ملة الإسلام

السورة 80 · 42 آية · Ali Muhsin Al Barwani

سورة عبس باللغة السواحلية

السورة بالعربية مع التفسير استمع إلى سورة عبس (1,320 قارئاً)
مكيةسورة عبس٤٢ آية

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

عَبَسَ وَتَوَلَّىٰٓ ١Alikunja kipaji na akageuka أَن جَآءَهُ ٱلۡأَعۡمَىٰ ٢Kwa sababu alimjia kipofu وَمَا يُدۡرِيكَ لَعَلَّهُۥ يَزَّكَّىٰٓ ٣Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika أَوۡ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ ٱلذِّكۡرَىٰٓ ٤Au atawaidhika, na mawaidha yamfae أَمَّا مَنِ ٱسۡتَغۡنَىٰ ٥Ama ajionaye hana haja فَأَنتَ لَهُۥ تَصَدَّىٰ ٦Wewe ndio unamshughulikia وَمَا عَلَيۡكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ ٧Na si juu yako kama hakutakasika وَأَمَّا مَن جَآءَكَ يَسۡعَىٰ ٨Ama anaye kujia kwa juhudi وَهُوَ يَخۡشَىٰ ٩Naye anaogopa فَأَنتَ عَنۡهُ تَلَهَّىٰ ١٠Ndio wewe unampuuza كـَلَّآ إِنَّهَا تَذۡكِرَةٌ ١١Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana فَمَن شَآءَ ذَكَرَهُۥ ١٢Basi anaye penda akumbuke فِي صُحُفٍ مُّكَرَّمَةٍ ١٣Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa مَّرۡفُوعَةٍ مُّطَهَّرَةِۭ ١٤Zilizo inuliwa, zilizo takaswa بِأَيۡدِي سَفَرَةٍ ١٥Zimo mikononi mwa Malaika waandishi كِرَامِۭ بَرَرَةٍ ١٦Watukufu, wema قُتِلَ ٱلۡإِنسَٰنُ مَآ أَكۡفَرَهُۥ ١٧Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha مِنۡ أَيِّ شَيۡءٍ خَلَقَهُۥ ١٨Kwa kitu gani amemuumba مِن نُّطۡفَةٍ خَلَقَهُۥ فَقَدَّرَهُۥ ١٩Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria ثُمَّ ٱلسَّبِيلَ يَسَّرَهُۥ ٢٠Kisha akamsahilishia njia ثُمَّ أَمَاتَهُۥ فَأَقۡبَرَهُۥ ٢١Kisha akamfisha, akamtia kaburini ثُمَّ إِذَا شَآءَ أَنشَرَهُۥ ٢٢Kisha apendapo atamfufua كـَلَّا لَمَّا يَقۡضِ مَآ أَمَرَهُۥ ٢٣La! Hajamaliza aliyo muamuru فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَٰنُ إِلَىٰ طَعَامِهِۦٓ ٢٤Hebu mtu na atazame chakula chake أَنَّا صَبَبۡنَا ٱلۡمَآءَ صَبًّا ٢٥Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu ثُمَّ شَقَقۡنَا ٱلۡأَرۡضَ شَقًّا ٢٦Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu فَأَنۢبَتۡنَا فِيهَا حَبًّا ٢٧Kisha tukaotesha humo nafaka وَعِنَبًا وَقَضۡبًا ٢٨Na zabibu, na mimea ya majani وَزَيۡتُونًا وَنَخۡلًا ٢٩Na mizaituni, na mitende وَحَدَآئِقَ غُلۡبًا ٣٠Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara وَفَٰكِهَةً وَأَبًّا ٣١Na matunda, na malisho ya wanyama مَّتَٰعًا لَّكُمۡ وَلِأَنۡعَٰمِكُمۡ ٣٢Kwa manufaa yenu na mifugo yenu فَإِذَا جَآءَتِ ٱلصَّآخَّةُ ٣٣Basi utakapo kuja ukelele يَوۡمَ يَفِرُّ ٱلۡمَرۡءُ مِنۡ أَخِيهِ ٣٤Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye وَأُمِّهِۦ وَأَبِيهِ ٣٥Na mamaye na babaye وَصَٰحِبَتِهِۦ وَبَنِيهِ ٣٦Na mkewe na wanawe لِكُلِّ ٱمۡرِيٍٕ مِّنۡهُمۡ يَوۡمَئِذٍ شَأۡنٌ يُغۡنِيهِ ٣٧Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha وُجُوهٌ يَوۡمَئِذٍ مُّسۡفِرَةٌ ٣٨Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri ضَاحِكَةٌ مُّسۡتَبۡشِرَةٌ ٣٩Zitacheka, zitachangamka وَوُجُوهٌ يَوۡمَئِذٍ عَلَيۡهَا غَبَرَةٌ ٤٠Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi تَرۡهَقُهَا قَتَرَةٌ ٤١Giza totoro litazifunika أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡكَفَرَةُ ٱلۡفَجَرَةُ ٤٢Hao ndio makafiri watenda maovu

الترجمة: Ali Muhsin Al Barwani.