ملة الإسلام

السورة 96 · 19 آية · Abdullah Muhammad Abu Bakr

سورة العلق باللغة السواحلية

السورة بالعربية مع التفسير استمع إلى سورة العلق (1,283 قارئاً)
مكيةسورة العلق١٩ آية

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

ٱقۡرَأۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلَّذِي خَلَقَ ١Soma, ewe Nabii, Qur’ani uliyoteremshiwa ukianza kwa Jina la Mola wako Aliyepwekeka kwa kuumba خَلَقَ ٱلۡإِنسَٰنَ مِنۡ عَلَقٍ ٢Aliyemuumba kila binadamu kwa pande la damu nzito nyekundu ٱقۡرَأۡ وَرَبُّكَ ٱلۡأَكۡرَمُ ٣Soma, ewe Nabii, kile ulichoteremshiwa, na Mola wako ni Mwingi wa wema, Mwingi wa ukarimu ٱلَّذِي عَلَّمَ بِٱلۡقَلَمِ ٤Aliyewafundisha viumbe vyake kuandika kwa kalamu عَلَّمَ ٱلۡإِنسَٰنَ مَا لَمۡ يَعۡلَمۡ ٥Alimfundisha binadamu vitu ambavyo hakuwa akivijua. Akamtoa kwenye giza la ujinga, Akampeleka kwenye nuru ya elimu كـَلَّآ إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ لَيَطۡغَىٰٓ ٦Kweli, binadamu hukiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu أَن رَّءَاهُ ٱسۡتَغۡنَىٰٓ ٧akijiona ametosheka kwa utajiri wake إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلرُّجۡعَىٰٓ ٨Basi, ajue kila mwenye kutupa mipaka kuwa mwisho atarudi kwa Mwenyezi Mungu Ambaye Atamlipa kila binadamu kwa alilolitenda أَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي يَنۡهَىٰ ٩Je, umeona ujeuri wa ajabu zaidi kuliko wa mtu huyu, Abu jahl عَبۡدًا إِذَا صَلَّىٰٓ ١٠Anayemkataza mja wetu, Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, anapomsalia Mola wake أَرَءَيۡتَ إِن كَانَ عَلَى ٱلۡهُدَىٰٓ ١١Waonaje iwapo mwenye kukatazwa kusali yuko uongofuni, vipi anamkataza أَوۡ أَمَرَ بِٱلتَّقۡوَىٰٓ ١٢Au iwapo anaamrisha mwigine kumcha Mungu, vipi anamkataza hilo أَرَءَيۡتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰٓ ١٣Waonaje iwapo huyu mwenye kukataza anakanusha lile alinganiwalo kwalo na kulipa mgongo أَلَمۡ يَعۡلَم بِأَنَّ ٱللَّهَ يَرَىٰ ١٤hajui kuwa Mwenyezi Mungu anaona kila analolifanya كـَلَّا لَئِن لَّمۡ يَنتَهِ لَنَسۡفَعَۢا بِٱلنَّاصِيَةِ ١٥Basi mambo si kama anvyodai Abu Jahl. Na asipokomeka na ushindani alionao na udhia wake, Tutamshika upaa wake kwa nguvu na kumtia Motoni نَاصِيَةٍ كَٰذِبَةٍ خَاطِئَةٍ ١٦Upaa wake ni upaa wenye maneno ya urongo na vitendo vya makosa فَلۡيَدۡعُ نَادِيَهُۥ ١٧Basi na awalete, mtupaji mipaka huyu, watu wa baraza ili wamsaidiye سَنَدۡعُ ٱلزَّبَانِيَةَ ١٨Sisi Tutawaita Malaika wa adhabu كـَلَّا لَا تُطِعۡهُ وَٱسۡجُدۡۤ وَٱقۡتَرِب ۩ ١٩Mambo si kama Abu Jahl anavyoyadhania. Yeye, ewe Mtume, hawezi kukufanya lolote la kukudhuru Usimfuate kwa lile alilokuitia la kuwa uache Swala, bali msujudie Mola wako na uwe karibu na Yeye kwa kujipendekeza Kwake kwa kumtii

الترجمة: Abdullah Muhammad Abu Bakr.