Millat al-Islam

Chapter 88 · 26 verses · Abdullah Muhammad Abu Bakr

Surah Al-Ghashiya in Swahili

Arabic with tafsir Listen to Surah Al-Ghashiya (1299 reciters)

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلۡغَٰشِيَةِ ١Je, ilikujia,ewe Mtume, habari ya Kiyama chenye vituko venye kuwaenea watu وُجُوهٌ يَوۡمَئِذٍ خَٰشِعَةٌ ٢Nyuso za Makafiri, Siku hiyo, zitakuwa zimenyongeka kwa adhabu عَامِلَةٌ نَّاصِبَةٌ ٣Zishughulishie, zimechoka na kutaabika تَصۡلَىٰ نَارًا حَامِيَةً ٤Zinachomwa kwa Moto wenye kuwaka kwa ukali تُسۡقَىٰ مِنۡ عَيۡنٍ ءَانِيَةٍ ٥Zitanyweshwa maji ya chemchemi yenye moto sana لَّيۡسَ لَهُمۡ طَعَامٌ إِلَّا مِن ضَرِيعٍ ٦Watu wa Motoni hawatakuwa na chakula isipokuwa kinachotoka kwenye mti wa miba ilioshikana na chini. Ni kibaya sana chakula hiko na ni kichafu mno لَّا يُسۡمِنُ وَلَا يُغۡنِي مِن جُوعٍ ٧Hakimnoneshi mwenye kukila, awapo amekonda, wala hakimuondolei njaa, awapo na njaa وُجُوهٌ يَوۡمَئِذٍ نَّاعِمَةٌ ٨Nyuso za Waumini, siku ya Kiyama, zitakuwa kwenye neema لِّسَعۡيِهَا رَاضِيَةٌ ٩Kwa kuwa zilijishughulisha ulimwenguni kumtii Mwenyezi Mungu na kuridhika na Akhera فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٍ ١٠Zitakuwa kwenye Pepo ya daraja ya juu لَّا تَسۡمَعُ فِيهَا لَٰغِيَةً ١١Hutasikia humo hata neno moja la upuuzi فِيهَا عَيۡنٌ جَارِيَةٌ ١٢Ndani yake kuna chemchemi yenye kuteremka maji yake فِيهَا سُرُرٌ مَّرۡفُوعَةٌ ١٣Ndani yake mna vitanda vilioangatika وَأَكۡوَابٌ مَّوۡضُوعَةٌ ١٤na vikombe vilivyotayarishwa kwa wenye kunywa وَنَمَارِقُ مَصۡفُوفَةٌ ١٥na mito iliyopangwa, mmoja baada ya mwingine وَزَرَابِيُّ مَبۡثُوثَةٌ ١٦na mazulia mengi yaliyotandikwa أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى ٱلۡإِبِلِ كَيۡفَ خُلِقَتۡ ١٧Kwani, hawa makafiri wenye kukanusha, hawaangalii ngamia namna walivyoumbwa kiajabu وَإِلَى ٱلسَّمَآءِ كَيۡفَ رُفِعَتۡ ١٨Na mbingu namna zlizoinuliwa juu kwa namna ya kupendeza وَإِلَى ٱلۡجِبَالِ كَيۡفَ نُصِبَتۡ ١٩Na milima namna iliyoimarishwa ukapatikana uthabiti na utulivu wa ardhi وَإِلَى ٱلۡأَرۡضِ كَيۡفَ سُطِحَتۡ ٢٠Na ardhi namna ilivyotandikwa na kutayarishwa فَذَكِّرۡ إِنَّمَآ أَنتَ مُذَكِّرٌ ٢١Basi wawaidhie, ewe Mtume, wale wenye kupa nyongo yale uliyotumilizwa kwayo wala usihuzunike kwa kupa mgongo kwao لَّسۡتَ عَلَيۡهِم بِمُصَيۡطِرٍ ٢٢Kwani wewe ni muwaidhiaji kwao, na si juu yako kuwalazimisha kuamini إِلَّا مَن تَوَلَّىٰ وَكَفَرَ ٢٣Lakini yule mwenye kuyapa mgongo makumbusho na mawaidha na akawa mkakamavu kwenye ukafiri wake فَيُعَذِّبُهُ ٱللَّهُ ٱلۡعَذَابَ ٱلۡأَكۡبَرَ ٢٤Mwenyezi Mungu Atamuadhibu adhabu kali Motoni إِنَّ إِلَيۡنَآ إِيَابَهُمۡ ٢٥Hakika wao watarudi kwetu baada ya kufa ثُمَّ إِنَّ عَلَيۡنَا حِسَابَهُم ٢٦Kisha ni juu yetu kuwalipa kwa waliyoyafanya

Translation: Abdullah Muhammad Abu Bakr.