Millat al-Islam

Chapter 91 · 15 verses · Abdullah Muhammad Abu Bakr

Surah Ash-Shams in Swahili

Arabic with tafsir Listen to Surah Ash-Shams (1346 reciters)
Meccanسورة الشمس15 verses

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلشَّمۡسِ وَضُحَىٰهَا ١Mwenyezi Mungu Anaapa kwa jua na mchana wake na mwangaza wake wa asubuhi وَٱلۡقَمَرِ إِذَا تَلَىٰهَا ٢Na kwa mwezi unapolifuata wakati wa kucha na kutwa وَٱلنَّهَارِ إِذَا جَلَّىٰهَا ٣Na kwa mchana unapoliondoa giza na kulifunua وَٱلَّيۡلِ إِذَا يَغۡشَىٰهَا ٤Na kwa usiku unapoifinika ardhi ikawa giza وَٱلسَّمَآءِ وَمَا بَنَىٰهَا ٥Na kwa mbingu na kujengeka kwake kiimara وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا طَحَىٰهَا ٦Na kwa ardhi na kutandikika kwake وَنَفۡسٍ وَمَا سَوَّىٰهَا ٧Na kwa kila nafsi na namna Mwenyezi Mungu alivyoikamilisha umbo lake ili itekeleze kazi iliyoumbiwa nayo فَأَلۡهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقۡوَىٰهَا ٨Akaibainishia njia ya shari na njia ya kheri قَدۡ أَفۡلَحَ مَن زَكَّىٰهَا ٩Amefaulu mwenye kuisafisha na kuikuza kwa kheri وَقَدۡ خَابَ مَن دَسَّىٰهَا ١٠Na ameingia kwenye hasara mwenye kuitia nafsi yake kwenye maasia كَذَّبَتۡ ثَمُودُ بِطَغۡوَىٰهَآ ١١Kabila la Thamūd lilimkanusha Nabii wake kwa kuvama kwenye uasi إِذِ ٱنۢبَعَثَ أَشۡقَىٰهَا ١٢Pindi walipotoka wabaya zaidi wa kabila hilo kumchinja Ngamia. Mtume wa Mwenyezi Mungu’ Ṣāliḥ, amani imshukie فَقَالَ لَهُمۡ رَسُولُ ٱللَّهِ نَاقَةَ ٱللَّهِ وَسُقۡيَٰهَا ١٣akawaambia: «Tahadharini kumgusa kwa ubaya ngamia ambaye ni miujiza ilioletwa na Mwenyezi Mungu kwenu inayoonyesha ukweli wa Nabii wenu, na msizuie kinywaji chake. Yeye ana siku yake ya kunywa na nyinyi mna siku yenu maalumu ya kunywa.» Hilo likawa zito kwao فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمۡدَمَ عَلَيۡهِمۡ رَبُّهُم بِذَنۢبِهِمۡ فَسَوَّىٰهَا ١٤Wakamkanusha na kulipuza onyo lake wakamchinja.Mola wao Akawafinika kwa adhabu, akaisawazisha juu yao na hakuna aliyeweza kuponyoka وَلَا يَخَافُ عُقۡبَٰهَا ١٥Wala Haogopi, Mwenye uwezo uliotukuka, athari ya adhabu kali Aliywateremshia

Translation: Abdullah Muhammad Abu Bakr.