Millat al-Islam

Chapter 56 · 96 verses · Abdullah Muhammad Abu Bakr

Surah Al-Waqi'a in Swahili

Arabic with tafsir Listen to Surah Al-Waqi'a (1348 reciters)

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

إِذَا وَقَعَتِ ٱلۡوَاقِعَةُ ١Kitakaposimama Kiyama لَيۡسَ لِوَقۡعَتِهَا كَاذِبَةٌ ٢Hakutakuwa na yoyote mwenye kukanusha kusimama kwake خَافِضَةٌ رَّافِعَةٌ ٣Ni chenye kuwainamisha chini maadui wa Mwenyezi Mungu ndani ya Moto na ni chenye kuwainua juu Peponi wale wenye kumtegemea إِذَا رُجَّتِ ٱلۡأَرۡضُ رَجًّا ٤Itakapotikiswa ardhi mtikiso wa nguvu وَبُسَّتِ ٱلۡجِبَالُ بَسًّا ٥Na yakamumunyuliwa majabali mmumunyuo wa kina فَكَانَتۡ هَبَآءً مُّنۢبَثًّا ٦Yakawa vumbi lenye kuruka angani lililosukumwa na upepo وَكُنتُمۡ أَزۡوَٰجًا ثَلَٰثَةً ٧Na mkawa, enyi viumbe, makundi matatu فَأَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ ٨Kundi la watu wa upande wa kulia, wenye daraja kubwa. Ni kikubwa kilioje cheo chao وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ ٩Kuna na kundi la watu wa upande wa kushoto, wenye daraja duni. Ni mbaya iliyoje hali yao وَٱلسَّٰبِقُونَ ٱلسَّٰبِقُونَ ١٠Na wale waliotangulia mbele kwenye kheri duniani ndio wenye kutangulia mbele kwenye daraja za juu huko Akhera أُوْلَٰٓئِكَ ٱلۡمُقَرَّبُونَ ١١Wao ndio walioletwa karibu kwa Mwenyezi Mungu فِي جَنَّٰتِ ٱلنَّعِيمِ ١٢Mola wao Atawatia kwenye mabustani ya Pepo ya starehe ثُلَّةٌ مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ ١٣Watayaingia watu wengi watu wa mwanzo wa ummah huu, na ummah wengineo wasiokuwa wao وَقَلِيلٌ مِّنَ ٱلۡأٓخِرِينَ ١٤na wachache miongoni mwa watu mwisho wa ummah huu عَلَىٰ سُرُرٍ مَّوۡضُونَةٍ ١٥wakiwa juu ya vitanda vilivyofumwa kwa dhahabu مُّتَّكِـِٔينَ عَلَيۡهَا مُتَقَٰبِلِينَ ١٦na wakiwa katika hali ya kuvitegemea na huku wanaelekeana na kukutana يَطُوفُ عَلَيۡهِمۡ وِلۡدَٰنٌ مُّخَلَّدُونَ ١٧Wanawazunguka wao kuwatumikia watumishi vijana wasiozeeka wala kufa بِأَكۡوَابٍ وَأَبَارِيقَ وَكَأۡسٍ مِّن مَّعِينٍ ١٨wakiwa na vikombe, mabirika na gilasi kutoka kwenye chemchemi ya pombe yenye kupita ndani ya Pepo لَّا يُصَدَّعُونَ عَنۡهَا وَلَا يُنزِفُونَ ١٩na hawaumwi na vichwa kutokana nayo wala hawarukwi na akili وَفَٰكِهَةٍ مِّمَّا يَتَخَيَّرُونَ ٢٠Na watawazunguka wao watumishi vijana na kila kitu wanachokichagua miongoni mwa matunda وَلَحۡمِ طَيۡرٍ مِّمَّا يَشۡتَهُونَ ٢١nyama ya ndege ambayo nafsi zao inavutika nayo وَحُورٌ عِينٌ ٢٢Na watakuwa na wanawake wenye macho makubwa kama kwamba wao كَأَمۡثَٰلِ ٱللُّؤۡلُوِٕ ٱلۡمَكۡنُونِ ٢٣kwa usafi wao na uzuri wao, ni lulu iliyohifadhiwa ndani ya mashaza yake جَزَآءَۢ بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ ٢٤hali hayo yakiwa ni malipo yao kwa yale waliokuwa wakiyafanya duniani لَا يَسۡمَعُونَ فِيهَا لَغۡوًا وَلَا تَأۡثِيمًا ٢٥Hawatasikia humo Peponi ubatilifu wala yale ya kuwatia madhambini kuyasikia إِلَّا قِيلًا سَلَٰمًا سَلَٰمًا ٢٦isipokuwa maneno yasiyokuwa na kasoro hizi na kusalimiana wao kwa wao وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡيَمِينِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡيَمِينِ ٢٧Na watu wa upande wa kulia فِي سِدۡرٍ مَّخۡضُودٍ ٢٨ni kikubwa kilioje cheo chao na malipo yao وَطَلۡحٍ مَّنضُودٍ ٢٩Watakuwa kwenye mikunazi isiyo na miba, na ndizi zilizopandana na kupangika وَظِلٍّ مَّمۡدُودٍ ٣٠kila ndizi juu ya nyingine, na vivuli vya daima visivyoondoka وَمَآءٍ مَّسۡكُوبٍ ٣١na maji yanayotembea yasiyokatika وَفَٰكِهَةٍ كَثِيرَةٍ ٣٢na matunda mengi لَّا مَقۡطُوعَةٍ وَلَا مَمۡنُوعَةٍ ٣٣yasiyomalizika wala kuwaishia wala hakuna kizuizi chochote kinachowazuia wao kuyafikia وَفُرُشٍ مَّرۡفُوعَةٍ ٣٤na matandiko yaliyoinuliwa juu ya vitanda إِنَّآ أَنشَأۡنَٰهُنَّ إِنشَآءً ٣٥Sisi tumewaumba wanawake wa watu wa Peponi umbile ambalo silo lile umbile lililokuwa duniani, umbile lililokamilika lisilokubali kutoweka فَجَعَلۡنَٰهُنَّ أَبۡكَارًا ٣٦na tumewafanya ni wanawali wenye kujipendekeza kwa waume zao عُرُبًا أَتۡرَابًا ٣٧hali ya kuwa ni marika na wao kimiaka لِّأَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ ٣٨Tumewaumbia wanawake hao watu wa upande wa kulia ثُلَّةٌ مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ ٣٩Nao ni kundi la watu wengi wa mwanzo وَثُلَّةٌ مِّنَ ٱلۡأٓخِرِينَ ٤٠na kundi la watu wengi wa mwisho وَأَصۡحَٰبُ ٱلشِّمَالِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلشِّمَالِ ٤١Na watu wa upande wa kushoto, ni mbaya iliyoje hali yao na malipo yao فِي سَمُومٍ وَحَمِيمٍ ٤٢Watakuwa kwenye upepo ulio moto utokanao na joto la Moto wa Jahanamu utakaozuia pumzi zao, na maji moto yanayochemka وَظِلٍّ مِّن يَحۡمُومٍ ٤٣na kivuli cha moshi mweusi sana لَّا بَارِدٍ وَلَا كَرِيمٍ ٤٤usio na mashukio baridi wala mandhari mazuri إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَبۡلَ ذَٰلِكَ مُتۡرَفِينَ ٤٥Kwani wao walikuwa duniani wakijistarehesha kwa vitu vya haramu wakijiepusha na yale ambayo Mitume walikuja nayo وَكَانُواْ يُصِرُّونَ عَلَى ٱلۡحِنثِ ٱلۡعَظِيمِ ٤٦Na walikuwa wamesimama wima katika kumkanusha Mwenyezi Mungu na kumshirikisha na kumuasi, na hawakuwa na nia ya kutubia kwa hayo وَكَانُواْ يَقُولُونَ أَئِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَٰمًا أَءِنَّا لَمَبۡعُوثُونَ ٤٧Na walikuwa wakisema hali ya kukanusha Ufufuzi, «Je hivi sisi tutafufuliwa tutakapokufa na tukawa mchanga na mifupa iliyochakaa?» Maneno yao hayo yanaonesha kuwa wao walikuwa wakiliona jambo hili la kufufuliwa kuwa liko mbali na ukweli na wakilikanusha أَوَءَابَآؤُنَا ٱلۡأَوَّلُونَ ٤٨«Je tutafufuliwa sisi na hali baba zetu waliotangulia wamekuwa mchanga uliotapakaa kwenye ardhi?» قُلۡ إِنَّ ٱلۡأَوَّلِينَ وَٱلۡأٓخِرِينَ ٤٩Sema uwaambie, «Hakika wa mwanzo na wa mwisho miongoni mwa binadamu لَمَجۡمُوعُونَ إِلَىٰ مِيقَٰتِ يَوۡمٍ مَّعۡلُومٍ ٥٠watakusanywa katika Siku iliyowekewa wakati maalumu, nayo ni Siku ya Kiyama ثُمَّ إِنَّكُمۡ أَيُّهَا ٱلضَّآلُّونَ ٱلۡمُكَذِّبُونَ ٥١«Kisha nyinyi, enyi mliopotea njia ya uongofu mnaokanusha onyo la Mwenyezi Mungu na agizo Lake لَأٓكِلُونَ مِن شَجَرٍ مِّن زَقُّومٍ ٥٢ni wenye kula kutokana na mti wa zaqqūm فَمَالِـُٔونَ مِنۡهَا ٱلۡبُطُونَ ٥٣nao ni katika miti mibaya zaidi, na ni wenye kujaza matumbo yenu kutokana nao kwa sababu ya ukali wa njaa فَشَٰرِبُونَ عَلَيۡهِ مِنَ ٱلۡحَمِيمِ ٥٤na ni wenye kunywa juu yake maji yaliyo moto hadi ya mwisho, yasiyomaliza kiu فَشَٰرِبُونَ شُرۡبَ ٱلۡهِيمِ ٥٥Mtayanywa maji hayo kwa wingi kama vile ngamia wenye kiu wasioshiba maji kwa ugonjwa uliowapata.» هَٰذَا نُزُلُهُمۡ يَوۡمَ ٱلدِّينِ ٥٦Adhabu hii watakayoipata ndiyo zawadi Aliyowaandalia Siku ya Kiyama. Katika haya kuna kuwalaumu na kuwacheza shere نَحۡنُ خَلَقۡنَٰكُمۡ فَلَوۡلَا تُصَدِّقُونَ ٥٧Sisi tumewaumba, enyi watu, na hamkuwa kitu chochote. Basi si msadiki kuwa kuna kufufuliwa أَفَرَءَيۡتُم مَّا تُمۡنُونَ ٥٨Mnayaonaje maji ya manii mnayoyatupa ndani ya vizazi vya wake zenu ءَأَنتُمۡ تَخۡلُقُونَهُۥٓ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡخَٰلِقُونَ ٥٩je nyinyi ndio mnaomuumba mwanadamu kutokana na hayo au ni sisi ndio wenye kuumba نَحۡنُ قَدَّرۡنَا بَيۡنَكُمُ ٱلۡمَوۡتَ وَمَا نَحۡنُ بِمَسۡبُوقِينَ ٦٠Sisi tumekadiria kifo kwenu عَلَىٰٓ أَن نُّبَدِّلَ أَمۡثَٰلَكُمۡ وَنُنشِئَكُمۡ فِي مَا لَا تَعۡلَمُونَ ٦١na sisi si wenye kushindwa kubadilisha umbo lenu Siku ya Kiyama na kuwaumba kwa sifa na namna msizozijua وَلَقَدۡ عَلِمۡتُمُ ٱلنَّشۡأَةَ ٱلۡأُولَىٰ فَلَوۡلَا تَذَكَّرُونَ ٦٢Na hakika mlijua kuwa Mwenyezi Mungu Aliwaumba uumbaji wa kwanza na hamkuwa kitu chochote. Basi si mkumbuke uweza wa Mwenyezi Mungu wa kuwaumba mara nyingine أَفَرَءَيۡتُم مَّا تَحۡرُثُونَ ٦٣Mnazionaje mbegu mnazozipanda ءَأَنتُمۡ تَزۡرَعُونَهُۥٓ أَمۡ نَحۡنُ ٱلزَّٰرِعُونَ ٦٤Je ni nyinyi mnaoziotesha kutoka ardhini? Sisi ndio tuaozituliza na kuziotesha ardhini لَوۡ نَشَآءُ لَجَعَلۡنَٰهُ حُطَٰمًا فَظَلۡتُمۡ تَفَكَّهُونَ ٦٥Lau tungalitaka tungaliifanya mimea inayotokana na mbegu hizo kuwa mapepe, haimkiniki kunufaika nayo kwa kula إِنَّا لَمُغۡرَمُونَ ٦٦mkawa mnaona ajabu kwa kilichoshukia mimea yenu na mnasema, «Sisi tumepata hasara na ni wenye kuungulika بَلۡ نَحۡنُ مَحۡرُومُونَ ٦٧Bali sisi tumekoseshwa riziki.» أَفَرَءَيۡتُمُ ٱلۡمَآءَ ٱلَّذِي تَشۡرَبُونَ ٦٨Mnayaonaje maji mnayokunywa ili mhuike kwayo ءَأَنتُمۡ أَنزَلۡتُمُوهُ مِنَ ٱلۡمُزۡنِ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡمُنزِلُونَ ٦٩Je ni nyinyi mliyoyateremsha kutoka kwenye mawingu hadi kwenye kituo cha ardhi au ni sisi tuliyoyateremsha ili kuwarehemu nyinyi لَوۡ نَشَآءُ جَعَلۡنَٰهُ أُجَاجًا فَلَوۡلَا تَشۡكُرُونَ ٧٠Lau tungalitaka tungaliyafanya maji haya yawe na chumvi sana, ikiwa haiwezekani kunufaika nayo kwa kunywa wala kwa mimea. Basi si mumshukuru Mola wenu kwa kuteremsha maji tamu kwa kuwanufaisha nyinyi أَفَرَءَيۡتُمُ ٱلنَّارَ ٱلَّتِي تُورُونَ ٧١Mnaouonaje moto mnaouwasha ءَأَنتُمۡ أَنشَأۡتُمۡ شَجَرَتَهَآ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡمُنشِـُٔونَ ٧٢Je ni nyinyi mlioufanya mti wake, unaozalisha moto kwa kukwaruzwa, upatikane au ni sisi tulioufanya upatikane نَحۡنُ جَعَلۡنَٰهَا تَذۡكِرَةً وَمَتَٰعًا لِّلۡمُقۡوِينَ ٧٣Sisi tumeufanya moto wenu mnaouwasha ni ukumbusho kwenu wa Moto wa Jahanamu na pia ni manufaa kwa wasafiri فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ ٧٤Basi mtakase Mola wako, ewe Nabii, Aliye mtukufu Mwenye ukamilifu wa majina na sifa, Mwingi wa wema na kheri ۞ فَلَآ أُقۡسِمُ بِمَوَٰقِعِ ٱلنُّجُومِ ٧٥Mwenyezi Mungu Anaapa kwa mapomoko ya nyota nyakati za kuzama kwake mbinguni وَإِنَّهُۥ لَقَسَمٌ لَّوۡ تَعۡلَمُونَ عَظِيمٌ ٧٦Nacho ni kiapo kikubwa lau mnajua kadiri yake إِنَّهُۥ لَقُرۡءَانٌ كَرِيمٌ ٧٧Hakika hii Qur’ani iliyoteremshiwa Muhammad ni Qur’ani yenye manufaa makubwa, yenye kheri nyingi na yenye elimu tele فِي كِتَٰبٍ مَّكۡنُونٍ ٧٨iliyo ndani ya Kitabu kilichohifadhiwa, kilichofichwa na macho ya viumbe, nacho ni Kitabu ambacho kiko mikononi mwa Malaika لَّا يَمَسُّهُۥٓ إِلَّا ٱلۡمُطَهَّرُونَ ٧٩Hawaigusi Qur’ani isipokuwa malaika watukufu ambao Mwenyezi Mungu Amewasafisha na aibu na madhambi. Na pia hawaigusi isipokuwa watu waliojitohirisha na ushirikina na janaba na ukosefu wa udhu تَنزِيلٌ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ٨٠Na hii Qur’ani tukufu imeteremshwa kutoka kwa Mola wa viumbe vyote, kwani hiyo ndiyo haki isiyo na shaka ndani yake أَفَبِهَٰذَا ٱلۡحَدِيثِ أَنتُم مُّدۡهِنُونَ ٨١je hii Qur’ani, enyi washirikina, mnaikanusha وَتَجۡعَلُونَ رِزۡقَكُمۡ أَنَّكُمۡ تُكَذِّبُونَ ٨٢Na je mnaifanya shukrani yenu kwa neema za Mola wenu ni kuwa nyinyi mnazikanusha na kukufuru? Hapa pana makaripio kwa anayedharau amri za Qur’ani na kutojali mwito wake فَلَوۡلَآ إِذَا بَلَغَتِ ٱلۡحُلۡقُومَ ٨٣Basi je mnaweza pindi roho ya mmoja wenu inapofika kwenye koo katika uchungu wa kifo وَأَنتُمۡ حِينَئِذٍ تَنظُرُونَ ٨٤na hali nyinyi mmehudhuria mnamtazama, kuizuia roho yake ndani ya mwili wake? Hamtaweza hilo وَنَحۡنُ أَقۡرَبُ إِلَيۡهِ مِنكُمۡ وَلَٰكِن لَّا تُبۡصِرُونَ ٨٥Na sisi tuko karibu na yeye zaidi, kupitia Malaika wetu, kuliko nyinyi, lakini nyinyi hamuwaoni فَلَوۡلَآ إِن كُنتُمۡ غَيۡرَ مَدِينِينَ ٨٦Na je mnaweza, iwapo nyinyi si wenye kuhesabiwa wala kulipwa kwa matendo yenu تَرۡجِعُونَهَآ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ ٨٧kuirudisha roho kwenye mwili, iwapo nyinyi ni wakweli? Hamtaweza kuirudisha فَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡمُقَرَّبِينَ ٨٨Basi iwapo yule anayekufa ni kati ya watu wa upande wa kulia, atapata rehema kunjufu na furaha فَرَوۡحٌ وَرَيۡحَانٌ وَجَنَّتُ نَعِيمٍ ٨٩wakati wa kufa kwake, na kila kinachoifurahisha nafsi yake, Na atapata Pepo ya starehe huko Akhera وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ ٩٠Na iwapo yule anayekufa ni kati ya watu wa upande wa kulia فَسَلَٰمٌ لَّكَ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ ٩١ataambiwa, «Umesalimika na kuwa kwenye amani, kwa kuwa wewe ni miongoni mwa watu wa upande wa kulia.» وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡمُكَذِّبِينَ ٱلضَّآلِّينَ ٩٢Na iwapo yule anayekufa ni miongoni mwa wenye kukanusha kufufuliwa, waliopotoka na njia ya uongofu فَنُزُلٌ مِّنۡ حَمِيمٍ ٩٣basi atapata makaribisho ya kinywaji cha moto wa Jahanamu kilichochemshwa, kilicho na joto hadi ya mwisho وَتَصۡلِيَةُ جَحِيمٍ ٩٤na atachomwa na Moto na aungulike na adhabu yake kali إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ حَقُّ ٱلۡيَقِينِ ٩٥Hakika habari hii tumezokuelezea, ewe Mtume, ni ukweli wa yakini usio na shaka فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ ٩٦Basi litakase jina la Mola wako Aliyetukuka na umtakase na yale ambayo madhalimu na wenye kukanusha wanayasema. Mwenyezi Mungu Yuko juu ya yale wanayoyasema ujuu mkubwa sana

Translation: Abdullah Muhammad Abu Bakr.