hali nanyi ni madhalili فَإِنَّمَا هِيَ زَجۡرَةٌ وَٰحِدَةٌ فَإِذَا هُمۡ يَنظُرُونَ ١٩Huko utapigwa ukelele mmoja tu! Na hapo ndio wataona وَقَالُواْ يَٰوَيۡلَنَا هَٰذَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ ٢٠Watasema: Ole wetu! Hii ndiyo Siku ya Malipo هَٰذَا يَوۡمُ ٱلۡفَصۡلِ ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ ٢١Hii ndiyo Siku ya Hukumu mliyo kuwa mkiikadhibisha ۞ ٱحۡشُرُواْ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ وَأَزۡوَٰجَهُمۡ وَمَا كَانُواْ يَعۡبُدُونَ ٢٢Wakusanyeni walio dhulumu, na wake zao, na hao walio kuwa wakiwaabudu مِن دُونِ ٱللَّهِ فَٱهۡدُوهُمۡ إِلَىٰ صِرَٰطِ ٱلۡجَحِيمِ ٢٣Badala ya Mwenyezi Mungu. Waongozeni njia ya Jahannamu وَقِفُوهُمۡۖ إِنَّهُم مَّسۡـُٔولُونَ ٢٤Na wasimamisheni. Hakika hao watasailiwa مَا لَكُمۡ لَا تَنَاصَرُونَ ٢٥Mna nini? Mbona hamsaidiani بَلۡ هُمُ ٱلۡيَوۡمَ مُسۡتَسۡلِمُونَ ٢٦Bali hii leo, watasalimu amri وَأَقۡبَلَ بَعۡضُهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٍ يَتَسَآءَلُونَ ٢٧Watakabiliana wao kwa wao kuulizana قَالُوٓاْ إِنَّكُمۡ كُنتُمۡ تَأۡتُونَنَا عَنِ ٱلۡيَمِينِ ٢٨Watasema: Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujia upande wa kulia قَالُواْ بَل لَّمۡ تَكُونُواْ مُؤۡمِنِينَ ٢٩Watasema (wakubwa): Bali nyinyi wenyewe hamkuwa Waumini وَمَا كَانَ لَنَا عَلَيۡكُم مِّن سُلۡطَٰنِۭۖ بَلۡ كُنتُمۡ قَوۡمًا طَٰغِينَ ٣٠Sisi hatukuwa na mamlaka juu yenu, bali nyinyi wenyewe mlikuwa wapotovu فَحَقَّ عَلَيۡنَا قَوۡلُ رَبِّنَآۖ إِنَّا لَذَآئِقُونَ ٣١Basi hukumu ya Mola wetu Mlezi imekwisha tuthibitikia. Hakika bila ya shaka tutaonja tu adhabu فَأَغۡوَيۡنَٰكُمۡ إِنَّا كُنَّا غَٰوِينَ ٣٢Tulikupotezeni kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu فَإِنَّهُمۡ يَوۡمَئِذٍ فِي ٱلۡعَذَابِ مُشۡتَرِكُونَ ٣٣Basi wao kwa hakika siku hiyo watashirikiana katika adhabu pamoja إِنَّا كَذَٰلِكَ نَفۡعَلُ بِٱلۡمُجۡرِمِينَ ٣٤Hivyo ndivyo tutakavyo wafanyia wakosefu إِنَّهُمۡ كَانُوٓاْ إِذَا قِيلَ لَهُمۡ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ يَسۡتَكۡبِرُونَ ٣٥Wao walipo kuwa wakiambiwa La ilaha illa 'Llahu Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu, wakijivuna وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُوٓاْ ءَالِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجۡنُونِۭ ٣٦Na wakisema: Hivyo sisi tuiache miungu yetu kwa ajili ya huyu mtunga mashairi mwendawazimu بَلۡ جَآءَ بِٱلۡحَقِّ وَصَدَّقَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ ٣٧Bali huyu amekuja kwa Haki, na amewasadikisha Mitume إِنَّكُمۡ لَذَآئِقُواْ ٱلۡعَذَابِ ٱلۡأَلِيمِ ٣٨Hakika nyinyi bila ya shaka mtaionja adhabu chungu وَمَا تُجۡزَوۡنَ إِلَّا مَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ ٣٩Wala hamlipwi ila hayo mliyo kuwa mkiyafanya إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلۡمُخۡلَصِينَ ٤٠Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa أُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ رِزۡقٌ مَّعۡلُومٌ ٤١Hao ndio watakao pata riziki maalumu فَوَٰكِهُ وَهُم مُّكۡرَمُونَ ٤٢Matunda, nao watahishimiwa فِي جَنَّٰتِ ٱلنَّعِيمِ ٤٣Katika Bustani za neema عَلَىٰ سُرُرٍ مُّتَقَٰبِلِينَ ٤٤Wako juu ya viti wamekabiliana يُطَافُ عَلَيۡهِم بِكَأۡسٍ مِّن مَّعِينِۭ ٤٥Wanazungushiwa kikombe chenye kinywaji cha chemchem بَيۡضَآءَ لَذَّةٍ لِّلشَّٰرِبِينَ ٤٦Kinywaji cheupe, kitamu kwa wanywao لَا فِيهَا غَوۡلٌ وَلَا هُمۡ عَنۡهَا يُنزَفُونَ ٤٧Hakina madhara, wala hakiwaleweshi وَعِندَهُمۡ قَٰصِرَٰتُ ٱلطَّرۡفِ عِينٌ ٤٨Na watakuwa nao wanawake wenye macho ya staha mazuri كَأَنَّهُنَّ بَيۡضٌ مَّكۡنُونٌ ٤٩Hao wanawake kama mayai yaliyo hifadhika فَأَقۡبَلَ بَعۡضُهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٍ يَتَسَآءَلُونَ ٥٠Waingie kuulizana wenyewe kwa wenyewe قَالَ قَآئِلٌ مِّنۡهُمۡ إِنِّي كَانَ لِي قَرِينٌ ٥١Aseme msemaji mmoja miongoni mwao: Hakika mimi nalikuwa na rafiki يَقُولُ أَءِنَّكَ لَمِنَ ٱلۡمُصَدِّقِينَ ٥٢Aliye kuwa akinambia: Hivyo wewe ni katika wanao sadiki أَءِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَٰمًا أَءِنَّا لَمَدِينُونَ ٥٣Ati tukisha kufa tukawa udongo na mafupa, ndio tutalipwa na kuhisabiwa قَالَ هَلۡ أَنتُم مُّطَّلِعُونَ ٥٤Atasema: Je! Nyie mnawaona فَٱطَّلَعَ فَرَءَاهُ فِي سَوَآءِ ٱلۡجَحِيمِ ٥٥Basi atachungulia amwone katikati ya Jahannamu قَالَ تَٱللَّهِ إِن كِدتَّ لَتُرۡدِينِ ٥٦Atasema: Wallahi! Ulikaribia kunipoteza وَلَوۡلَا نِعۡمَةُ رَبِّي لَكُنتُ مِنَ ٱلۡمُحۡضَرِينَ ٥٧Na lau kuwa si neema ya Mola wangu Mlezi bila ya shaka ningeli kuwa miongoni mwa walio hudhurishwa أَفَمَا نَحۡنُ بِمَيِّتِينَ ٥٨Je! Sisi hatutakufa إِلَّا مَوۡتَتَنَا ٱلۡأُولَىٰ وَمَا نَحۡنُ بِمُعَذَّبِينَ ٥٩Isipo kuwa kifo chetu cha kwanza? Wala sisi hatutaadhibiwa إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ ٦٠Hakika huku bila ya shaka ndiko kufuzu kukubwa لِمِثۡلِ هَٰذَا فَلۡيَعۡمَلِ ٱلۡعَٰمِلُونَ ٦١Kwa mfano wa haya nawatende watendao أَذَٰلِكَ خَيۡرٌ نُّزُلًا أَمۡ شَجَرَةُ ٱلزَّقُّومِ ٦٢Je! Kukaribishwa hivi si ndio bora, au mti wa Zaqqum إِنَّا جَعَلۡنَٰهَا فِتۡنَةً لِّلظَّٰلِمِينَ ٦٣Hakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni mateso kwa walio dhulumu إِنَّهَا شَجَرَةٌ تَخۡرُجُ فِيٓ أَصۡلِ ٱلۡجَحِيمِ ٦٤Hakika huo ni mti unao toka katikati ya Jahannamu طَلۡعُهَا كَأَنَّهُۥ رُءُوسُ ٱلشَّيَٰطِينِ ٦٥Mashada ya matunda yake kama kwamba vichwa vya mashet'ani فَإِنَّهُمۡ لَأٓكِلُونَ مِنۡهَا فَمَالِـُٔونَ مِنۡهَا ٱلۡبُطُونَ ٦٦Basi hakika bila ya shaka hao watayala hayo, na wajaze matumbo ثُمَّ إِنَّ لَهُمۡ عَلَيۡهَا لَشَوۡبًا مِّنۡ حَمِيمٍ ٦٧Kisha juu yake wanyweshwe mchanganyo wa maji yamoto yaliyo chemka ثُمَّ إِنَّ مَرۡجِعَهُمۡ لَإِلَى ٱلۡجَحِيمِ ٦٨Kisha hakika marejeo yao bila ya shaka yatakuwa kwenye Jahannamu إِنَّهُمۡ أَلۡفَوۡاْ ءَابَآءَهُمۡ ضَآلِّينَ ٦٩Hakika waliwakuta baba zao wamepotea فَهُمۡ عَلَىٰٓ ءَاثَٰرِهِمۡ يُهۡرَعُونَ ٧٠Na wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao وَلَقَدۡ ضَلَّ قَبۡلَهُمۡ أَكۡثَرُ ٱلۡأَوَّلِينَ ٧١Na bila ya shaka walikwisha potea kabla yao wengi wa watu wa zamani وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا فِيهِم مُّنذِرِينَ ٧٢Na Sisi hakika tuliwapelekea waonyaji فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُنذَرِينَ ٧٣Basi hebu angalia ulikuwaje mwisho wa walio onywa إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلۡمُخۡلَصِينَ ٧٤Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa وَلَقَدۡ نَادَىٰنَا نُوحٌ فَلَنِعۡمَ ٱلۡمُجِيبُونَ ٧٥Na hakika Nuhu alitwita, na Sisi ni bora wa waitikiaji وَنَجَّيۡنَٰهُ وَأَهۡلَهُۥ مِنَ ٱلۡكَرۡبِ ٱلۡعَظِيمِ ٧٦Na tulimwokoa yeye na ahali zake kutokana na msiba mkubwa وَجَعَلۡنَا ذُرِّيَّتَهُۥ هُمُ ٱلۡبَاقِينَ ٧٧Na tuliwajaalia dhuriya zake ndio wenye kubakia وَتَرَكۡنَا عَلَيۡهِ فِي ٱلۡأٓخِرِينَ ٧٨Na tukamwachia (sifa njema) kwa walio kuja baadaye سَلَٰمٌ عَلَىٰ نُوحٍ فِي ٱلۡعَٰلَمِينَ ٧٩Iwe salama kwa Nuhu ulimwenguni kote إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ ٨٠Kwa hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema إِنَّهُۥ مِنۡ عِبَادِنَا ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ٨١Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini ثُمَّ أَغۡرَقۡنَا ٱلۡأٓخَرِينَ ٨٢Kisha tukawazamisha wale wengine ۞ وَإِنَّ مِن شِيعَتِهِۦ لَإِبۡرَٰهِيمَ ٨٣Na hakika Ibrahim alikuwa katika kundi lake إِذۡ جَآءَ رَبَّهُۥ بِقَلۡبٍ سَلِيمٍ ٨٤Alipo mjia Mola wake Mlezi kwa moyo mzima إِذۡ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوۡمِهِۦ مَاذَا تَعۡبُدُونَ ٨٥Alimwambia baba yake na watu wake: Mnaabudu nini أَئِفۡكًا ءَالِهَةً دُونَ ٱللَّهِ تُرِيدُونَ ٨٦Kwa kuzua tu mnataka miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu فَمَا ظَنُّكُم بِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ٨٧Mnamdhania nini Mola Mlezi wa walimwengu wote فَنَظَرَ نَظۡرَةً فِي ٱلنُّجُومِ ٨٨Kisha akapiga jicho kutazama nyota فَقَالَ إِنِّي سَقِيمٌ ٨٩Akasema: Hakika mimi ni mgonjwa فَتَوَلَّوۡاْ عَنۡهُ مُدۡبِرِينَ ٩٠Nao wakamwacha, wakampa kisogo فَرَاغَ إِلَىٰٓ ءَالِهَتِهِمۡ فَقَالَ أَلَا تَأۡكُلُونَ ٩١Basi akaiendea miungu yao kwa siri, akaiambia: Mbona hamli مَا لَكُمۡ لَا تَنطِقُونَ ٩٢Mna nini hata hamsemi فَرَاغَ عَلَيۡهِمۡ ضَرۡبَۢا بِٱلۡيَمِينِ ٩٣Kisha akaigeukia kuipiga kwa mkono wa kulia فَأَقۡبَلُوٓاْ إِلَيۡهِ يَزِفُّونَ ٩٤Basi wakamjia upesi upesi قَالَ أَتَعۡبُدُونَ مَا تَنۡحِتُونَ ٩٥Akasema: Hivyo mnaviabudu vitu mnavyo vichonga wenyewe وَٱللَّهُ خَلَقَكُمۡ وَمَا تَعۡمَلُونَ ٩٦Na hali Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni nyinyi na hivyo mnavyo vifanya قَالُواْ ٱبۡنُواْ لَهُۥ بُنۡيَٰنًا فَأَلۡقُوهُ فِي ٱلۡجَحِيمِ ٩٧Wakasema: Mjengeeni jengo, na kisha mtupeni motoni humo فَأَرَادُواْ بِهِۦ كَيۡدًا فَجَعَلۡنَٰهُمُ ٱلۡأَسۡفَلِينَ ٩٨Basi walitaka kumfanyia vitimbi, lakini tukawafanya wao ndio wa chini وَقَالَ إِنِّي ذَاهِبٌ إِلَىٰ رَبِّي سَيَهۡدِينِ ٩٩Na akasema: Hakika mimi nahama, nakwenda kwa Mola wangu Mlezi; Yeye ataniongoa رَبِّ هَبۡ لِي مِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ ١٠٠Ewe Mola wangu Mlezi! Nitunukie aliye miongoni mwa watenda mema فَبَشَّرۡنَٰهُ بِغُلَٰمٍ حَلِيمٍ ١٠١Basi tukambashiria mwana aliye mpole فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ ٱلسَّعۡيَ قَالَ يَٰبُنَيَّ إِنِّيٓ أَرَىٰ فِي ٱلۡمَنَامِ أَنِّيٓ أَذۡبَحُكَ فَٱنظُرۡ مَاذَا تَرَىٰۚ قَالَ يَٰٓأَبَتِ ٱفۡعَلۡ مَا تُؤۡمَرُۖ سَتَجِدُنِيٓ إِن شَآءَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلصَّٰبِرِينَ ١٠٢Basi alipo fika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyo amrishwa, utanikuta mimi, Inshallah, katika wanao subiri فَلَمَّآ أَسۡلَمَا وَتَلَّهُۥ لِلۡجَبِينِ ١٠٣Basi wote wawili walipo jisalimisha, na akamlaza juu ya kipaji وَنَٰدَيۡنَٰهُ أَن يَٰٓإِبۡرَٰهِيمُ ١٠٤Tulimwita: Ewe Ibrahim قَدۡ صَدَّقۡتَ ٱلرُّءۡيَآۚ إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ ١٠٥Umekwisha itimiliza ndoto. Hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao tenda mema إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ ٱلۡبَلَٰٓؤُاْ ٱلۡمُبِينُ ١٠٦Hakika haya ni majaribio yaliyo dhaahiri وَفَدَيۡنَٰهُ بِذِبۡحٍ عَظِيمٍ ١٠٧Basi tukamtolea fidia kwa dhabihu mtukufu وَتَرَكۡنَا عَلَيۡهِ فِي ٱلۡأٓخِرِينَ ١٠٨Na tukamwachia (sifa njema) kwa watu walio kuja baadaye سَلَٰمٌ عَلَىٰٓ إِبۡرَٰهِيمَ ١٠٩Iwe salama kwa Ibrahim كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ ١١٠Hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema إِنَّهُۥ مِنۡ عِبَادِنَا ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ١١١Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini وَبَشَّرۡنَٰهُ بِإِسۡحَٰقَ نَبِيًّا مِّنَ ٱلصَّٰلِحِينَ ١١٢Na tukambashiria kuzaliwa Is-haqa, naye ni Nabii miongoni mwa watu wema وَبَٰرَكۡنَا عَلَيۡهِ وَعَلَىٰٓ إِسۡحَٰقَۚ وَمِن ذُرِّيَّتِهِمَا مُحۡسِنٌ وَظَالِمٌ لِّنَفۡسِهِۦ مُبِينٌ ١١٣Na tukambarikia yeye na Is-haqa. Na miongoni mwa dhuriya zao walitokea wema na wenye kudhulumu nafsi zao waziwazi وَلَقَدۡ مَنَنَّا عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَٰرُونَ ١١٤Na kwa hakika tuliwafanyia hisani Musa na Haruni وَنَجَّيۡنَٰهُمَا وَقَوۡمَهُمَا مِنَ ٱلۡكَرۡبِ ٱلۡعَظِيمِ ١١٥Na tukawaokoa wao na watu wao kutokana na dhiki kubwa وَنَصَرۡنَٰهُمۡ فَكَانُواْ هُمُ ٱلۡغَٰلِبِينَ ١١٦Na tukawanusuru; na wakawa wao ndio wenye kushinda وَءَاتَيۡنَٰهُمَا ٱلۡكِتَٰبَ ٱلۡمُسۡتَبِينَ ١١٧Na tukawapa wawili hao Kitabu kinacho bainisha وَهَدَيۡنَٰهُمَا ٱلصِّرَٰطَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ ١١٨Na tukawaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka وَتَرَكۡنَا عَلَيۡهِمَا فِي ٱلۡأٓخِرِينَ ١١٩Na tukawaachia (sifa njema) katika watu walio kuja baadaye سَلَٰمٌ عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَٰرُونَ ١٢٠Iwe salama kwa Musa na Haruni إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ ١٢١Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema إِنَّهُمَا مِنۡ عِبَادِنَا ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ١٢٢Hakika wawili hao ni katika waja wetu walio amini وَإِنَّ إِلۡيَاسَ لَمِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ ١٢٣Na hakika Ilyas bila ya shaka alikuwa miongoni mwa Mitume إِذۡ قَالَ لِقَوۡمِهِۦٓ أَلَا تَتَّقُونَ ١٢٤Alipo waambia watu wake: Hamwogopi أَتَدۡعُونَ بَعۡلًا وَتَذَرُونَ أَحۡسَنَ ٱلۡخَٰلِقِينَ ١٢٥Mnamwomba Baa'li na mnamwacha Mbora wa waumbaji ٱللَّهَ رَبَّكُمۡ وَرَبَّ ءَابَآئِكُمُ ٱلۡأَوَّلِينَ ١٢٦Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa zamani فَكَذَّبُوهُ فَإِنَّهُمۡ لَمُحۡضَرُونَ ١٢٧Wakamkadhibisha. Basi kwa hakika watahudhurishwa إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلۡمُخۡلَصِينَ ١٢٨Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa وَتَرَكۡنَا عَلَيۡهِ فِي ٱلۡأٓخِرِينَ ١٢٩Na tumemwachia (sifa nzuri) kwa walio kuja baadaye سَلَٰمٌ عَلَىٰٓ إِلۡ يَاسِينَ ١٣٠Iwe salama kwa Ilyas إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ ١٣١Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema إِنَّهُۥ مِنۡ عِبَادِنَا ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ١٣٢Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini وَإِنَّ لُوطًا لَّمِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ ١٣٣Na hakika Lut'i bila ya shaka ni miongoni mwa Mitume إِذۡ نَجَّيۡنَٰهُ وَأَهۡلَهُۥٓ أَجۡمَعِينَ ١٣٤Tulipo mwokoa yeye na ahali zake wote إِلَّا عَجُوزًا فِي ٱلۡغَٰبِرِينَ ١٣٥Isipo kuwa mwanamke mkongwe katika wale walio bakia nyuma ثُمَّ دَمَّرۡنَا ٱلۡأٓخَرِينَ ١٣٦Kisha tukawaangamiza wale wengineo وَإِنَّكُمۡ لَتَمُرُّونَ عَلَيۡهِم مُّصۡبِحِينَ ١٣٧Na hakika nyinyi mnawapitia wakati wa asubuhi وَبِٱلَّيۡلِۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ ١٣٨Na usiku. Basi je! Hamyatii akilini وَإِنَّ يُونُسَ لَمِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ ١٣٩Na hakika Yunus alikuwa miongoni mwa Mitume إِذۡ أَبَقَ إِلَى ٱلۡفُلۡكِ ٱلۡمَشۡحُونِ ١٤٠Alipo kimbia katika jahazi lilio sheheni فَسَاهَمَ فَكَانَ مِنَ ٱلۡمُدۡحَضِينَ ١٤١Akaingia katika kupigiwa kura, na akawa katika walio shindwa فَٱلۡتَقَمَهُ ٱلۡحُوتُ وَهُوَ مُلِيمٌ ١٤٢Samaki akammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa فَلَوۡلَآ أَنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلۡمُسَبِّحِينَ ١٤٣Na ingeli kuwa hakuwa katika wanao mtakasa Mwenyezi Mungu لَلَبِثَ فِي بَطۡنِهِۦٓ إِلَىٰ يَوۡمِ يُبۡعَثُونَ ١٤٤Bila ya shaka angeli kaa ndani yake mpaka siku ya kufufuliwa ۞ فَنَبَذۡنَٰهُ بِٱلۡعَرَآءِ وَهُوَ سَقِيمٌ ١٤٥Lakini tulimtupa ufukweni patupu, hali yu mgonjwa وَأَنۢبَتۡنَا عَلَيۡهِ شَجَرَةً مِّن يَقۡطِينٍ ١٤٦Na tukauotesha juu yake mmea wa kabila ya mung'unye وَأَرۡسَلۡنَٰهُ إِلَىٰ مِاْئَةِ أَلۡفٍ أَوۡ يَزِيدُونَ ١٤٧Na tulimtuma kwa watu laki moja au zaidi فَـَٔامَنُواْ فَمَتَّعۡنَٰهُمۡ إِلَىٰ حِينٍ ١٤٨Basi wakaamini, na tukawastarehesha kwa muda فَٱسۡتَفۡتِهِمۡ أَلِرَبِّكَ ٱلۡبَنَاتُ وَلَهُمُ ٱلۡبَنُونَ ١٤٩Basi waulize: Ati Mola wako Mlezi ndiye mwenye watoto wa kike, na wao wanao watoto wa kiume أَمۡ خَلَقۡنَا ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ إِنَٰثًا وَهُمۡ شَٰهِدُونَ ١٥٠Au tumewaumba Malaika kuwa ni wanawake, na wao wakashuhudia أَلَآ إِنَّهُم مِّنۡ إِفۡكِهِمۡ لَيَقُولُونَ ١٥١Ati ni kwa uzushi wao ndio wanasema وَلَدَ ٱللَّهُ وَإِنَّهُمۡ لَكَٰذِبُونَ ١٥٢Mwenyezi Mungu amezaa! Ama hakika bila ya shaka hao ni waongo أَصۡطَفَى ٱلۡبَنَاتِ عَلَى ٱلۡبَنِينَ ١٥٣Ati amekhiari watoto wa kike kuliko wanaume مَا لَكُمۡ كَيۡفَ تَحۡكُمُونَ ١٥٤Mna nini? Mnahukumu vipi nyinyi أَفَلَا تَذَكَّرُونَ ١٥٥Hamkumbuki أَمۡ لَكُمۡ سُلۡطَٰنٌ مُّبِينٌ ١٥٦Au mnayo hoja iliyo wazi فَأۡتُواْ بِكِتَٰبِكُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ ١٥٧Basi leteni Kitabu chenu kama mnasema kweli وَجَعَلُواْ بَيۡنَهُۥ وَبَيۡنَ ٱلۡجِنَّةِ نَسَبًاۚ وَلَقَدۡ عَلِمَتِ ٱلۡجِنَّةُ إِنَّهُمۡ لَمُحۡضَرُونَ ١٥٨Na wameweka makhusiano ya nasaba baina yake na majini; na majini wamekwisha jua bila ya shaka kuwa wao watahudhurishwa سُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يَصِفُونَ ١٥٩Subhana 'Llah Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo msingizia إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلۡمُخۡلَصِينَ ١٦٠Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa فَإِنَّكُمۡ وَمَا تَعۡبُدُونَ ١٦١Basi hakika nyinyi na mnao waabudu مَآ أَنتُمۡ عَلَيۡهِ بِفَٰتِنِينَ ١٦٢Hamwezi kuwapoteza إِلَّا مَنۡ هُوَ صَالِ ٱلۡجَحِيمِ ١٦٣Isipo kuwa yule atakaye ingia Motoni وَمَا مِنَّآ إِلَّا لَهُۥ مَقَامٌ مَّعۡلُومٌ ١٦٤Na hapana katika sisi ila anapo mahali pake maalumu وَإِنَّا لَنَحۡنُ ٱلصَّآفُّونَ ١٦٥Na hakika bila ya shaka sisi ndio wajipangao safu وَإِنَّا لَنَحۡنُ ٱلۡمُسَبِّحُونَ ١٦٦Na hakika sisi ndio wenye kusabihi kutakasa وَإِن كَانُواْ لَيَقُولُونَ ١٦٧Na walikuwapo walio kuwa wakisema لَوۡ أَنَّ عِندَنَا ذِكۡرًا مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ ١٦٨Tungeli kuwa na Ukumbusho kama wa watu wa zamani لَكُنَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلۡمُخۡلَصِينَ ١٦٩Bila ya shaka tungeli kuwa ni waja wa Mwenyezi Mungu wenye ikhlasi فَكَفَرُواْ بِهِۦۖ فَسَوۡفَ يَعۡلَمُونَ ١٧٠Lakini waliukataa. Basi watakuja jua وَلَقَدۡ سَبَقَتۡ كَلِمَتُنَا لِعِبَادِنَا ٱلۡمُرۡسَلِينَ ١٧١Na bila ya shaka neno letu lilikwisha tangulia kwa waja wetu walio tumwa إِنَّهُمۡ لَهُمُ ٱلۡمَنصُورُونَ ١٧٢Ya kuwa wao bila ya shaka ndio watakao nusuriwa وَإِنَّ جُندَنَا لَهُمُ ٱلۡغَٰلِبُونَ ١٧٣Na kwamba jeshi letu ndilo litakalo shinda فَتَوَلَّ عَنۡهُمۡ حَتَّىٰ حِينٍ ١٧٤Basi waachilie mbali kwa muda وَأَبۡصِرۡهُمۡ فَسَوۡفَ يُبۡصِرُونَ ١٧٥Na watazame, nao wataona أَفَبِعَذَابِنَا يَسۡتَعۡجِلُونَ ١٧٦Je! Wanaihimiza adhabu yetu فَإِذَا نَزَلَ بِسَاحَتِهِمۡ فَسَآءَ صَبَاحُ ٱلۡمُنذَرِينَ ١٧٧Basi itakapo shuka uwanjani kwao, itakuwa asubuhi mbaya kwa walio onywa وَتَوَلَّ عَنۡهُمۡ حَتَّىٰ حِينٍ ١٧٨Na waache kwa muda وَأَبۡصِرۡ فَسَوۡفَ يُبۡصِرُونَ ١٧٩Na tazama, na wao wataona سُبۡحَٰنَ رَبِّكَ رَبِّ ٱلۡعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ ١٨٠Subhana Rabbi'l'Izzat Ametakasika Mola Mlezi Mwenye enzi na yale wanayo mzulia وَسَلَٰمٌ عَلَى ٱلۡمُرۡسَلِينَ ١٨١Na Salamu juu ya Mitume وَٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ١٨٢Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote

الترجمة: Ali Muhsin Al Barwani.