ملة الإسلام

السورة 89 · 30 آية · Abdullah Muhammad Abu Bakr

سورة الفجر باللغة السواحلية

السورة بالعربية مع التفسير استمع إلى سورة الفجر (1,345 قارئاً)
مكيةسورة الفجر٣٠ آية

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلۡفَجۡرِ ١Mwenyezi Mungu Anaapa kwa wakati wa alfajiri وَلَيَالٍ عَشۡرٍ ٢na masiku kumi ya kwanza ya Mfungotatu na kwa kile kilichoyafanya yawe matukufu وَٱلشَّفۡعِ وَٱلۡوَتۡرِ ٣kwa kila idadi igawanyikayo na isiyogawanyika وَٱلَّيۡلِ إِذَا يَسۡرِ ٤kwa usiku upitapo na giza lake هَلۡ فِي ذَٰلِكَ قَسَمٌ لِّذِي حِجۡرٍ ٥Kwani hakuna katika kiapo kiliyotajwa chenye kukinaisha kwa mwenye akili أَلَمۡ تَرَ كَيۡفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِعَادٍ ٦Huoni, ewe Mtume, vipi Mola wako إِرَمَ ذَاتِ ٱلۡعِمَادِ ٧Alivyoiangamiza kaumu ya Ād'. kabila la Irama lenye nguvu na majengo yaliyoinuliwa juu ya vipia ٱلَّتِي لَمۡ يُخۡلَقۡ مِثۡلُهَا فِي ٱلۡبِلَٰدِ ٨ambalo hakukuumbwa mfano wake katika miji, kwa ukubwa wa miili na wingi wa nguvu وَثَمُودَ ٱلَّذِينَ جَابُواْ ٱلصَّخۡرَ بِٱلۡوَادِ ٩Na vipi Alivyowafanya Thamūd, kaumu ya Ṣāliḥ, ambao waliweza kuchonga jabali na kufanya nyumba ndani yake وَفِرۡعَوۡنَ ذِي ٱلۡأَوۡتَادِ ١٠Na vipi Alivyomfanya Firauni, mfalme wa Misri, aliyekuwa na askari waliouhami ufalme wake na kuutilia nguvu ٱلَّذِينَ طَغَوۡاْ فِي ٱلۡبِلَٰدِ ١١Hawa ndio waliokitumia nguvu na kudhulumu mijini فَأَكۡثَرُواْ فِيهَا ٱلۡفَسَادَ ١٢Wakaeneza humo, kwa dhuluma zao, uharibifu فَصَبَّ عَلَيۡهِمۡ رَبُّكَ سَوۡطَ عَذَابٍ ١٣Mwenyezi Mungu Akawamiminia adhabu kali إِنَّ رَبَّكَ لَبِٱلۡمِرۡصَادِ ١٤Hakika Mola wako,ewe Mtume, Anamwangalia mwenye kumuasi kwa kumpa muhula kidogo, kisha Humpatiliza kwa uwezo na ushindi فَأَمَّا ٱلۡإِنسَٰنُ إِذَا مَا ٱبۡتَلَىٰهُ رَبُّهُۥ فَأَكۡرَمَهُۥ وَنَعَّمَهُۥ فَيَقُولُ رَبِّيٓ أَكۡرَمَنِ ١٥Huyu binadamu, Mola wake Anapompa mtihani wa neema, Anapomkunjulia riziki yake na kumpa maisha mazuri, huwa akidhani kuwa hayo ni kwa kuwa yeye ana cheo kwa Mola wake na huwa akisema :»Mola wangu Amenitukuza.» وَأَمَّآ إِذَا مَا ٱبۡتَلَىٰهُ فَقَدَرَ عَلَيۡهِ رِزۡقَهُۥ فَيَقُولُ رَبِّيٓ أَهَٰنَنِ ١٦Na Anapomuonja na Akambania riziki yake, huwa akidhani kuwa hayo ni kwa kuwa yeye amefanywa mnyonge na Mwenyezi Mungu na huwa akisema: «Mola wangu Amenifanya mnyonge.» كـَلَّاۖ بَل لَّا تُكۡرِمُونَ ٱلۡيَتِيمَ ١٧Hali ya mambo si kama anavyodhania binadamu huyu, kwani mtu hutukuzwa kwa kumtii Mwenyzi Mungu na hufanywa mnyonge kwa kumuasi Mwenyezi Mungu. Na nyinyi hamwakirimu mayatima na kuwatendea wema وَلَا تَحَٰٓضُّونَ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ ١٨Wala hamhimizani kulisha maskini وَتَأۡكُلُونَ ٱلتُّرَاثَ أَكۡلًا لَّمًّا ١٩Na mnakula haki za watu, katika kurithi, kwa pupa وَتُحِبُّونَ ٱلۡمَالَ حُبًّا جَمًّا ٢٠Na mnapenda mali kupita kiasi كـَلَّآۖ إِذَا دُكَّتِ ٱلۡأَرۡضُ دَكًّا دَكًّا ٢١Basi hali zenu zisiwe namna hiyo. Kumbukeni pindi ardhi itakapotikiswa na kuvunjwavunjwa وَجَآءَ رَبُّكَ وَٱلۡمَلَكُ صَفًّا صَفًّا ٢٢Na Akaja Mola wako kutoa uamuzi kwa waja Wake hali Malaika wamepiga safu وَجِاْيٓءَ يَوۡمَئِذِۭ بِجَهَنَّمَۚ يَوۡمَئِذٍ يَتَذَكَّرُ ٱلۡإِنسَٰنُ وَأَنَّىٰ لَهُ ٱلذِّكۡرَىٰ ٢٣Na ukaletwa, Siku Hiyo kubwa, moto wa Jahanamu. Hiyo ndiyo Siku kafiri atakumbuka na kutubia. Kutamfalia nini sasa kukumbuka kwake na kutubia, na yeye katika ulimwengu alikuwa ameyapuuza hayo, na wakati wake umekwisha kupita يَقُولُ يَٰلَيۡتَنِي قَدَّمۡتُ لِحَيَاتِي ٢٤Atakuwa akisema: ‘Laiti mimi nilitanguliza ulimwenguni amali zenye kunifaa katika maisha yangu ya Akhera’ فَيَوۡمَئِذٍ لَّا يُعَذِّبُ عَذَابَهُۥٓ أَحَدٌ ٢٥Katika Siku Hiyo ngumu yenye vituko, hakuna atakaye kuweza kuadhibu kama adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa anayemuasi وَلَا يُوثِقُ وَثَاقَهُۥٓ أَحَدٌ ٢٦Na hakuna atakaye kuweza kufunga kama kifungo Chake wala kufikia hadi yake يَٰٓأَيَّتُهَا ٱلنَّفۡسُ ٱلۡمُطۡمَئِنَّةُ ٢٧Ewe nafsi iliyotulia kwa kumtaja Mwenyezi Mungu, kumwamini Yeye na kuamini starehe ya Pepo Aliyowaandalia waumini ٱرۡجِعِيٓ إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةً مَّرۡضِيَّةً ٢٨Rudi kwa Mola wako hali ya kuridhika na takrima ya Mwenyezi Mungu kwako na hali ya kuwa Mwenyezi Mungu Ameridhika na wewe فَٱدۡخُلِي فِي عِبَٰدِي ٢٩Ingia miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu walio wema وَٱدۡخُلِي جَنَّتِي ٣٠na ingia kwenye Pepo yangu

الترجمة: Abdullah Muhammad Abu Bakr.