Millat al-Islam

Chapter 87 · 19 verses · Abdullah Muhammad Abu Bakr

Surah Al-Ala in Swahili

Arabic with tafsir Listen to Surah Al-Ala (1421 reciters)
Meccanسورة الأعلى19 verses

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

سَبِّحِ ٱسۡمَ رَبِّكَ ٱلۡأَعۡلَى ١Takasa Jina la Mola wako Aliyetukuka na kuepukana na mshirika na kila sifa pungufu kwa namna inayonasibiana na utukufu Wake na utakatifu Wake ٱلَّذِي خَلَقَ فَسَوَّىٰ ٢Aliyeumba viumbe Akalitengeneza umbo lao na kulifanya zuri وَٱلَّذِي قَدَّرَ فَهَدَىٰ ٣Na Aliyekadiria kila kitu na kukipeleka njia inayonasibiana nacho وَٱلَّذِيٓ أَخۡرَجَ ٱلۡمَرۡعَىٰ ٤Na Aliyeotesha nyasi mbiti zenye rangi ya kijani فَجَعَلَهُۥ غُثَآءً أَحۡوَىٰ ٥Akazifanya baadaye kuwa kavu zilizobadilika rangi سَنُقۡرِئُكَ فَلَا تَنسَىٰٓ ٦Tutakusomea, ewe Mtume, hii Qur’ani kisomo ambacho hutakisahau إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُۚ إِنَّهُۥ يَعۡلَمُ ٱلۡجَهۡرَ وَمَا يَخۡفَىٰ ٧Isipokuwa iwapo Mwenyezi Mungu Ataka usahau kwa hekima na maslahi anayoyajua Yeye. Kwani Yeye ni Mjuzi wa yaliyo wazi na yaliyofichika, ya maneno na ya vitendo وَنُيَسِّرُكَ لِلۡيُسۡرَىٰ ٨Tutakufanyia mapesi mambo yako yote; miongoni mwayo ni kukusahilishia kubeba majukumu ya utume na kuifanya nyepesi Dini uliyokuja nayo فَذَكِّرۡ إِن نَّفَعَتِ ٱلذِّكۡرَىٰ ٩Basi wawaidhie kaumu zako, ewe Mtume, kwa namna tulivyokutayarishia ufanye kwenye wahyi ulioletewa, uwaongoze njia yenye kheri na wao na uwahusu kwa mawaidha yako wale wanaotarajiwa kuwaidhika nayo. Wala usijisumbue kuwashauri wale ambao mawidha hayawaathiri isipokuwa kuwatia ujeuri na kuwafanya wayakimbie سَيَذَّكَّرُ مَن يَخۡشَىٰ ١٠Atanufaika kwa mawaidha anayemcha Mola wke وَيَتَجَنَّبُهَا ٱلۡأَشۡقَى ١١na atajiepusha na mawaidha aliye mbaya asiyemuogopa Mola wake ٱلَّذِي يَصۡلَى ٱلنَّارَ ٱلۡكُبۡرَىٰ ١٢atakayeingia kwenye Moto wa Jahanamu akiadhibika kwa ukali wake ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحۡيَىٰ ١٣Kisha hatakuwa ni mwenye kufa akapumzika wala ni mwenye kuishi akanufaika قَدۡ أَفۡلَحَ مَن تَزَكَّىٰ ١٤Hakika amefuzu mwenye kuisafisha nafsi yake na tabia mbovu وَذَكَرَ ٱسۡمَ رَبِّهِۦ فَصَلَّىٰ ١٥na akamtaja Mwenyezi Mungu, akampwekesha, akamuomba, akafanya vitendo vya kumridhisha na akasimamisha Swala kwa nyakati zake kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu na kufuata sheria Aliyoiweka بَلۡ تُؤۡثِرُونَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا ١٦Hakika yenu, nyinyi watu, mnafadhilisha pambo la maisha ya kilimwengu juu ya starehe za Akhera وَٱلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٌ وَأَبۡقَىٰٓ ١٧Na hakika ya mambo ni kuwa nyumba ya Akhera na starehe zake ni bora zaidi kuliko ulimwngu na ni yenye kusalia zaidi إِنَّ هَٰذَا لَفِي ٱلصُّحُفِ ٱلۡأُولَىٰ ١٨Haya mlioosimuliwa ndani ya Sura hii ni miongoni mwa yaliyotajwa kimaana katika Kurasa zilizotangulia kuteremshwa kabla ya Qur’ani صُحُفِ إِبۡرَٰهِيمَ وَمُوسَىٰ ١٩Nazo ni Kurasa za Ibrāhīm na Mūsā, amani ziwashukie

Translation: Abdullah Muhammad Abu Bakr.