بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
وَٱلَّيۡلِ إِذَا يَغۡشَىٰ ١Mwenyezi Mungu Anaapa kwa usiku unapoifinika ardhi na vilivyoko juu yake kwa giza lake وَٱلنَّهَارِ إِذَا تَجَلَّىٰ ٢Na kwa mchana unapofunuka mwangaza wake kutoka kwenye giza la usiku وَمَا خَلَقَ ٱلذَّكَرَ وَٱلۡأُنثَىٰٓ ٣Na kwa kuumba mbea mbili: ya kiume na ya kike إِنَّ سَعۡيَكُمۡ لَشَتَّىٰ ٤Kuwa vitendo vyenu vinatofautiana: kuna wenye kufanyia dunia na wenye kufanyia Akhera فَأَمَّا مَنۡ أَعۡطَىٰ وَٱتَّقَىٰ ٥Ama mwenye kutoa kwenye mali yake, akamcha Mwenyezi Mungu katika huko kutoa وَصَدَّقَ بِٱلۡحُسۡنَىٰ ٦akaamini «Lā Ilāha Illā Allāh» na yanayotakiwa na Imani hiyo na akaamini malipo yanayofungamana nayo فَسَنُيَسِّرُهُۥ لِلۡيُسۡرَىٰ ٧Tutamuongoza na kumuafikia njia za kheri na wema na kumsahilishia mambo yake وَأَمَّا مَنۢ بَخِلَ وَٱسۡتَغۡنَىٰ ٨Na ama mwenye kuyafanyia ubakhili mali yake, asiwe na haja ya malipo ya Mola wake وَكَذَّبَ بِٱلۡحُسۡنَىٰ ٩akakanusha neno la «Lā Ilāha Illā Allāh» na yanayotakiwa na neno hilo na akakanusha malipo yanayofungamana nalo فَسَنُيَسِّرُهُۥ لِلۡعُسۡرَىٰ ١٠Tutamnyoshea njia za mateso وَمَا يُغۡنِي عَنۡهُ مَالُهُۥٓ إِذَا تَرَدَّىٰٓ ١١Wala hayatamfaa yeye mali yake aliyoyafanyia ubakhili atakapotumbukia Motoni إِنَّ عَلَيۡنَا لَلۡهُدَىٰ ١٢Ni juu Yetu, kwa fadhila Zetu na busara Yetu, kueleza njia ya uongofu yenye kufikisha kwa Mwenyezi Mungu na ya upotevu وَإِنَّ لَنَا لَلۡأٓخِرَةَ وَٱلۡأُولَىٰ ١٣Na Sisi Tuna mamlaka ya maisha ya Akhera na maisha ya ulimwenguni فَأَنذَرۡتُكُمۡ نَارًا تَلَظَّىٰ ١٤Ndipo nikawaonya , enyi watu, na kuwatisha moto wenye kuwaka, nao ni moto wa Jahanamu لَا يَصۡلَىٰهَآ إِلَّا ٱلۡأَشۡقَى ١٥Hataingia Moto huo isipokuwa aliyekuwa mbaya sana. Mwenye kumkanusha Nabii Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie ٱلَّذِي كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ ١٦na akakataa kumwamini na kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake وَسَيُجَنَّبُهَا ٱلۡأَتۡقَى ١٧Na ataepushwa nao mchaji Mwenyezi Mungu sana ٱلَّذِي يُؤۡتِي مَالَهُۥ يَتَزَكَّىٰ ١٨Ambaye hutoa mali yake kwa kutaka nyongeza za kheri وَمَا لِأَحَدٍ عِندَهُۥ مِن نِّعۡمَةٍ تُجۡزَىٰٓ ١٩kutoa Kwake si kwa kulipa zema alizofanyiwa na mtu إِلَّا ٱبۡتِغَآءَ وَجۡهِ رَبِّهِ ٱلۡأَعۡلَىٰ ٢٠Lakini anatoa kwa kutaka uso wa Mola wake na radhi zake. Basi Mwenyezi Mungu atampa وَلَسَوۡفَ يَرۡضَىٰ ٢١huko Peponi, malipo ya kumridhisha