بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
ٱقۡرَأۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلَّذِي خَلَقَ ١Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba خَلَقَ ٱلۡإِنسَٰنَ مِنۡ عَلَقٍ ٢Amemuumba binaadamu kwa tone la damu ٱقۡرَأۡ وَرَبُّكَ ٱلۡأَكۡرَمُ ٣Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote ٱلَّذِي عَلَّمَ بِٱلۡقَلَمِ ٤Ambaye amefundisha kwa kalamu عَلَّمَ ٱلۡإِنسَٰنَ مَا لَمۡ يَعۡلَمۡ ٥Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui كـَلَّآ إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ لَيَطۡغَىٰٓ ٦Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri أَن رَّءَاهُ ٱسۡتَغۡنَىٰٓ ٧Akijiona katajirika إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلرُّجۡعَىٰٓ ٨Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo أَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي يَنۡهَىٰ ٩Umemwona yule anaye mkataza عَبۡدًا إِذَا صَلَّىٰٓ ١٠Mja anapo sali أَرَءَيۡتَ إِن كَانَ عَلَى ٱلۡهُدَىٰٓ ١١Umeona kama yeye yuko juu ya uwongofu أَوۡ أَمَرَ بِٱلتَّقۡوَىٰٓ ١٢Au anaamrisha uchamngu أَرَءَيۡتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰٓ ١٣Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma أَلَمۡ يَعۡلَم بِأَنَّ ٱللَّهَ يَرَىٰ ١٤Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona كـَلَّا لَئِن لَّمۡ يَنتَهِ لَنَسۡفَعَۢا بِٱلنَّاصِيَةِ ١٥Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele نَاصِيَةٍ كَٰذِبَةٍ خَاطِئَةٍ ١٦Shungi la uwongo, lenye makosa فَلۡيَدۡعُ نَادِيَهُۥ ١٧Basi na awaite wenzake سَنَدۡعُ ٱلزَّبَانِيَةَ ١٨Nasi tutawaita Mazabania كـَلَّا لَا تُطِعۡهُ وَٱسۡجُدۡۤ وَٱقۡتَرِب ۩ ١٩Hasha! Usimt'ii! Nawe sujudu na ujongee