تَبَّتۡ يَدَآ أَبِي لَهَبٍ وَتَبَّ ١Imehasirika mikono miwili ya Abu Lahab, na yeye mwenyewe ameangamia, kwa kumuudhi Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. Hasara ya Abu Lahab ilithubutuمَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُ مَالُهُۥ وَمَا كَسَبَ ٢Hayakumfalia kitu mali yake na watoto wake. Kwani hivyo havitamkinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu pindi ikimshukiaسَيَصۡلَىٰ نَارًا ذَاتَ لَهَبٍ ٣Ataingia kwenye Moto wenye kuroromaوَٱمۡرَأَتُهُۥ حَمَّالَةَ ٱلۡحَطَبِ ٤yeye na mke wake ambaye alikuwa akibeba miba na kuiweka kwenye njia anayopita Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ili kumuudhiفِي جِيدِهَا حَبۡلٌ مِّن مَّسَدِۭ٥Kwenye shingo yake patakuwa na kamba imara ya lifu gumu lilio kavu; atabebewa nayo kwenye Moto wa Jahanamu, kisha atarushwa nayo mpaka chini