بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
أَلۡهَىٰكُمُ ٱلتَّكَاثُرُ ١Kumewashughulisha kujifahiri kwa mali na watoto mkawacha kumtii Mwenyezi Mungu حَتَّىٰ زُرۡتُمُ ٱلۡمَقَابِرَ ٢Kujishughulisha kwenu na hilo kumeendelea mpaka mkawa makaburini na mkazikwa humo كـَلَّا سَوۡفَ تَعۡلَمُونَ ٣Siyo namna hii inatakiwa iwapumbaze kushindana kwa wingi wa mali. Itawadhihirikia kuwa Nyumba ya Akhera ni bora kwenu ثُمَّ كـَلَّا سَوۡفَ تَعۡلَمُونَ ٤Kisha tahadharini mtajua mwisho mbaya wa kutojishughulisha na Akhera كـَلَّا لَوۡ تَعۡلَمُونَ عِلۡمَ ٱلۡيَقِينِ ٥Siyo namna hii inatakiwa iwashughulishe kushindana kwa wingi wa mali.Lau mnajua kikweli, mngalirudi nyuma na mngaliangusiliza kuokoa nafsi zenu kutoka kwenye maangamivu لَتَرَوُنَّ ٱلۡجَحِيمَ ٦Mtauona Moto ثُمَّ لَتَرَوُنَّهَا عَيۡنَ ٱلۡيَقِينِ ٧Kisha mtauona bila shaka ثُمَّ لَتُسۡـَٔلُنَّ يَوۡمَئِذٍ عَنِ ٱلنَّعِيمِ ٨Kisha mtaulizwa kuhusu kila aina ya starehe mliyokuwa nayo