بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
طسٓمٓ ١T'aa Siin Miim. (T'. S. M) تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡمُبِينِ ٢Hizi ni Aya za Kitabu kinacho bainisha لَعَلَّكَ بَٰخِعٌ نَّفۡسَكَ أَلَّا يَكُونُواْ مُؤۡمِنِينَ ٣Huenda labda ukajikera nafsi yako kwa kuwa hawawi Waumini إِن نَّشَأۡ نُنَزِّلۡ عَلَيۡهِم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ ءَايَةً فَظَلَّتۡ أَعۡنَٰقُهُمۡ لَهَا خَٰضِعِينَ ٤Tunge penda tungeli wateremshia kutoka mbinguni Ishara zikanyenyekea shingo zao وَمَا يَأۡتِيهِم مِّن ذِكۡرٍ مِّنَ ٱلرَّحۡمَٰنِ مُحۡدَثٍ إِلَّا كَانُواْ عَنۡهُ مُعۡرِضِينَ ٥Wala hauwafikii ukumbusho mpya kutoka kwa Arrahman ila wao hujitenga nao فَقَدۡ كَذَّبُواْ فَسَيَأۡتِيهِمۡ أَنۢبَٰٓؤُاْ مَا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ ٦Kwa yakini wamekanusha; kwa hivyo zitakuja wafikia khabari za yale waliyo kuwa wakiyafanyia mzaha أَوَلَمۡ يَرَوۡاْ إِلَى ٱلۡأَرۡضِ كَمۡ أَنۢبَتۡنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوۡجٍ كَرِيمٍ ٧Je! Hawakuiona ardhi, mimea mingapi tumeiotesha humo, ya kila namna nzuri إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةًۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ ٨Hakika katika haya zipo Ishara. Lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ ٩Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu وَإِذۡ نَادَىٰ رَبُّكَ مُوسَىٰٓ أَنِ ٱئۡتِ ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّٰلِمِينَ ١٠Na Mola wako Mlezi, alipo mwita Musa, akamwambia: Fika kwa watu madhaalimu قَوۡمَ فِرۡعَوۡنَۚ أَلَا يَتَّقُونَ ١١Watu wa Firauni. Hawaogopi قَالَ رَبِّ إِنِّيٓ أَخَافُ أَن يُكَذِّبُونِ ١٢Akasema: Hakika mimi nachelea wasinikanushe وَيَضِيقُ صَدۡرِي وَلَا يَنطَلِقُ لِسَانِي فَأَرۡسِلۡ إِلَىٰ هَٰرُونَ ١٣Na kifua changu kina dhiki, na ulimi wangu haukunjuki vyema. Basi mtumie ujumbe Harun وَلَهُمۡ عَلَيَّ ذَنۢبٌ فَأَخَافُ أَن يَقۡتُلُونِ ١٤Na wao wana kisasi juu yangu, kwa hivyo naogopa wasije kuniuwa قَالَ كـَلَّاۖ فَٱذۡهَبَا بِـَٔايَٰتِنَآۖ إِنَّا مَعَكُم مُّسۡتَمِعُونَ ١٥Akasema: Siyo hivyo kabisa! Nendeni na miujiza yetu. Hakika Sisi tu pamoja nanyi, tunasikiliza فَأۡتِيَا فِرۡعَوۡنَ فَقُولَآ إِنَّا رَسُولُ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ١٦Basi mfikieni Firauni na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote أَنۡ أَرۡسِلۡ مَعَنَا بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ١٧Waachilie Wana wa Israili wende nasi قَالَ أَلَمۡ نُرَبِّكَ فِينَا وَلِيدًا وَلَبِثۡتَ فِينَا مِنۡ عُمُرِكَ سِنِينَ ١٨(Firauni) akasema: Sisi hatukukulea wewe utotoni, na ukakaa kwetu katika umri wako miaka mingi وَفَعَلۡتَ فَعۡلَتَكَ ٱلَّتِي فَعَلۡتَ وَأَنتَ مِنَ ٱلۡكَٰفِرِينَ ١٩Na ukatenda kitendo chako ulicho tenda, nawe ukawa miongoni mwa wasio na shukrani قَالَ فَعَلۡتُهَآ إِذًا وَأَنَا۠ مِنَ ٱلضَّآلِّينَ ٢٠(Musa) akasema: Nilitenda hayo hapo nilipo kuwa miongoni mwa wale walio potea فَفَرَرۡتُ مِنكُمۡ لَمَّا خِفۡتُكُمۡ فَوَهَبَ لِي رَبِّي حُكۡمًا وَجَعَلَنِي مِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ ٢١Basi nikakukimbieni nilipo kuogopeni, tena Mola wangu Mlezi akanitunukia hukumu, na akanijaalia niwe miongoni mwa Mitume وَتِلۡكَ نِعۡمَةٌ تَمُنُّهَا عَلَيَّ أَنۡ عَبَّدتَّ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ٢٢Na hiyo ndiyo neema ya kunisumbulia, na wewe umewatia utumwani Wana wa Israili قَالَ فِرۡعَوۡنُ وَمَا رَبُّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ٢٣Firauni akasema: Na nani huyo Mola Mlezi wa walimwengu wote قَالَ رَبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَآۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ ٢٤Akasema: Ndiye Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na viliomo baina yao, ikiwa nyinyi ni wenye yakini قَالَ لِمَنۡ حَوۡلَهُۥٓ أَلَا تَسۡتَمِعُونَ ٢٥(Firauni) akawaambia walio mzunguka: Hamsikilizi قَالَ رَبُّكُمۡ وَرَبُّ ءَابَآئِكُمُ ٱلۡأَوَّلِينَ ٢٦(Musa) akasema: Ndiye Mola wenu Mlezi, na Mola Mlezi wa baba zenu wa kwanza قَالَ إِنَّ رَسُولَكُمُ ٱلَّذِيٓ أُرۡسِلَ إِلَيۡكُمۡ لَمَجۡنُونٌ ٢٧(Firauni) akasema: Hakika huyu Mtume wenu aliye tumwa kwenu ni mwendawazimu قَالَ رَبُّ ٱلۡمَشۡرِقِ وَٱلۡمَغۡرِبِ وَمَا بَيۡنَهُمَآۖ إِن كُنتُمۡ تَعۡقِلُونَ ٢٨(Musa) akasema: Ndiye Mola Mlezi wa Mashariki na Magharibi na viliomo baina yao, ikiwa nyinyi mnatia akilini قَالَ لَئِنِ ٱتَّخَذۡتَ إِلَٰهًا غَيۡرِي لَأَجۡعَلَنَّكَ مِنَ ٱلۡمَسۡجُونِينَ ٢٩(Firauni) akasema: Ukimfuata mungu mwengine asiye kuwa mimi, basi bila ya shaka nitakufunga gerezani قَالَ أَوَلَوۡ جِئۡتُكَ بِشَيۡءٍ مُّبِينٍ ٣٠Akasema: Je! Ijapo kuwa nitakuletea kitu cha kubainisha wazi قَالَ فَأۡتِ بِهِۦٓ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ ٣١Akasema: Kilete basi, kama wewe ni katika wasemao kweli فَأَلۡقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ ثُعۡبَانٌ مُّبِينٌ ٣٢Basi akaitupa fimbo yake, mara ikawa nyoka wa kuonekana dhaahiri وَنَزَعَ يَدَهُۥ فَإِذَا هِيَ بَيۡضَآءُ لِلنَّٰظِرِينَ ٣٣Na akautoa mkono wake, na mara ukawa mweupe kwa watazamao قَالَ لِلۡمَلَإِ حَوۡلَهُۥٓ إِنَّ هَٰذَا لَسَٰحِرٌ عَلِيمٌ ٣٤(Firauni) akawaambia waheshimiwa walio mzunguka: Hakika huyu ni mchawi mtaalamu يُرِيدُ أَن يُخۡرِجَكُم مِّنۡ أَرۡضِكُم بِسِحۡرِهِۦ فَمَاذَا تَأۡمُرُونَ ٣٥Anataka kukutoeni katika nchi yenu kwa uchawi wake. Basi mna shauri gani قَالُوٓاْ أَرۡجِهۡ وَأَخَاهُ وَٱبۡعَثۡ فِي ٱلۡمَدَآئِنِ حَٰشِرِينَ ٣٦Wakasema: Mpe muda yeye na nduguye na uwatume mijini wapigao mbiu ya mgambo يَأۡتُوكَ بِكُلِّ سَحَّارٍ عَلِيمٍ ٣٧Wakuletee kila mchawi bingwa mtaalamu فَجُمِعَ ٱلسَّحَرَةُ لِمِيقَٰتِ يَوۡمٍ مَّعۡلُومٍ ٣٨Basi wakakusanywa wachawi wakati na siku maalumu وَقِيلَ لِلنَّاسِ هَلۡ أَنتُم مُّجۡتَمِعُونَ ٣٩Na watu wakaambiwa: Je! Mtakusanyika لَعَلَّنَا نَتَّبِعُ ٱلسَّحَرَةَ إِن كَانُواْ هُمُ ٱلۡغَٰلِبِينَ ٤٠Huenda tutawafuata wachawi wakiwa wao ndio watakao shinda فَلَمَّا جَآءَ ٱلسَّحَرَةُ قَالُواْ لِفِرۡعَوۡنَ أَئِنَّ لَنَا لَأَجۡرًا إِن كُنَّا نَحۡنُ ٱلۡغَٰلِبِينَ ٤١Basi walipo kuja wachawi wakamwambia Firauni: Je! Tutapata ujira tukiwa sisi ndio tulio shinda قَالَ نَعَمۡ وَإِنَّكُمۡ إِذًا لَّمِنَ ٱلۡمُقَرَّبِينَ ٤٢Naam! Na hakika mtakuwa katika watu wa mbele قَالَ لَهُم مُّوسَىٰٓ أَلۡقُواْ مَآ أَنتُم مُّلۡقُونَ ٤٣Musa akwaambia: Tupeni mnavyo taka kutupa فَأَلۡقَوۡاْ حِبَالَهُمۡ وَعِصِيَّهُمۡ وَقَالُواْ بِعِزَّةِ فِرۡعَوۡنَ إِنَّا لَنَحۡنُ ٱلۡغَٰلِبُونَ ٤٤Basi wakatupa kamba zao na fimbo zao, na wakasema: Kwa nguvu za Firauni hakika sisi hapana shaka ni wenye kushinda فَأَلۡقَىٰ مُوسَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ تَلۡقَفُ مَا يَأۡفِكُونَ ٤٥Musa tena akatupa fimbo yake, nayo mara ikavimeza walivyo vizua فَأُلۡقِيَ ٱلسَّحَرَةُ سَٰجِدِينَ ٤٦Hapo wachawi walipinduka wakasujudu قَالُوٓاْ ءَامَنَّا بِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ٤٧Wakasema: Tunamuamini Mola Mlezi wa walimwengu wote رَبِّ مُوسَىٰ وَهَٰرُونَ ٤٨Mola Mlezi wa Musa na Harun قَالَ ءَامَنتُمۡ لَهُۥ قَبۡلَ أَنۡ ءَاذَنَ لَكُمۡۖ إِنَّهُۥ لَكَبِيرُكُمُ ٱلَّذِي عَلَّمَكُمُ ٱلسِّحۡرَ فَلَسَوۡفَ تَعۡلَمُونَۚ لَأُقَطِّعَنَّ أَيۡدِيَكُمۡ وَأَرۡجُلَكُم مِّنۡ خِلَٰفٍ وَلَأُصَلِّبَنَّكُمۡ أَجۡمَعِينَ ٤٩(Firauni) akasema: Je! Mmemuamini kabla sijakuruhusuni? Bila ya shaka yeye basi ndiye mkubwa wenu aliye kufunzeni uchawi. Basi mtakuja jua! Nitakata mikono yenu na miguu yenu kwa kutafautisha. Na nitakubandikeni misalabani nyote قَالُواْ لَا ضَيۡرَۖ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا مُنقَلِبُونَ ٥٠Wakasema: Haidhuru, kwani sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi إِنَّا نَطۡمَعُ أَن يَغۡفِرَ لَنَا رَبُّنَا خَطَٰيَٰنَآ أَن كُنَّآ أَوَّلَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ٥١Hakika sisi tunatumai Mola wetu Mlezi atatusamehe makosa yetu, kwa kuwa ndio wa kwanza wa kuamini ۞ وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنۡ أَسۡرِ بِعِبَادِيٓ إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ ٥٢Na tulimuamrisha Musa kwa wahyi: Nenda na waja wangu wakati wa usiku. Kwa hakika mtafuatwa فَأَرۡسَلَ فِرۡعَوۡنُ فِي ٱلۡمَدَآئِنِ حَٰشِرِينَ ٥٣Basi Firauni akawatuma mijini wapiga mbiu za mgambo إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ لَشِرۡذِمَةٌ قَلِيلُونَ ٥٤(Wakieneza): Hakika hawa ni kikundi kidogo وَإِنَّهُمۡ لَنَا لَغَآئِظُونَ ٥٥Nao wanatuudhi وَإِنَّا لَجَمِيعٌ حَٰذِرُونَ ٥٦Na sisi ni wengi, wenye kuchukua hadhari فَأَخۡرَجۡنَٰهُم مِّن جَنَّٰتٍ وَعُيُونٍ ٥٧Basi tukawatoa katika mabustani na chemchem وَكُنُوزٍ وَمَقَامٍ كَرِيمٍ ٥٨Na makhazina, na vyeo vya hishima كَذَٰلِكَۖ وَأَوۡرَثۡنَٰهَا بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ٥٩Kadhaalika; na tukawarithisha hayo Wana wa Israili فَأَتۡبَعُوهُم مُّشۡرِقِينَ ٦٠Basi wakawafuata lilipo chomoza jua فَلَمَّا تَرَٰٓءَا ٱلۡجَمۡعَانِ قَالَ أَصۡحَٰبُ مُوسَىٰٓ إِنَّا لَمُدۡرَكُونَ ٦١Na yalipo onana majeshi mawili haya, watu wa Musa wakasema: Hakika sisi bila ya shaka tumepatikana قَالَ كـَلَّآۖ إِنَّ مَعِيَ رَبِّي سَيَهۡدِينِ ٦٢(Musa) akasema: Hasha! Hakika yu pamoja nami Mola wangu Mlezi. Yeye ataniongoa فَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنِ ٱضۡرِب بِّعَصَاكَ ٱلۡبَحۡرَۖ فَٱنفَلَقَ فَكَانَ كُلُّ فِرۡقٍ كَٱلطَّوۡدِ ٱلۡعَظِيمِ ٦٣Tulimletea wahyi Musa tukamwambia: Piga bahari kwa fimbo yako. Basi ikatengana, na kila sehemu ikawa kama mlima mkubwa وَأَزۡلَفۡنَا ثَمَّ ٱلۡأٓخَرِينَ ٦٤Na tukawajongeza hapo wale wengine وَأَنجَيۡنَا مُوسَىٰ وَمَن مَّعَهُۥٓ أَجۡمَعِينَ ٦٥Tukawaokoa Musa na walio kuwa pamoja naye wote ثُمَّ أَغۡرَقۡنَا ٱلۡأٓخَرِينَ ٦٦Kisha tukawazamisha hao wengine إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةًۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ ٦٧Hakika bila ya shaka katika hayo ipo Ishara; lakini wengi wao si katika wenye kuamini وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ ٦٨Na kwa hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu وَٱتۡلُ عَلَيۡهِمۡ نَبَأَ إِبۡرَٰهِيمَ ٦٩Na wasomee khabari za Ibrahim إِذۡ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوۡمِهِۦ مَا تَعۡبُدُونَ ٧٠Alipo mwambia baba yake na kaumu yake: Mnaabudu nini قَالُواْ نَعۡبُدُ أَصۡنَامًا فَنَظَلُّ لَهَا عَٰكِفِينَ ٧١Wakasema: Tunaabudu masanamu, daima tunayanyenyekea قَالَ هَلۡ يَسۡمَعُونَكُمۡ إِذۡ تَدۡعُونَ ٧٢Akasema: Je! Yanakusikieni mnapo yaita أَوۡ يَنفَعُونَكُمۡ أَوۡ يَضُرُّونَ ٧٣Au yanakufaeni, au yanakudhuruni قَالُواْ بَلۡ وَجَدۡنَآ ءَابَآءَنَا كَذَٰلِكَ يَفۡعَلُونَ ٧٤Wakasema: Bali tumewakuta baba zetu wakifanya hivyo hivyo قَالَ أَفَرَءَيۡتُم مَّا كُنتُمۡ تَعۡبُدُونَ ٧٥Je! Mmewaona hawa mnao waabudu أَنتُمۡ وَءَابَآؤُكُمُ ٱلۡأَقۡدَمُونَ ٧٦Nyinyi na baba zenu wa zamani فَإِنَّهُمۡ عَدُوٌّ لِّيٓ إِلَّا رَبَّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ٧٧Kwani hakika hao ni adui zangu, isipo kuwa Mola Mlezi wa walimwengu wote ٱلَّذِي خَلَقَنِي فَهُوَ يَهۡدِينِ ٧٨Ambaye ndiye aliye niumba, na Yeye ndiye ananiongoa وَٱلَّذِي هُوَ يُطۡعِمُنِي وَيَسۡقِينِ ٧٩Na ambaye ndiye ananilisha na kuninywesha وَإِذَا مَرِضۡتُ فَهُوَ يَشۡفِينِ ٨٠Na ninapo ugua ni Yeye ndiye anaye niponesha وَٱلَّذِي يُمِيتُنِي ثُمَّ يُحۡيِينِ ٨١Na ambaye atanifisha, na kisha atanihuisha وَٱلَّذِيٓ أَطۡمَعُ أَن يَغۡفِرَ لِي خَطِيٓـَٔتِي يَوۡمَ ٱلدِّينِ ٨٢Na ambaye ndiye ninaye mtumai kunisamehe makosa yangu Siku ya Malipo رَبِّ هَبۡ لِي حُكۡمًا وَأَلۡحِقۡنِي بِٱلصَّٰلِحِينَ ٨٣Mola wangu Mlezi! Nitunukie hukumu na uniunganishe na watendao mema وَٱجۡعَل لِّي لِسَانَ صِدۡقٍ فِي ٱلۡأٓخِرِينَ ٨٤Na unijaalie nitajwe kwa wema na watu watakao kuja baadaye وَٱجۡعَلۡنِي مِن وَرَثَةِ جَنَّةِ ٱلنَّعِيمِ ٨٥Na unijaalie katika warithi wa Bustani za neema وَٱغۡفِرۡ لِأَبِيٓ إِنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلضَّآلِّينَ ٨٦Na umsamehe baba yangu, kwani hakika alikuwa miongoni mwa wapotovu وَلَا تُخۡزِنِي يَوۡمَ يُبۡعَثُونَ ٨٧Wala usinihizi Siku watapo fufuliwa يَوۡمَ لَا يَنفَعُ مَالٌ وَلَا بَنُونَ ٨٨Siku ambayo kwamba mali hayato faa kitu wala wana إِلَّا مَنۡ أَتَى ٱللَّهَ بِقَلۡبٍ سَلِيمٍ ٨٩Isipo kuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyo safi وَأُزۡلِفَتِ ٱلۡجَنَّةُ لِلۡمُتَّقِينَ ٩٠Na Pepo itasogezwa kwa wachamngu وَبُرِّزَتِ ٱلۡجَحِيمُ لِلۡغَاوِينَ ٩١Na Jahannamu itadhihirishwa kwa wapotovu وَقِيلَ لَهُمۡ أَيۡنَ مَا كُنتُمۡ تَعۡبُدُونَ ٩٢Na wataambiwa: Wako wapi mlio kuwa mkiwaabudu مِن دُونِ ٱللَّهِ هَلۡ يَنصُرُونَكُمۡ أَوۡ يَنتَصِرُونَ ٩٣Badala ya Mwenyezi Mungu? Je! Wanakusaidieni, au wanajisaidia wenyewe فَكُبۡكِبُواْ فِيهَا هُمۡ وَٱلۡغَاوُۥنَ ٩٤Basi watavurumizwa humo wao na hao wakosefu وَجُنُودُ إِبۡلِيسَ أَجۡمَعُونَ ٩٥Na majeshi ya Ibilisi yote قَالُواْ وَهُمۡ فِيهَا يَخۡتَصِمُونَ ٩٦Watasema, na hali ya kuwa wanazozana humo تَٱللَّهِ إِن كُنَّا لَفِي ضَلَٰلٍ مُّبِينٍ ٩٧Wallahi! Kwa yakini tulikuwa katika upotovu ulio dhaahiri إِذۡ نُسَوِّيكُم بِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ٩٨Tulipo kufanyeni ni sawa na Mola Mlezi wa walimwengu wote وَمَآ أَضَلَّنَآ إِلَّا ٱلۡمُجۡرِمُونَ ٩٩Na hawakutupoteza ila wale wakosefu فَمَا لَنَا مِن شَٰفِعِينَ ١٠٠Basi hatuna waombezi وَلَا صَدِيقٍ حَمِيمٍ ١٠١Wala rafiki wa dhati فَلَوۡ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَكُونَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ١٠٢Laiti tungeli pata kurejea tena tungeli kuwa katika Waumini إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةًۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ ١٠٣Hakika katika haya ipo Ishara, lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ ١٠٤Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu كَذَّبَتۡ قَوۡمُ نُوحٍ ٱلۡمُرۡسَلِينَ ١٠٥Kaumu ya Nuhu waliwakadhibisha Mitume إِذۡ قَالَ لَهُمۡ أَخُوهُمۡ نُوحٌ أَلَا تَتَّقُونَ ١٠٦Alipo waambia ndugu yao, Nuhu: Je! Hamchimngu إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٌ ١٠٧Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ ١٠٨Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi وَمَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ١٠٩Na sikutakini juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ ١١٠Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi ۞ قَالُوٓاْ أَنُؤۡمِنُ لَكَ وَٱتَّبَعَكَ ٱلۡأَرۡذَلُونَ ١١١Wakasema: Je! Tukuamini wewe, hali wanao kufuata ni watu wa chini قَالَ وَمَا عِلۡمِي بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ ١١٢Akasema: Nayajuaje waliyo kuwa wakiyafanya إِنۡ حِسَابُهُمۡ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّيۖ لَوۡ تَشۡعُرُونَ ١١٣Hisabu yao haiko ila kwa Mola wao Mlezi, laiti mngeli tambua وَمَآ أَنَا۠ بِطَارِدِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ١١٤Wala mimi si wa kuwafukuza Waumini إِنۡ أَنَا۠ إِلَّا نَذِيرٌ مُّبِينٌ ١١٥Mimi si cho chote ila ni Mwonyaji wa dhaahiri shaahiri قَالُواْ لَئِن لَّمۡ تَنتَهِ يَٰنُوحُ لَتَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمَرۡجُومِينَ ١١٦Wakasema: Ikiwa huachi, ewe Nuhu, bila ya shaka utapigwa mawe قَالَ رَبِّ إِنَّ قَوۡمِي كَذَّبُونِ ١١٧Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikanusha فَٱفۡتَحۡ بَيۡنِي وَبَيۡنَهُمۡ فَتۡحًا وَنَجِّنِي وَمَن مَّعِيَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ١١٨Basi hukumu baina yangu na wao kwa hukumu yako, na uniokoe mimi na walio pamoja nami, Waumini فَأَنجَيۡنَٰهُ وَمَن مَّعَهُۥ فِي ٱلۡفُلۡكِ ٱلۡمَشۡحُونِ ١١٩Kwa hivyo tukamwokoa yeye na walio kuwa pamoja naye katika marikebu iliyo sheheni ثُمَّ أَغۡرَقۡنَا بَعۡدُ ٱلۡبَاقِينَ ١٢٠Kisha tukawazamisha baadaye walio bakia إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةًۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ ١٢١Hakika katika haya ipo Ishara, lakini si wengi wao walio kuwa Waumini وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ ١٢٢Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu كَذَّبَتۡ عَادٌ ٱلۡمُرۡسَلِينَ ١٢٣Kina A'd waliwakanusha Mitume إِذۡ قَالَ لَهُمۡ أَخُوهُمۡ هُودٌ أَلَا تَتَّقُونَ ١٢٤Alipo waambia ndugu yao, Hud: Je! Hamchimngu إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٌ ١٢٥Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ ١٢٦Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi وَمَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ١٢٧Wala sikutakeni juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote أَتَبۡنُونَ بِكُلِّ رِيعٍ ءَايَةً تَعۡبَثُونَ ١٢٨Je! Mnajenga juu ya kila mnyanyuko kumbusho la kufanyia upuuzi وَتَتَّخِذُونَ مَصَانِعَ لَعَلَّكُمۡ تَخۡلُدُونَ ١٢٩Na mnajenga majengo ya fakhari kama kwamba mtaishi milele وَإِذَا بَطَشۡتُم بَطَشۡتُمۡ جَبَّارِينَ ١٣٠Na mnapo tumia nguvu mnatumia nguvu kwa ujabari فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ ١٣١Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini وَٱتَّقُواْ ٱلَّذِيٓ أَمَدَّكُم بِمَا تَعۡلَمُونَ ١٣٢Na mcheni aliye kupeni haya mnayo yajua أَمَدَّكُم بِأَنۡعَٰمٍ وَبَنِينَ ١٣٣Amekupeni wanyama wa kufuga na wana وَجَنَّٰتٍ وَعُيُونٍ ١٣٤Na mabustani na chemchem إِنِّيٓ أَخَافُ عَلَيۡكُمۡ عَذَابَ يَوۡمٍ عَظِيمٍ ١٣٥Hakika mimi ninakukhofieni adhabu ya Siku Kubwa قَالُواْ سَوَآءٌ عَلَيۡنَآ أَوَعَظۡتَ أَمۡ لَمۡ تَكُن مِّنَ ٱلۡوَٰعِظِينَ ١٣٦Wakasema: Ni mamoja kwetu, ukitupa mawaidha au hukuwa miongoni mwa watoao mawaidha إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا خُلُقُ ٱلۡأَوَّلِينَ ١٣٧Haya si chochote ila ni mtindo wa watu wa tokea zamani وَمَا نَحۡنُ بِمُعَذَّبِينَ ١٣٨Wala sisi hatutaadhibiwa فَكَذَّبُوهُ فَأَهۡلَكۡنَٰهُمۡۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةًۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ ١٣٩Wakamkanusha; nasi tukawaangamiza. Hakika bila ya shaka katika haya ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ ١٤٠Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu كَذَّبَتۡ ثَمُودُ ٱلۡمُرۡسَلِينَ ١٤١Kina Thamud waliwakanusha Mitume إِذۡ قَالَ لَهُمۡ أَخُوهُمۡ صَٰلِحٌ أَلَا تَتَّقُونَ ١٤٢Alipo waambia ndugu yao Saleh: Je! Hamumchimngu إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٌ ١٤٣Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ ١٤٤Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini وَمَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ١٤٥Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote أَتُتۡرَكُونَ فِي مَا هَٰهُنَآ ءَامِنِينَ ١٤٦Je! Mtaachwa salama usalimina katika haya yaliyopo hapa فِي جَنَّٰتٍ وَعُيُونٍ ١٤٧Katika mabustani, na chemchem وَزُرُوعٍ وَنَخۡلٍ طَلۡعُهَا هَضِيمٌ ١٤٨Na konde na mitende yenye makole yaliyo wiva وَتَنۡحِتُونَ مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتًا فَٰرِهِينَ ١٤٩Na mnachonga milimani majumba kwa ustadi فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ ١٥٠Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi وَلَا تُطِيعُوٓاْ أَمۡرَ ٱلۡمُسۡرِفِينَ ١٥١Wala msit'ii amri za walio pindukia mipaka ٱلَّذِينَ يُفۡسِدُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا يُصۡلِحُونَ ١٥٢Ambao wanafanya ufisadi katika nchi, wala hawatengenezi قَالُوٓاْ إِنَّمَآ أَنتَ مِنَ ٱلۡمُسَحَّرِينَ ١٥٣Wakasema: Hakika wewe ni miongoni mwa walio rogwa مَآ أَنتَ إِلَّا بَشَرٌ مِّثۡلُنَا فَأۡتِ بِـَٔايَةٍ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ ١٥٤Wewe si chochote ila ni mtu kama sisi. Basi lete Ishara ukiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli قَالَ هَٰذِهِۦ نَاقَةٌ لَّهَا شِرۡبٌ وَلَكُمۡ شِرۡبُ يَوۡمٍ مَّعۡلُومٍ ١٥٥Akasema: Huyu ngamia jike; awe na zamu yake ya kunywa, na nyinyi muwe na zamu yenu ya kunywa katika siku maalumu وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوٓءٍ فَيَأۡخُذَكُمۡ عَذَابُ يَوۡمٍ عَظِيمٍ ١٥٦Wala msimguse kwa uwovu, isije ikakushikeni adhabu ya Siku Kubwa فَعَقَرُوهَا فَأَصۡبَحُواْ نَٰدِمِينَ ١٥٧Lakini wakamuuwa, na wakawa wenye kujuta فَأَخَذَهُمُ ٱلۡعَذَابُۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةًۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ ١٥٨Basi ikawapata adhabu. Hakika katika hayo ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ ١٥٩Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu كَذَّبَتۡ قَوۡمُ لُوطٍ ٱلۡمُرۡسَلِينَ ١٦٠Watu wa Lut'i waliwakanusha Mitume إِذۡ قَالَ لَهُمۡ أَخُوهُمۡ لُوطٌ أَلَا تَتَّقُونَ ١٦١Alipo waambia ndugu yao, Lut'i: Je! Hamumchimngu إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٌ ١٦٢Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu kwenu فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ ١٦٣Basi mcheni Mwenyezi Mungu na nit'iini mimi وَمَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ١٦٤Wala mimi sikutakini ujira juu yake; ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote أَتَأۡتُونَ ٱلذُّكۡرَانَ مِنَ ٱلۡعَٰلَمِينَ ١٦٥Je! Katika viumbe vyote mnawaingilia wanaume وَتَذَرُونَ مَا خَلَقَ لَكُمۡ رَبُّكُم مِّنۡ أَزۡوَٰجِكُمۚ بَلۡ أَنتُمۡ قَوۡمٌ عَادُونَ ١٦٦Na mnaacha alicho kuumbieni Mola wenu Mlezi katika wake zenu? Ama kweli nyinyi ni watu mnao ruka mipaka قَالُواْ لَئِن لَّمۡ تَنتَهِ يَٰلُوطُ لَتَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُخۡرَجِينَ ١٦٧Wakasema: Ewe Lut'i! Usipo acha, hapana shaka utakuwa miongoni mwa wanao tolewa mji قَالَ إِنِّي لِعَمَلِكُم مِّنَ ٱلۡقَالِينَ ١٦٨Akasema: Hakika mimi ni katika wanao kichukia hichi kitendo chenu رَبِّ نَجِّنِي وَأَهۡلِي مِمَّا يَعۡمَلُونَ ١٦٩Mola wangu Mlezi! Niokoe mimi na ahali zangu na haya wayatendayo فَنَجَّيۡنَٰهُ وَأَهۡلَهُۥٓ أَجۡمَعِينَ ١٧٠Basi tukamwokoa yeye na ahali zake wote إِلَّا عَجُوزًا فِي ٱلۡغَٰبِرِينَ ١٧١Isipo kuwa kikongwe katika walio kaa nyuma ثُمَّ دَمَّرۡنَا ٱلۡأٓخَرِينَ ١٧٢Kisha tukawaangamiza wale wengine وَأَمۡطَرۡنَا عَلَيۡهِم مَّطَرًاۖ فَسَآءَ مَطَرُ ٱلۡمُنذَرِينَ ١٧٣Na tukawanyeshea mvua, basi ni ovu mno mvua ya waliyo onywa إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةًۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ ١٧٤Hakika katika hayo ipo Ishara. Na hawakuwa wengi wao wenye kuamini وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ ١٧٥Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu كَذَّبَ أَصۡحَٰبُ لۡـَٔيۡكَةِ ٱلۡمُرۡسَلِينَ ١٧٦Watu wa Machakani waliwakanusha Mitume إِذۡ قَالَ لَهُمۡ شُعَيۡبٌ أَلَا تَتَّقُونَ ١٧٧Shuaibu alipo waambia: Je! Hamfanyi mkamchamngu إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٌ ١٧٨Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ ١٧٩Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi وَمَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ١٨٠Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote ۞ أَوۡفُواْ ٱلۡكَيۡلَ وَلَا تَكُونُواْ مِنَ ٱلۡمُخۡسِرِينَ ١٨١Timizeni kipimo sawa sawa, wala msiwe katika wanao punja وَزِنُواْ بِٱلۡقِسۡطَاسِ ٱلۡمُسۡتَقِيمِ ١٨٢Na pimeni kwa haki iliyo nyooka وَلَا تَبۡخَسُواْ ٱلنَّاسَ أَشۡيَآءَهُمۡ وَلَا تَعۡثَوۡاْ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُفۡسِدِينَ ١٨٣Wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye jeuri kwa ufisadi وَٱتَّقُواْ ٱلَّذِي خَلَقَكُمۡ وَٱلۡجِبِلَّةَ ٱلۡأَوَّلِينَ ١٨٤Na mcheni aliye kuumbeni nyinyi na vizazi vilivyo tangulia قَالُوٓاْ إِنَّمَآ أَنتَ مِنَ ٱلۡمُسَحَّرِينَ ١٨٥Wakasema: Hakika wewe ni katika walio rogwa وَمَآ أَنتَ إِلَّا بَشَرٌ مِّثۡلُنَا وَإِن نَّظُنُّكَ لَمِنَ ٱلۡكَٰذِبِينَ ١٨٦Na wewe si chochote ila ni mtu tu kama sisi, na kwa yakini tunakuona wewe ni katika waongo فَأَسۡقِطۡ عَلَيۡنَا كِسَفًا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ ١٨٧Hebu tuangushie vipande kutoka mbinguni ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli قَالَ رَبِّيٓ أَعۡلَمُ بِمَا تَعۡمَلُونَ ١٨٨Akasema: Mola wangu Mlezi anajua zaidi mnayo yatenda فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَهُمۡ عَذَابُ يَوۡمِ ٱلظُّلَّةِۚ إِنَّهُۥ كَانَ عَذَابَ يَوۡمٍ عَظِيمٍ ١٨٩Basi walimkanusha, na ikawashika adhabu ya siku ya kivuli. Hakika hiyo ilikuwa adhabu ya siku kubwa إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةًۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ ١٩٠Hakika katika hayo ipo Ishara, lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ ١٩١Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu وَإِنَّهُۥ لَتَنزِيلُ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ١٩٢Na bila ya shaka hii ni Uteremsho wa Mola Mlezi wa walimwengu wote نَزَلَ بِهِ ٱلرُّوحُ ٱلۡأَمِينُ ١٩٣Ameuteremsha Roho muaminifu عَلَىٰ قَلۡبِكَ لِتَكُونَ مِنَ ٱلۡمُنذِرِينَ ١٩٤Juu ya moyo wako, ili uwe katika Waonyaji بِلِسَانٍ عَرَبِيٍّ مُّبِينٍ ١٩٥Kwa ulimi wa Kiarabu ulio wazi وَإِنَّهُۥ لَفِي زُبُرِ ٱلۡأَوَّلِينَ ١٩٦Na hakika bila ya shaka haya yamo katika Vitabu vya kale أَوَلَمۡ يَكُن لَّهُمۡ ءَايَةً أَن يَعۡلَمَهُۥ عُلَمَٰٓؤُاْ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ١٩٧Je! Haikuwa kwao ni Ishara kwamba wanayajua haya wanazuoni wa Wana wa Israili وَلَوۡ نَزَّلۡنَٰهُ عَلَىٰ بَعۡضِ ٱلۡأَعۡجَمِينَ ١٩٨Na lau kuwa tungeli iteremsha juu ya mmoja wa wasio kuwa Waarabu فَقَرَأَهُۥ عَلَيۡهِم مَّا كَانُواْ بِهِۦ مُؤۡمِنِينَ ١٩٩Na akawasomea, wasingeli kuwa wenye kuamini كَذَٰلِكَ سَلَكۡنَٰهُ فِي قُلُوبِ ٱلۡمُجۡرِمِينَ ٢٠٠Namna hivi tunaingiza katika nyoyo za wakosefu لَا يُؤۡمِنُونَ بِهِۦ حَتَّىٰ يَرَوُاْ ٱلۡعَذَابَ ٱلۡأَلِيمَ ٢٠١Hawataiamini mpaka waione adhabu chungu فَيَأۡتِيَهُم بَغۡتَةً وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ ٢٠٢Basi itawafikia kwa ghafla, na hali hawana khabari فَيَقُولُواْ هَلۡ نَحۡنُ مُنظَرُونَ ٢٠٣Na watasema: Je, tutapewa muhula أَفَبِعَذَابِنَا يَسۡتَعۡجِلُونَ ٢٠٤Basi, je, wanaihimiza adhabu yetu أَفَرَءَيۡتَ إِن مَّتَّعۡنَٰهُمۡ سِنِينَ ٢٠٥Waonaje kama tukiwastarehesha kwa miaka ثُمَّ جَآءَهُم مَّا كَانُواْ يُوعَدُونَ ٢٠٦Kisha yakawafikia waliyo kuwa wakiahidiwa مَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يُمَتَّعُونَ ٢٠٧Yatawafaa nini yale waliyo stareheshewa وَمَآ أَهۡلَكۡنَا مِن قَرۡيَةٍ إِلَّا لَهَا مُنذِرُونَ ٢٠٨Wala hatukuangamiza mji wo wote ila ulikuwa na waonyaji ذِكۡرَىٰ وَمَا كُنَّا ظَٰلِمِينَ ٢٠٩Kuwa ni ukumbusho. Wala Sisi hatukuwa wenye kudhulumu وَمَا تَنَزَّلَتۡ بِهِ ٱلشَّيَٰطِينُ ٢١٠Wala Mashet'ani hawakuteremka nayo وَمَا يَنۢبَغِي لَهُمۡ وَمَا يَسۡتَطِيعُونَ ٢١١Wala haitakiwi kwao, na wala hawawezi إِنَّهُمۡ عَنِ ٱلسَّمۡعِ لَمَعۡزُولُونَ ٢١٢Hakika hao wametengwa na kusikia فَلَا تَدۡعُ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَ فَتَكُونَ مِنَ ٱلۡمُعَذَّبِينَ ٢١٣Basi usimwombe mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu ukawa miongoni mwa watakao adhibiwa وَأَنذِرۡ عَشِيرَتَكَ ٱلۡأَقۡرَبِينَ ٢١٤Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe وَٱخۡفِضۡ جَنَاحَكَ لِمَنِ ٱتَّبَعَكَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ٢١٥Na watwae kwa upole wanao kufuata miongoni mwa Waumini فَإِنۡ عَصَوۡكَ فَقُلۡ إِنِّي بَرِيٓءٌ مِّمَّا تَعۡمَلُونَ ٢١٦Na ikiwa watakuasi basi sema: Mimi najitenga mbali na hayo mnayo yatenda وَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱلۡعَزِيزِ ٱلرَّحِيمِ ٢١٧Na umtegemee Mtukufu Mwenye nguvu Mwenye kurehemu ٱلَّذِي يَرَىٰكَ حِينَ تَقُومُ ٢١٨Ambaye anakuona unapo simama وَتَقَلُّبَكَ فِي ٱلسَّٰجِدِينَ ٢١٩Na mageuko yako kati ya wanao sujudu إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ ٢٢٠Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua هَلۡ أُنَبِّئُكُمۡ عَلَىٰ مَن تَنَزَّلُ ٱلشَّيَٰطِينُ ٢٢١Je! Nikwambieni nani wanawashukia Mashet'ani تَنَزَّلُ عَلَىٰ كُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٍ ٢٢٢Wanamshukia kila mzushi mkubwa mwingi wa dhambi يُلۡقُونَ ٱلسَّمۡعَ وَأَكۡثَرُهُمۡ كَٰذِبُونَ ٢٢٣Wanawapelekea yale wanayo yasikia; na wengi wao ni waongo وَٱلشُّعَرَآءُ يَتَّبِعُهُمُ ٱلۡغَاوُۥنَ ٢٢٤Na watungaji mashairi ni wapotofu ndio wanawafuata أَلَمۡ تَرَ أَنَّهُمۡ فِي كُلِّ وَادٍ يَهِيمُونَ ٢٢٥Je! Huwaoni kwamba wao wanatangatanga katika kila bonde وَأَنَّهُمۡ يَقُولُونَ مَا لَا يَفۡعَلُونَ ٢٢٦Na kwamba wao husema wasiyo yatenda إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ وَذَكَرُواْ ٱللَّهَ كَثِيرًا وَٱنتَصَرُواْ مِنۢ بَعۡدِ مَا ظُلِمُواْۗ وَسَيَعۡلَمُ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوٓاْ أَيَّ مُنقَلَبٍ يَنقَلِبُونَ ٢٢٧Isipo kuwa wale walio amini, na wakatenda mema, na wakamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi, na wakajitetea wanapo dhulumiwa. Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka