ملة الإسلام

السورة 85 · 22 آية · Abdullah Muhammad Abu Bakr

سورة البروج باللغة السواحلية

السورة بالعربية مع التفسير استمع إلى سورة البروج (1,332 قارئاً)
مكيةسورة البروج٢٢ آية

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلۡبُرُوجِ ١Mwenyezi Mungu Anaapa kwa mbingu zenye njia za kupitia jua na mwezi وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡمَوۡعُودِ ٢Na kwa Siku ya Kiyama ambayo Amewaahidi viumbe kuwa Atawakusanya وَشَاهِدٍ وَمَشۡهُودٍ ٣Na kwa shahidi, mwenye kutoa ushahidi, na mwenye kutolewa ushahidi juu yake. Mwenyezi Mungu Huapa kwa Anachokitaka. Lakini kiumbe hafai kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni ushirikina قُتِلَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡأُخۡدُودِ ٤Wamelaaniwa waliofukua chini ya ardhi shimo kubwa ili kuwatesa Waumini ٱلنَّارِ ذَاتِ ٱلۡوَقُودِ ٥Wakawasha moto mkubwa wenye kuni nyingi إِذۡ هُمۡ عَلَيۡهَا قُعُودٌ ٦Wakawa wamekaa kwenye kingo za shimo hilo وَهُمۡ عَلَىٰ مَا يَفۡعَلُونَ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ شُهُودٌ ٧Wakishuhudia vitendo vya mateso na adhabu wanavyowafanyia Waumini وَمَا نَقَمُواْ مِنۡهُمۡ إِلَّآ أَن يُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَمِيدِ ٨Na hawakuwatesa mateso hayo isipokuwa wenye kuteswa walikuwa wanamuamini Mwenyezi Mungu Mshindi Asiyeshindwa, Mhimidiwa wa maneno Yake vitendo Vyake na sifa Zake ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٍ شَهِيدٌ ٩Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi Ambaye, kutakasika na sifa za upungufu ni kwake, Anashuhudia kila kitu, hakuna kinachofichika kwake إِنَّ ٱلَّذِينَ فَتَنُواْ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ ثُمَّ لَمۡ يَتُوبُواْ فَلَهُمۡ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمۡ عَذَابُ ٱلۡحَرِيقِ ١٠Hakika, wale waliowachoma kwa moto Waumini, wa kike na wa kiume, ili kuwazuia watu na dini ya Mwenyezi Mungu, kisha wasitubie, watapata, Siku ya Akhera, adhabu ya Jahanamu na watapata adhabu kali yenye kuchoma إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَهُمۡ جَنَّٰتٌ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۚ ذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡكَبِيرُ ١١Wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakafanya amali njema, watapata Pepo ambayo chini ya majumba yake ya kifahari yapita mito. Huko ni kufaulu kukubwa إِنَّ بَطۡشَ رَبِّكَ لَشَدِيدٌ ١٢Hakika malipizo ya Mola wako kwa maadui Zake na mateso Yake juu yao ni mazito إِنَّهُۥ هُوَ يُبۡدِئُ وَيُعِيدُ ١٣Ndiye Yeye Mwenye kuanzisha kuumba na kisha kurudisha وَهُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلۡوَدُودُ ١٤Ndiye Yeye Mwingi wa kusamehe kwa wenye kutubia, Mwingi wa mapenzi kwa wanaoikurubisha kwake ذُو ٱلۡعَرۡشِ ٱلۡمَجِيدُ ١٥Mwenye Arshi tukufu فَعَّالٌ لِّمَا يُرِيدُ ١٦Mfanya Alitakalo: hakuna kitu Anachotaka kiwe kisiwe هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلۡجُنُودِ ١٧Je, ewe Mtume, imekufikia habari ya makundi yaliyokufuru na kukanusha Mitume walioletwa, ya فِرۡعَوۡنَ وَثَمُودَ ١٨Firauni na Thamūd, misiba na adhabu iliyowashukia? Hawakuzingatia kwa habari hiyo بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فِي تَكۡذِيبٍ ١٩Bali waliokufuru waendelea kukanusha kwao, kama walivyokuwa waliokuja kabla yao وَٱللَّهُ مِن وَرَآئِهِم مُّحِيطُۢ ٢٠Na Mwenyezi Mungu Amewazunguka kwa Ujuzi na Uweza Wake, hakuna chenye kufichika Kwake kuhusu wao na vitendo vyao. Hii Qu’ani siyo kama wanavyodai wenye kukanusha katika washirikina kuwa ni mashairi na uchawi ndipo wakaikanusha بَلۡ هُوَ قُرۡءَانٌ مَّجِيدٌ ٢١Bali hii ni Qur’ani kubwa iliyo tukufu فِي لَوۡحٍ مَّحۡفُوظِۭ ٢٢iliyomo kwenye Ubao Uliohifadhiwa, haufikiwi na kubadilishwa wala kupotoshwa

الترجمة: Abdullah Muhammad Abu Bakr.