ملة الإسلام

السورة 82 · 19 آية · Abdullah Muhammad Abu Bakr

سورة الانفطار باللغة السواحلية

السورة بالعربية مع التفسير استمع إلى سورة الانفطار (1,366 قارئاً)
مكيةسورة الانفطار١٩ آية

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنفَطَرَتۡ ١Pindi mbingu zitakapopasuka na ukaharibika mpango wake وَإِذَا ٱلۡكَوَاكِبُ ٱنتَثَرَتۡ ٢Na pindi nyota zitakapoangukiana وَإِذَا ٱلۡبِحَارُ فُجِّرَتۡ ٣Na pindi Mwenyezi Mungu Atakapozifanya bahari kulipuka na maji yake kutoweka وَإِذَا ٱلۡقُبُورُ بُعۡثِرَتۡ ٤Na pindi makaburi yatakapogeuzwa kwa kufufuliwa waliokuwamo ndani yake عَلِمَتۡ نَفۡسٌ مَّا قَدَّمَتۡ وَأَخَّرَتۡ ٥Wakati huo itajua kila nafsi vitendo vyake vyote ilivyovifanya, vilivyotangulia na vilivyoahirika na italipwa kwa vitendo hivyo يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡإِنسَٰنُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ ٱلۡكَرِيمِ ٦Ewe binadamu unayekanusha kufufuliwa! Ni kipi kilichokufanya uhadaike na ughurike kuhusu Mola wako Mpaji Mwenye kheri nyingi, Anayestahiki kushukuriwa na kutiiwa ٱلَّذِي خَلَقَكَ فَسَوَّىٰكَ فَعَدَلَكَ ٧Kwani si Yeye Aliyekuumba, Akalisawazisha umbo lako, Akakuweka katika hali ya sawa na Akakurekibisha ili uweze kutekeleza nyadhifa zako فِيٓ أَيِّ صُورَةٍ مَّا شَآءَ رَكَّبَكَ ٨katika sura yoyote ile Aliyoitaka Akakuumba كـَلَّا بَلۡ تُكَذِّبُونَ بِٱلدِّينِ ٩Mambo hayako kama vile mnavyosema kwamba nyinyi mna haki ya kumuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Hesabu na Malipo وَإِنَّ عَلَيۡكُمۡ لَحَٰفِظِينَ ١٠Na mjue kuwa wako na nyinyi Malaika wachunguzi كِرَامًا كَٰتِبِينَ ١١watukufu kwa Mwenyezi Mungu, waandishi wa yale waliyowakilishwa kuyadhibiti. Hakiwapiti, katika vitendo vyenu na siri zenu, chochote يَعۡلَمُونَ مَا تَفۡعَلُونَ ١٢Wanayajua mnayoyafanya, ya kheri au ya shari إِنَّ ٱلۡأَبۡرَارَ لَفِي نَعِيمٍ ١٣Hakika wachamungu wanaotekeleza haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake watakuwa kwenye neema وَإِنَّ ٱلۡفُجَّارَ لَفِي جَحِيمٍ ١٤Hakika watu waovu waliopuuza haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake watakuwa katika Moto mkali يَصۡلَوۡنَهَا يَوۡمَ ٱلدِّينِ ١٥Ukali wake, Moto huo, utawapata Siku ya Malipo.Na wala wao hawatakuwa ni wenye kughibu وَمَا هُمۡ عَنۡهَا بِغَآئِبِينَ ١٦wakawa hawamo ndani ya Moto wa Jahanamu, si kwa kutoka wala kwa kufa وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ ١٧Ni kipi kinachokujuza ni upi utukufu wa Siku ya Hesabu ثُمَّ مَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ ١٨Kisha ni kipi kinachokujuza ni upi utukufu wa Siku ya Hesabu يَوۡمَ لَا تَمۡلِكُ نَفۡسٌ لِّنَفۡسٍ شَيۡـًٔاۖ وَٱلۡأَمۡرُ يَوۡمَئِذٍ لِّلَّهِ ١٩Siku ya Hesabu, hataweza yoyote kumnufaisha yoyote. Na amri zote Siku Hiyo ni za Mwenyezi Mungu Peke yake Ambaye hakuna mwenye kumshinda, wala hakuna mwenye kumtendesha nguvu, wala hakuna mwenye kushindana na Yeye

الترجمة: Abdullah Muhammad Abu Bakr.