بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
لَآ أُقۡسِمُ بِهَٰذَا ٱلۡبَلَدِ ١Mwenyezi Mungu Anaapa kwa mji huu mtakatifu wa Makkah وَأَنتَ حِلُّۢ بِهَٰذَا ٱلۡبَلَدِ ٢Na wewe, ewe Nabii, ni mkazi wa mji huu mtakatifu وَوَالِدٍ وَمَا وَلَدَ ٣Na Anaapa kwa mzazi wa wanaadamu, ambaye ni Ādam, amani imshukie, na kilichozalikana na yeye لَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ فِي كَبَدٍ ٤Hakika Tumemuumba binadamu katika usumbufu na shida za kilimwengu أَيَحۡسَبُ أَن لَّن يَقۡدِرَ عَلَيۡهِ أَحَدٌ ٥Kwani anadhani kwa mali aliyoyakusanya kuwa Mwenyezi Mungu Hatakuwa na uwezo juu yake يَقُولُ أَهۡلَكۡتُ مَالًا لُّبَدًا ٦Huwa akisema kwa kujigamba: «Nimetumia mali mengi.» أَيَحۡسَبُ أَن لَّمۡ يَرَهُۥٓ أَحَدٌ ٧Kwani anadhani, kwa kitendo chake hiko, kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kushinda, Hamuoni wala hatamhesabu juu ya kubwa na dogo أَلَمۡ نَجۡعَل لَّهُۥ عَيۡنَيۡنِ ٨Kwani hatukumpa macho mawili ya kuonea وَلِسَانًا وَشَفَتَيۡنِ ٩ulimi na midomo miwili ya kusemea وَهَدَيۡنَٰهُ ٱلنَّجۡدَيۡنِ ١٠na kumfafanulia njia mbili: ya kheri na ya shari فَلَا ٱقۡتَحَمَ ٱلۡعَقَبَةَ ١١Basi ajiepushe na janga la Akhera kwa kutoa mali yake ili aokoke وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡعَقَبَةُ ١٢Ni kitu gani kilichojulisha ni lipi hilo janga la Akhera na ni mambo gani yenye kusaidia kujiepusha nalo فَكُّ رَقَبَةٍ ١٣Ni kuacha huru shingo iliyoamini kuikomboa na utumwa أَوۡ إِطۡعَٰمٌ فِي يَوۡمٍ ذِي مَسۡغَبَةٍ ١٤Au kulisha, wakati wa shida ya njaa يَتِيمًا ذَا مَقۡرَبَةٍ ١٥yatima mwenye ujamaa, ili ipatikane fadhila ya sadaka na ya kuunga kizazi أَوۡ مِسۡكِينًا ذَا مَتۡرَبَةٍ ١٦au masikini asiyekuwa na kitu ثُمَّ كَانَ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَتَوَاصَوۡاْ بِٱلصَّبۡرِ وَتَوَاصَوۡاْ بِٱلۡمَرۡحَمَةِ ١٧Kisha akawa, baada ya kufanya amali njema zilizotajwa, ni miongoni mwa waliotakasa Imani yao kwa Mwenyezi Mungu, wakausiana kusubiri juu ya kumtii Mwenyezi Mungu kwa kufuata maamrisho Yake na kujiepusha na vitendo vya kumuasi na wakausiana kuwahurumia viumbe أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ ١٨Wenye kufanya hayo ndiwo watu wa kulia ambao watapelekwa Siku ya Kiyama upande wa kulia kuelekea Peponi وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِنَا هُمۡ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ ١٩Na wale waliokanusha Qur’ani ndio ambao watapelekwa, Siku ya Kiyama, upande wa kushoto kuelekea Motoni عَلَيۡهِمۡ نَارٌ مُّؤۡصَدَةُۢ ٢٠Malipo yao ni Moto wa Jahanamu wenye kuwafinika na kuwaziba