ملة الإسلام

السورة 80 · 42 آية · Abdullah Muhammad Abu Bakr

سورة عبس باللغة السواحلية

السورة بالعربية مع التفسير استمع إلى سورة عبس (1,320 قارئاً)
مكيةسورة عبس٤٢ آية

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

عَبَسَ وَتَوَلَّىٰٓ ١Yalidhihiri mabadiliko na mkunjiko katika uso wa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie أَن جَآءَهُ ٱلۡأَعۡمَىٰ ٢na akapa nyongo kwa sababu ya kwamba Abdallah bin Ummi Maktum alimjilia akitaka aelekezwe. Na alikuwa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ameshughulika kuwalingania miamba wa Kikureshi katika Uislamu وَمَا يُدۡرِيكَ لَعَلَّهُۥ يَزَّكَّىٰٓ ٣Ni kitu gani kinakufanya wewe ujue uhakika wa jambo lake? Kwani huenda ikawa, kwa kuuliza kwake, nafsi yake itatakasika na kusafika أَوۡ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ ٱلذِّكۡرَىٰٓ ٤Au pengine apate mazingatio zaidi na kutishika أَمَّا مَنِ ٱسۡتَغۡنَىٰ ٥Basi yule alijyejitosheleza na kutouhitajia uongozi wako فَأَنتَ لَهُۥ تَصَدَّىٰ ٦wewe ndiye unayemjali na wapulikiza maneno yake وَمَا عَلَيۡكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ ٧Na ni kitu gani kinachokupa jukumu kwako iwapo hakusafika na ukafiri wake وَأَمَّا مَن جَآءَكَ يَسۡعَىٰ ٨Ama yule ambaye amekuwa na pupa la kukutana na wewe وَهُوَ يَخۡشَىٰ ٩na huku anamuogopa Mwenyezi Mungu asiwe na kasoro katika kupata uongofu فَأَنتَ عَنۡهُ تَلَهَّىٰ ١٠wewe unampuuza. Ilivyotakikana ufanye si kama ulivyofanya, ewe Mtume كـَلَّآ إِنَّهَا تَذۡكِرَةٌ ١١Hakika Sura hii ni mawaidha kwako na kwa kila anayetaka kuwaidhika فَمَن شَآءَ ذَكَرَهُۥ ١٢Basi atakaye atamkumbuka Mwenyezi Mungu na kumtaja na atafuata Wahyi Wake فِي صُحُفٍ مُّكَرَّمَةٍ ١٣Wahyi huu, nao ni Qur’ani, uko katika kurasa zilizotukuzwa مَّرۡفُوعَةٍ مُّطَهَّرَةِۭ ١٤zenye kuheshimiwa, zenye cheo cha juu بِأَيۡدِي سَفَرَةٍ ١٥zilizosafishwa na uchafu, uongezaji na upunguzaji كِرَامِۭ بَرَرَةٍ ١٦Zilizoko mikononi mwa Malaika waandishi, mabalozi kati ya Mwenyezi Mungu na viumbe Wake, wenye maumbile mema, tabia zao ni nzuri na njema na pia matendo yao قُتِلَ ٱلۡإِنسَٰنُ مَآ أَكۡفَرَهُۥ ١٧Amelaaniwa mtu kafiri na ataadhibiwa. Ni uovu ulioje wa ukafiri wake kwa Mola wake مِنۡ أَيِّ شَيۡءٍ خَلَقَهُۥ ١٨Kwani hajui ni kwa kitu gani Mwenyezi Mungu Alimuumba kwacho mwanzo wake مِن نُّطۡفَةٍ خَلَقَهُۥ فَقَدَّرَهُۥ ١٩Mwenyezi Mungu Alimuumba kwa maji machache, nayo ni manii. Akayakadiria miongo yake ثُمَّ ٱلسَّبِيلَ يَسَّرَهُۥ ٢٠Kisha Akambainishia njia ya kheri na ya shari ثُمَّ أَمَاتَهُۥ فَأَقۡبَرَهُۥ ٢١Kisha humkosesha uhai, na Amemuekea mahali pa kuzikiwa ثُمَّ إِذَا شَآءَ أَنشَرَهُۥ ٢٢Kisha Akitaka Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na sifa mbaya, Atamhuisha na kumfufua baada ya kifo chake, kwa ajili ya kuhesabiwa na kulipwa كـَلَّا لَمَّا يَقۡضِ مَآ أَمَرَهُۥ ٢٣Mambo siyo kama yale anayoyasema kafiri na anayoyafanya. Bado hajatakeleza Aliyomuamrisha kwayo Mwenyezi Mungu katika kuamini na kutenda wema kwa kumtii فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَٰنُ إِلَىٰ طَعَامِهِۦٓ ٢٤Na azingatie binadamu, vipi Mwenyezi Mungu Amekiumba chakula chake ambacho ndicho kinachoendeleza maisha yake أَنَّا صَبَبۡنَا ٱلۡمَآءَ صَبًّا ٢٥Aone kwamba Sisi Tumeyamimina maji ya mvua juu ya ardhi kwa wingi ثُمَّ شَقَقۡنَا ٱلۡأَرۡضَ شَقًّا ٢٦Kisha Tumeipasua ardhi kwa Tulivyo vitoa kutoka humo miongoni mwa mimea tofauti فَأَنۢبَتۡنَا فِيهَا حَبًّا ٢٧Tukaotesha humo nafaka وَعِنَبًا وَقَضۡبًا ٢٨na zabibu, na nyasi za wanyama.Na mizaituni na mitende وَزَيۡتُونًا وَنَخۡلًا ٢٩Na mabustani yenye miti mikubwa وَحَدَآئِقَ غُلۡبًا ٣٠Na matunda وَفَٰكِهَةً وَأَبًّا ٣١na ndisha مَّتَٰعًا لَّكُمۡ وَلِأَنۡعَٰمِكُمۡ ٣٢Mnajistareheshea kwazo, nyinyi na wanyama wenu فَإِذَا جَآءَتِ ٱلصَّآخَّةُ ٣٣Utakapokuja Ukelele wa Siku ya Kiyama, ambao utayatia uziwi, kwa kitisho chake, masikizi يَوۡمَ يَفِرُّ ٱلۡمَرۡءُ مِنۡ أَخِيهِ ٣٤Siku mtu atakapomkimbia, kwa kitisho cha Siku Hiyo, nduguye وَأُمِّهِۦ وَأَبِيهِ ٣٥na babake na mamake na وَصَٰحِبَتِهِۦ وَبَنِيهِ ٣٦mkewe na wanawe لِكُلِّ ٱمۡرِيٍٕ مِّنۡهُمۡ يَوۡمَئِذٍ شَأۡنٌ يُغۡنِيهِ ٣٧Kila mmoja Siku Hiyo, atakuwa na jambo litakalomzuia asishughulike na mwingine وُجُوهٌ يَوۡمَئِذٍ مُّسۡفِرَةٌ ٣٨Nyuso za wenye neema, Siku Hiyo, zitakuwa ni zenye kung’ara ضَاحِكَةٌ مُّسۡتَبۡشِرَةٌ ٣٩zenye furaha na nderemo وَوُجُوهٌ يَوۡمَئِذٍ عَلَيۡهَا غَبَرَةٌ ٤٠Na nyuso za watu wa Motoni zitakuwa na giza تَرۡهَقُهَا قَتَرَةٌ ٤١nyeusi, zafinikwa na unyonge أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡكَفَرَةُ ٱلۡفَجَرَةُ ٤٢Hao wenye kusifika na sifa hiyo ndiwo wale waliozikufuru neema za Mwenyezi Mungu na wakazikanusha aya zake na wakayakeuka Aliyoyaharamisha kwa kutenda maovu na kukiuka mipaka

الترجمة: Abdullah Muhammad Abu Bakr.