ملة الإسلام

السورة 84 · 25 آية · Abdullah Muhammad Abu Bakr

سورة الانشقاق باللغة السواحلية

السورة بالعربية مع التفسير استمع إلى سورة الانشقاق (1,276 قارئاً)
مكيةسورة الانشقاق٢٥ آية

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنشَقَّتۡ ١Pindi mbingu itakapopasuka na kudhihiri mawingu katika pasuko zake Siku ya Kiyama وَأَذِنَتۡ لِرَبِّهَا وَحُقَّتۡ ٢Na ikatii amri ya Mola wake ya kuwa ipasuke, na inastahili kufuata amri hiyo وَإِذَا ٱلۡأَرۡضُ مُدَّتۡ ٣Na pindi ardhi itakapotandikwa na kukunjuliwa وَأَلۡقَتۡ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتۡ ٤Na milima yake kuvunjwa-vunjwa Siku hiyo وَأَذِنَتۡ لِرَبِّهَا وَحُقَّتۡ ٥Na ikatii amri ya Mola wake ya kuwa ifanye hivyo, na inastahili kufuata amri hiyo يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡإِنسَٰنُ إِنَّكَ كَادِحٌ إِلَىٰ رَبِّكَ كَدۡحًا فَمُلَٰقِيهِ ٦Ewe binadamu, wewe unaenda kwa Mwenyezi Mungu na unafanya amali nzuri na mbaya, kisha utakutana na Yeye Siku ya Kiyama. Na huna budi kupata kutoka Kwake malipo mazuri zaidi ya amali yako njema au yanayolingana na amali yako mbaya فَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ ٧Yule mwenye kupewa waraka wa amali zake kwa mkono wake wa kulia فَسَوۡفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا ٨naye ni yule aliyemuamini Mola wake, atahesabiwa hesabu pesi وَيَنقَلِبُ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ مَسۡرُورًا ٩Na atarudi kwa watu wake Peponi akiwa ni mwenye furaha وَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ وَرَآءَ ظَهۡرِهِۦ ١٠Na yule mwenye kupewa waraka wa amali zake kwa nyuma ya mgongo wake فَسَوۡفَ يَدۡعُواْ ثُبُورًا ١١naye ni yule aliyemkanusha Mwenyezi Mungu, ataita maangamvu na hasara وَيَصۡلَىٰ سَعِيرًا ١٢na ataingia Motoni إِنَّهُۥ كَانَ فِيٓ أَهۡلِهِۦ مَسۡرُورًا ١٣Hakika yeye alikuwa kwa watu wake ulimwenguni ni mwenye furaha na majivuno, hafikirii mwisho wake utakuwa namna gani إِنَّهُۥ ظَنَّ أَن لَّن يَحُورَ ١٤Alidhani hatarudi kwa Muumba wake, akiwa hai, kwa kuhesabiwa بَلَىٰٓۚ إِنَّ رَبَّهُۥ كَانَ بِهِۦ بَصِيرًا ١٥Sivyo hivyo! Mwenyezi Mungu Atamrudisha kama alivomuumba na kumlipa kwa amali zake. Kwani Yeye kwake ni Mtambuzi na kwa hali yake ni Mjuzi kuanzia Alipomuumba mpaka kumfufua فَلَآ أُقۡسِمُ بِٱلشَّفَقِ ١٦Mwenyezi Mungu Ameapa kwa wekundu wa pambizo za mbingu wakati wa kutwa jua وَٱلَّيۡلِ وَمَا وَسَقَ ١٧Na kwa usiku na viunbe tofauti - tofauti vya kutambaa, kuruka na kutembea kwa miguu, uliokusanya وَٱلۡقَمَرِ إِذَا ٱتَّسَقَ ١٨Na kwa mwezi ukamilikapo mwangaza wake لَتَرۡكَبُنَّ طَبَقًا عَن طَبَقٍ ١٩Mtapitia, enyi watu, miongo mbalimbali na hali tofauti : kutoka kwenye tone la manii, kuptia pande la damu, nofu la nyama hadi kutiwa roho, mpaka kufa na mpaka kufufuliwa. Haifai kwa kiumbe kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, afanyapo hilo atakuwa ameingia kwenye ushirikina فَمَا لَهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ ٢٠Ni kitu gani kinachowazuia kumwamini baada ya aya zake kufafanuliwa kwao وَإِذَا قُرِئَ عَلَيۡهِمُ ٱلۡقُرۡءَانُ لَا يَسۡجُدُونَۤ ۩ ٢١Na wana nini wao wanaposomewa Qur’ani hawamsujudii Mwenyezi Mungu wala hawajisalimishi kufuata yaliyokuja ndani yake بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يُكَذِّبُونَ ٢٢Hakika tabia ya waliokufuru ni kuikanusha na kuikataa haki وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا يُوعُونَ ٢٣Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi wa ukaidi wao wanaouficha kwenye nyoyo zao hali wao wanajua kuwa yale yaliyoletwa na Qur’ani ni kweli فَبَشِّرۡهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ٢٤Basi wape bishara, ewe Mtume, kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kuwa juu, Amewaandalia adhabu yenye uchungu إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَهُمۡ أَجۡرٌ غَيۡرُ مَمۡنُونِۭ ٢٥Lakini wale wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakatekeleza amri waliyofaradhiwa na Mwenyezi Mungu watakuwa na malipo, Siku ya Akhera, yasiyokatika wala kupungua

الترجمة: Abdullah Muhammad Abu Bakr.