Millat al-Islam

Chapter 56 · 96 verses · Ali Muhsin Al Barwani

Surah Al-Waqi'a in Swahili

Arabic with tafsir Listen to Surah Al-Waqi'a (1348 reciters)

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

إِذَا وَقَعَتِ ٱلۡوَاقِعَةُ ١Litakapo tukia hilo Tukio لَيۡسَ لِوَقۡعَتِهَا كَاذِبَةٌ ٢Hapana cha kukanusha kutukia kwake خَافِضَةٌ رَّافِعَةٌ ٣Literemshalo linyanyualo إِذَا رُجَّتِ ٱلۡأَرۡضُ رَجًّا ٤Itakapo tikiswa ardhi kwa mtikiso وَبُسَّتِ ٱلۡجِبَالُ بَسًّا ٥Na milima itapo sagwasagwa فَكَانَتۡ هَبَآءً مُّنۢبَثًّا ٦Iwe mavumbi yanayo peperushwa وَكُنتُمۡ أَزۡوَٰجًا ثَلَٰثَةً ٧Na nyinyi mtakuwa namna tatu فَأَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ ٨Basi watakuwepo wa kuliani; je, ni wepi wa kuliani وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ ٩Na wa kushotoni; je, ni wepi wa kushotoni وَٱلسَّٰبِقُونَ ٱلسَّٰبِقُونَ ١٠Na wa mbele watakuwa mbele أُوْلَٰٓئِكَ ٱلۡمُقَرَّبُونَ ١١Hao ndio watakao karibishwa فِي جَنَّٰتِ ٱلنَّعِيمِ ١٢Katika Bustani zenye neema ثُلَّةٌ مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ ١٣Fungu kubwa katika wa mwanzo وَقَلِيلٌ مِّنَ ٱلۡأٓخِرِينَ ١٤Na wachache katika wa mwisho عَلَىٰ سُرُرٍ مَّوۡضُونَةٍ ١٥Watakuwa juu ya viti vya fakhari vilivyo tonewa مُّتَّكِـِٔينَ عَلَيۡهَا مُتَقَٰبِلِينَ ١٦Wakiviegemea wakielekeana يَطُوفُ عَلَيۡهِمۡ وِلۡدَٰنٌ مُّخَلَّدُونَ ١٧Wakitumikiwa na wavulana wa ujana wa milele بِأَكۡوَابٍ وَأَبَارِيقَ وَكَأۡسٍ مِّن مَّعِينٍ ١٨Kwa vikombe na mabirika na bilauri za vinywaji kutoka chemchem safi لَّا يُصَدَّعُونَ عَنۡهَا وَلَا يُنزِفُونَ ١٩Hawataumwa kichwa kwa vinywaji hivyo wala hawatoleweshwa وَفَٰكِهَةٍ مِّمَّا يَتَخَيَّرُونَ ٢٠Na matunda wayapendayo وَلَحۡمِ طَيۡرٍ مِّمَّا يَشۡتَهُونَ ٢١Na nyama za ndege kama wanavyo tamani وَحُورٌ عِينٌ ٢٢Na Mahurulaini كَأَمۡثَٰلِ ٱللُّؤۡلُوِٕ ٱلۡمَكۡنُونِ ٢٣Walio kama mfano wa lulu zilio hifadhiwa جَزَآءَۢ بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ ٢٤Ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyatenda لَا يَسۡمَعُونَ فِيهَا لَغۡوًا وَلَا تَأۡثِيمًا ٢٥Humo hawatasikia porojo wala maneno ya dhambi إِلَّا قِيلًا سَلَٰمًا سَلَٰمًا ٢٦Isipo kuwa maneno ya Salama, Salama وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡيَمِينِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡيَمِينِ ٢٧Na wale wa mkono wa kulia, ni yepi yatakuwa ya wa kuliani فِي سِدۡرٍ مَّخۡضُودٍ ٢٨Katika mikunazi isiyo na miba وَطَلۡحٍ مَّنضُودٍ ٢٩Na migomba iliyo pangiliwa وَظِلٍّ مَّمۡدُودٍ ٣٠Na kivuli kilicho tanda وَمَآءٍ مَّسۡكُوبٍ ٣١Na maji yanayo miminika وَفَٰكِهَةٍ كَثِيرَةٍ ٣٢Na matunda mengi لَّا مَقۡطُوعَةٍ وَلَا مَمۡنُوعَةٍ ٣٣Hayatindikii wala hayakatazwi وَفُرُشٍ مَّرۡفُوعَةٍ ٣٤Na matandiko yaliyo nyanyuliwa إِنَّآ أَنشَأۡنَٰهُنَّ إِنشَآءً ٣٥Hakika Sisi tutawaumba (Mahurulaini) upya فَجَعَلۡنَٰهُنَّ أَبۡكَارًا ٣٦Na tutawafanya vijana عُرُبًا أَتۡرَابًا ٣٧Wanapendana na waume zao, hirimu moja لِّأَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ ٣٨Kwa ajili ya watu wa kuliani ثُلَّةٌ مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ ٣٩Fungu kubwa katika wa mwanzo وَثُلَّةٌ مِّنَ ٱلۡأٓخِرِينَ ٤٠Na fungu kubwa katika wa mwisho وَأَصۡحَٰبُ ٱلشِّمَالِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلشِّمَالِ ٤١Na watu wa kushotoni; je ni yepi ya wa kushotoni فِي سَمُومٍ وَحَمِيمٍ ٤٢Katika upepo wa moto, na maji yanayo chemka وَظِلٍّ مِّن يَحۡمُومٍ ٤٣Na kivuli cha moshi mweusi لَّا بَارِدٍ وَلَا كَرِيمٍ ٤٤Si cha kuburudisha wala kustarehesha إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَبۡلَ ذَٰلِكَ مُتۡرَفِينَ ٤٥Hakika hao walikuwa kabla ya haya wakiishi maisha ya anasa وَكَانُواْ يُصِرُّونَ عَلَى ٱلۡحِنثِ ٱلۡعَظِيمِ ٤٦Na walikuwa wakishikilia kufanya madhambi makubwa وَكَانُواْ يَقُولُونَ أَئِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَٰمًا أَءِنَّا لَمَبۡعُوثُونَ ٤٧Na walikuwa wakisema: Tutakapo kufa na tukawa udongo na mafupa, ati ndio tutafufuliwa أَوَءَابَآؤُنَا ٱلۡأَوَّلُونَ ٤٨Au baba zetu wa zamani قُلۡ إِنَّ ٱلۡأَوَّلِينَ وَٱلۡأٓخِرِينَ ٤٩Sema: Hakika wa zamani na wa mwisho لَمَجۡمُوعُونَ إِلَىٰ مِيقَٰتِ يَوۡمٍ مَّعۡلُومٍ ٥٠Bila ya shaka watakusanywa kwa wakati wa siku maalumu ثُمَّ إِنَّكُمۡ أَيُّهَا ٱلضَّآلُّونَ ٱلۡمُكَذِّبُونَ ٥١Kisha nyinyi, mlio potea, mnao kanusha لَأٓكِلُونَ مِن شَجَرٍ مِّن زَقُّومٍ ٥٢Kwa yakini mtakula mti wa Zaqqumu فَمَالِـُٔونَ مِنۡهَا ٱلۡبُطُونَ ٥٣Na kwa mti huo mtajaza matumbo فَشَٰرِبُونَ عَلَيۡهِ مِنَ ٱلۡحَمِيمِ ٥٤Na juu yake mtakunywa maji yanayo chemka فَشَٰرِبُونَ شُرۡبَ ٱلۡهِيمِ ٥٥Tena mtakunywa kama wanavyo kunywa ngamia wenye kiu هَٰذَا نُزُلُهُمۡ يَوۡمَ ٱلدِّينِ ٥٦Hiyo ndiyo karamu yao Siku ya Malipo نَحۡنُ خَلَقۡنَٰكُمۡ فَلَوۡلَا تُصَدِّقُونَ ٥٧Sisi tumekuumbeni; basi hamsadiki أَفَرَءَيۡتُم مَّا تُمۡنُونَ ٥٨Je! Mnaiona mbegu ya uzazi mnayo idondokeza ءَأَنتُمۡ تَخۡلُقُونَهُۥٓ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡخَٰلِقُونَ ٥٩Je! Mnaiumba nyinyi, au ni Sisi ndio Waumbaji نَحۡنُ قَدَّرۡنَا بَيۡنَكُمُ ٱلۡمَوۡتَ وَمَا نَحۡنُ بِمَسۡبُوقِينَ ٦٠Sisi tumekuwekeeni mauti; na wala Sisi hatushindwi عَلَىٰٓ أَن نُّبَدِّلَ أَمۡثَٰلَكُمۡ وَنُنشِئَكُمۡ فِي مَا لَا تَعۡلَمُونَ ٦١Kuwaleta wengine badala yenu na kukuumbeni nyinyi kwa umbo msilo lijua وَلَقَدۡ عَلِمۡتُمُ ٱلنَّشۡأَةَ ٱلۡأُولَىٰ فَلَوۡلَا تَذَكَّرُونَ ٦٢Na bila ya shaka mlikwisha jua umbo la kwanza, basi kwa nini hamkumbuki أَفَرَءَيۡتُم مَّا تَحۡرُثُونَ ٦٣Je! Mnaona makulima mnayo yapanda ءَأَنتُمۡ تَزۡرَعُونَهُۥٓ أَمۡ نَحۡنُ ٱلزَّٰرِعُونَ ٦٤Je! Ni nyinyi mnayo yaotesha au ni Sisi ndio wenye kuotesha لَوۡ نَشَآءُ لَجَعَلۡنَٰهُ حُطَٰمًا فَظَلۡتُمۡ تَفَكَّهُونَ ٦٥Tungeli taka tungeli yafanya yakawa mapepe, mkabaki mnastaajabu إِنَّا لَمُغۡرَمُونَ ٦٦Mkisema: Hakika sisi tumegharimika بَلۡ نَحۡنُ مَحۡرُومُونَ ٦٧Bali sisi tumenyimwa أَفَرَءَيۡتُمُ ٱلۡمَآءَ ٱلَّذِي تَشۡرَبُونَ ٦٨Je! Mnayaona maji mnayo yanywa ءَأَنتُمۡ أَنزَلۡتُمُوهُ مِنَ ٱلۡمُزۡنِ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡمُنزِلُونَ ٦٩Je! Ni nyinyi mnayo yateremsha kutoka mawinguni au ni Sisi ndio wenye kuyateremsha لَوۡ نَشَآءُ جَعَلۡنَٰهُ أُجَاجًا فَلَوۡلَا تَشۡكُرُونَ ٧٠Tungeli penda tungeli yafanya ya chumvi. Basi mbona hamshukuru أَفَرَءَيۡتُمُ ٱلنَّارَ ٱلَّتِي تُورُونَ ٧١Je! Mnauona moto mnao uwasha ءَأَنتُمۡ أَنشَأۡتُمۡ شَجَرَتَهَآ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡمُنشِـُٔونَ ٧٢Ni nyinyi mlio uumba mti wake au Sisi ndio Waumbaji نَحۡنُ جَعَلۡنَٰهَا تَذۡكِرَةً وَمَتَٰعًا لِّلۡمُقۡوِينَ ٧٣Sisi tumeufanya uwe ni ukumbusho na manufaa kwa walioko nyikani فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ ٧٤Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkuu ۞ فَلَآ أُقۡسِمُ بِمَوَٰقِعِ ٱلنُّجُومِ ٧٥Basi naapa kwa maanguko ya nyota وَإِنَّهُۥ لَقَسَمٌ لَّوۡ تَعۡلَمُونَ عَظِيمٌ ٧٦Na hakika bila ya shaka hichi ni kiapo kikubwa, laiti mngeli jua إِنَّهُۥ لَقُرۡءَانٌ كَرِيمٌ ٧٧Hakika hii bila ya shaka ni Qur'ani Tukufu فِي كِتَٰبٍ مَّكۡنُونٍ ٧٨Katika Kitabu kilicho hifadhiwa لَّا يَمَسُّهُۥٓ إِلَّا ٱلۡمُطَهَّرُونَ ٧٩Hapana akigusaye ila walio takaswa تَنزِيلٌ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ٨٠Ni uteremsho unao toka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote أَفَبِهَٰذَا ٱلۡحَدِيثِ أَنتُم مُّدۡهِنُونَ ٨١Ni maneno haya ndiyo nyinyi mnayapuuza وَتَجۡعَلُونَ رِزۡقَكُمۡ أَنَّكُمۡ تُكَذِّبُونَ ٨٢Na badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha فَلَوۡلَآ إِذَا بَلَغَتِ ٱلۡحُلۡقُومَ ٨٣Yawaje basi itakapo fika roho kwenye koo وَأَنتُمۡ حِينَئِذٍ تَنظُرُونَ ٨٤Na nyinyi wakati huo mnatazama وَنَحۡنُ أَقۡرَبُ إِلَيۡهِ مِنكُمۡ وَلَٰكِن لَّا تُبۡصِرُونَ ٨٥Na Sisi tuko karibu zaidi naye kuliko nyinyi فَلَوۡلَآ إِن كُنتُمۡ غَيۡرَ مَدِينِينَ ٨٦Na lau kuwa nyinyi hamumo katika mamlaka yangu تَرۡجِعُونَهَآ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ ٨٧Kwanini hamuirudishi hiyo roho, ikiwa nyinyi mnasema kweli فَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡمُقَرَّبِينَ ٨٨Basi akiwa miongoni mwa walio karibishwa فَرَوۡحٌ وَرَيۡحَانٌ وَجَنَّتُ نَعِيمٍ ٨٩Basi ni raha, na manukato, na Bustani zenye neema وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ ٩٠Na akiwa katika watu wa upande wa kulia فَسَلَٰمٌ لَّكَ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ ٩١Basi ni Salamu kwako uliye miongoni mwa watu wa upande wa kulia وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡمُكَذِّبِينَ ٱلضَّآلِّينَ ٩٢Na ama akiwa katika walio kadhibisha wapotovu فَنُزُلٌ مِّنۡ حَمِيمٍ ٩٣Basi karamu yake ni maji yanayo chemka وَتَصۡلِيَةُ جَحِيمٍ ٩٤Na kutiwa Motoni إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ حَقُّ ٱلۡيَقِينِ ٩٥Hakika hii ndiyo haki yenye yakini فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ ٩٦Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkubwa

Translation: Ali Muhsin Al Barwani.