Millat al-Islam

Chapter 55 · 78 verses · Ali Muhsin Al Barwani

Surah Ar-Rahman in Swahili

Arabic with tafsir Listen to Surah Ar-Rahman (1411 reciters)
Medinanسورة الرحمن78 verses

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

ٱلرَّحۡمَٰنُ ١Arrah'man, Mwingi wa Rehema عَلَّمَ ٱلۡقُرۡءَانَ ٢Amefundisha Qur'ani خَلَقَ ٱلۡإِنسَٰنَ ٣Amemuumba mwanaadamu عَلَّمَهُ ٱلۡبَيَانَ ٤Akamfundisha kubaini ٱلشَّمۡسُ وَٱلۡقَمَرُ بِحُسۡبَانٍ ٥Jua na mwezi huenda kwa hisabu وَٱلنَّجۡمُ وَٱلشَّجَرُ يَسۡجُدَانِ ٦Na mimea yenye kutambaa, na miti, inanyenyekea وَٱلسَّمَآءَ رَفَعَهَا وَوَضَعَ ٱلۡمِيزَانَ ٧Na mbingu ameziinua, na ameweka mizani أَلَّا تَطۡغَوۡاْ فِي ٱلۡمِيزَانِ ٨Ili msidhulumu katika mizani وَأَقِيمُواْ ٱلۡوَزۡنَ بِٱلۡقِسۡطِ وَلَا تُخۡسِرُواْ ٱلۡمِيزَانَ ٩Na wekeni mizani kwa haki, wala msipunje katika mizani وَٱلۡأَرۡضَ وَضَعَهَا لِلۡأَنَامِ ١٠Na ardhi ameiweka kwa ajili ya viumbe فِيهَا فَٰكِهَةٌ وَٱلنَّخۡلُ ذَاتُ ٱلۡأَكۡمَامِ ١١Humo yamo matunda na mitende yenye mafumba وَٱلۡحَبُّ ذُو ٱلۡعَصۡفِ وَٱلرَّيۡحَانُ ١٢Na nafaka zenye makapi, na rehani فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ١٣Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha خَلَقَ ٱلۡإِنسَٰنَ مِن صَلۡصَٰلٍ كَٱلۡفَخَّارِ ١٤Amemuumba mtu kwa udongo wa kinamo وَخَلَقَ ٱلۡجَآنَّ مِن مَّارِجٍ مِّن نَّارٍ ١٥Na akawaumba majini kwa ulimi wa moto فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ١٦Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha رَبُّ ٱلۡمَشۡرِقَيۡنِ وَرَبُّ ٱلۡمَغۡرِبَيۡنِ ١٧Mola Mlezi wa mashariki mbili na wa magharibi mbili فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ١٨Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha مَرَجَ ٱلۡبَحۡرَيۡنِ يَلۡتَقِيَانِ ١٩Anaziendesha bahari mbili zikutane بَيۡنَهُمَا بَرۡزَخٌ لَّا يَبۡغِيَانِ ٢٠Baina yao kipo kizuizi, zisiingiliane فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٢١Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha يَخۡرُجُ مِنۡهُمَا ٱللُّؤۡلُؤُ وَٱلۡمَرۡجَانُ ٢٢Katika hizo bahari mbili zinatoka lulu na marijani فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٢٣Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha وَلَهُ ٱلۡجَوَارِ ٱلۡمُنشَـَٔاتُ فِي ٱلۡبَحۡرِ كَٱلۡأَعۡلَٰمِ ٢٤Na ni vyake Yeye hivi viendavyo baharini vilivyo undwa kama vilima فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٢٥Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha كُلُّ مَنۡ عَلَيۡهَا فَانٍ ٢٦Kila kilioko juu yake kitatoweka وَيَبۡقَىٰ وَجۡهُ رَبِّكَ ذُو ٱلۡجَلَٰلِ وَٱلۡإِكۡرَامِ ٢٧Na atabakia Mwenyewe Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٢٨Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha يَسۡـَٔلُهُۥ مَن فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ كُلَّ يَوۡمٍ هُوَ فِي شَأۡنٍ ٢٩Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika mambo فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٣٠Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha سَنَفۡرُغُ لَكُمۡ أَيُّهَ ٱلثَّقَلَانِ ٣١Tutakuhisabuni enyi makundi mawili فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٣٢Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha يَٰمَعۡشَرَ ٱلۡجِنِّ وَٱلۡإِنسِ إِنِ ٱسۡتَطَعۡتُمۡ أَن تَنفُذُواْ مِنۡ أَقۡطَارِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ فَٱنفُذُواْۚ لَا تَنفُذُونَ إِلَّا بِسُلۡطَٰنٍ ٣٣Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa madaraka فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٣٤Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha يُرۡسَلُ عَلَيۡكُمَا شُوَاظٌ مِّن نَّارٍ وَنُحَاسٌ فَلَا تَنتَصِرَانِ ٣٥Mtapelekewa muwako wa moto na shaba; wala hamtashinda فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٣٦Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha فَإِذَا ٱنشَقَّتِ ٱلسَّمَآءُ فَكَانَتۡ وَرۡدَةً كَٱلدِّهَانِ ٣٧Itakapo pasuka mbingu ikawa nyekundu kama mafuta فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٣٨Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha فَيَوۡمَئِذٍ لَّا يُسۡـَٔلُ عَن ذَنۢبِهِۦٓ إِنسٌ وَلَا جَآنٌّ ٣٩Siku hiyo hataulizwa dhambi zake mtu wala jini فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٤٠Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha يُعۡرَفُ ٱلۡمُجۡرِمُونَ بِسِيمَٰهُمۡ فَيُؤۡخَذُ بِٱلنَّوَٰصِي وَٱلۡأَقۡدَامِ ٤١Watajuulikana wakosefu kwa alama zao, basi watashikwa kwa nywele zao za utosini na kwa miguu فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٤٢Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha هَٰذِهِۦ جَهَنَّمُ ٱلَّتِي يُكَذِّبُ بِهَا ٱلۡمُجۡرِمُونَ ٤٣Hii ndiyo Jahannamu ambayo wakosefu wakiikanusha يَطُوفُونَ بَيۡنَهَا وَبَيۡنَ حَمِيمٍ ءَانٍ ٤٤Watakuwa wakizunguka baina ya hiyo na maji ya moto yanayo chemka فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٤٥Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha وَلِمَنۡ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِۦ جَنَّتَانِ ٤٦Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi atapata Bustani mbili فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٤٧Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha ذَوَاتَآ أَفۡنَانٍ ٤٨Bustani zenye matawi yaliyo tanda فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٤٩Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha فِيهِمَا عَيۡنَانِ تَجۡرِيَانِ ٥٠Ndani yake zimo chemchem mbili zinazo pita فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٥١Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha فِيهِمَا مِن كُلِّ فَٰكِهَةٍ زَوۡجَانِ ٥٢Humo katika kila matunda zimo namna mbili فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٥٣Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha مُتَّكِـِٔينَ عَلَىٰ فُرُشِۭ بَطَآئِنُهَا مِنۡ إِسۡتَبۡرَقٍۚ وَجَنَى ٱلۡجَنَّتَيۡنِ دَانٍ ٥٤Wawe wameegemea matandiko yenye bit'ana ya hariri nzito; na matunda ya Bustani hizo yapo karibu فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٥٥Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha فِيهِنَّ قَٰصِرَٰتُ ٱلطَّرۡفِ لَمۡ يَطۡمِثۡهُنَّ إِنسٌ قَبۡلَهُمۡ وَلَا جَآنٌّ ٥٦Humo watakuwamo wanawake watulizao macho yao; hajawagusa mtu kabla yao wala jini فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٥٧Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha كَأَنَّهُنَّ ٱلۡيَاقُوتُ وَٱلۡمَرۡجَانُ ٥٨Kama kwamba wao ni yakuti na marijani فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٥٩Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha هَلۡ جَزَآءُ ٱلۡإِحۡسَٰنِ إِلَّا ٱلۡإِحۡسَٰنُ ٦٠Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٦١Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha وَمِن دُونِهِمَا جَنَّتَانِ ٦٢Na zaidi ya hizo zipo Bustani nyengine mbili فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٦٣Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha مُدۡهَآمَّتَانِ ٦٤Za kijani kibivu فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٦٥Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha فِيهِمَا عَيۡنَانِ نَضَّاخَتَانِ ٦٦Na chemchem mbili zinazo furika فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٦٧Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha فِيهِمَا فَٰكِهَةٌ وَنَخۡلٌ وَرُمَّانٌ ٦٨Imo humo miti ya matunda, na mitende na mikomamanga فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٦٩Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha فِيهِنَّ خَيۡرَٰتٌ حِسَانٌ ٧٠Humo wamo wanawake wema wazuri فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٧١Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha حُورٌ مَّقۡصُورَٰتٌ فِي ٱلۡخِيَامِ ٧٢Wanawake wazuri wanao tawishwa katika makhema فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٧٣Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha لَمۡ يَطۡمِثۡهُنَّ إِنسٌ قَبۡلَهُمۡ وَلَا جَآنٌّ ٧٤Hajawagusa mtu wala jini kabla yao فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٧٥Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha مُتَّكِـِٔينَ عَلَىٰ رَفۡرَفٍ خُضۡرٍ وَعَبۡقَرِيٍّ حِسَانٍ ٧٦Wameegemea juu ya matakia ya kijani na mazulia mazuri فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ٧٧Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha تَبَٰرَكَ ٱسۡمُ رَبِّكَ ذِي ٱلۡجَلَٰلِ وَٱلۡإِكۡرَامِ ٧٨Limetukuka jina la Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu

Translation: Ali Muhsin Al Barwani.