Millat al-Islam

Chapter 101 · 11 verses · Abdullah Muhammad Abu Bakr

Surah Al-Qaria in Swahili

Arabic with tafsir Listen to Surah Al-Qaria (1290 reciters)

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

ٱلۡقَارِعَةُ ١Kiyama chenye kugonga nyoyo za watu kwa vituko vyake مَا ٱلۡقَارِعَةُ ٢Ni kitu gani hiko chenye kugonga وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡقَارِعَةُ ٣Na ni lipi lililokujulisha ni kipi hiko chenye kugonga يَوۡمَ يَكُونُ ٱلنَّاسُ كَٱلۡفَرَاشِ ٱلۡمَبۡثُوثِ ٤Siku hiyo watu watakuwa , kwa wingi wao, kugawanyika kwao na kuzunguka kwao, ni kama pandzi walioenea. Nao ni wale wanaojitupa motoni وَتَكُونُ ٱلۡجِبَالُ كَٱلۡعِهۡنِ ٱلۡمَنفُوشِ ٥Na majabali yatakuwa ni kama pamba yenye rangi tofauti inayochambuliwa kwa mkono ikawa ni mapepe na ikamalizika فَأَمَّا مَن ثَقُلَتۡ مَوَٰزِينُهُۥ ٦Basi mwenye kuwa mizani za mema yake ni nzito فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ ٧atakuwa kwenye maisha ya kuridhika Peponi وَأَمَّا مَنۡ خَفَّتۡ مَوَٰزِينُهُۥ ٨Ama mwenye kuwa mizani za mema yake ni nyepesi na mizani za maovu yake ni nzito فَأُمُّهُۥ هَاوِيَةٌ ٩makazi yake yatakuwa ni Moto wa Jahanamu وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا هِيَهۡ ١٠Ni lipi lililokujulisha, ewe Mtume, ni ipi hii Jahanamu inayoitwa «Hāwiyah» نَارٌ حَامِيَةُۢ ١١Ni Moto unaowaka sana kwa kuni ziliomo ndani yake

Translation: Abdullah Muhammad Abu Bakr.