بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
عَمَّ يَتَسَآءَلُونَ ١Kuhusu kitu gani baadhi ya makafiri wa Kikureshi wanaulizana عَنِ ٱلنَّبَإِ ٱلۡعَظِيمِ ٢Wanaulizana kuhusu habari iliyo na uzito mkubwa kabisa ٱلَّذِي هُمۡ فِيهِ مُخۡتَلِفُونَ ٣nayo ni Qur’ani tukufu inayotoa habari za kufufuliwa ambako makafiri wa Kikureshi wana shaka nako na wanakukanusha كـَلَّا سَيَعۡلَمُونَ ٤Mambo sivyo kama wanavyodhania hawa washirikina. Hapo watajua hawa washirikina upeo wa kukanusha kwao na kitawadhihirikia waziwazi kile Atakachowatenda Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama ثُمَّ كـَلَّا سَيَعۡلَمُونَ ٥Kisha litahakikishika kwao jambo hilo na utahakikishika kwao ukweli wa yale aliyokuja nayo Mtume Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kuhusu Qur’ani na kufufuliwa. Huu ni utisho na makemeo kwao أَلَمۡ نَجۡعَلِ ٱلۡأَرۡضَ مِهَٰدًا ٦Kwani hatukuwatandazia ardhi kama tandiko وَٱلۡجِبَالَ أَوۡتَادًا ٧Na Tukawafanyia majabali kuwa ni vigingi, ili isitisike nanyi وَخَلَقۡنَٰكُمۡ أَزۡوَٰجًا ٨Na Tukawaumba aina mbali-mbali, mume na mke وَجَعَلۡنَا نَوۡمَكُمۡ سُبَاتًا ٩Na Tukafanya usingizi wenu ni mapumziko kwa viwiliwili vyenu: ndani yake mnatulia na kupumzika وَجَعَلۡنَا ٱلَّيۡلَ لِبَاسًا ١٠Na Tukaufanya usiku kuwa ni vazi, unawavisha giza lake na kuwafinika, kama nguo inavyomsitiri mwenye kuivaa وَجَعَلۡنَا ٱلنَّهَارَ مَعَاشًا ١١Na Tukaufanya mchana ni kipindi cha kutafuta maisha, mnaenea humo kwa ajili ya maisha yenu na mnatembea humo kwa ajili ya maslahi yenu وَبَنَيۡنَا فَوۡقَكُمۡ سَبۡعًا شِدَادًا ١٢Na Tukajenga juu yenu mbingu saba, madhubuti jengo lake, lilioumbwa kwa uzuri, halina mapasuko wala nyufa وَجَعَلۡنَا سِرَاجًا وَهَّاجًا ١٣Na Tukalifanya jua kuwa ni taa iwakayo na kung’ara وَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلۡمُعۡصِرَٰتِ مَآءً ثَجَّاجًا ١٤Na Tukateremsha kutoka kwenye mawingu yanyeshayo maji yamiminikayo kwa wingi لِّنُخۡرِجَ بِهِۦ حَبًّا وَنَبَاتًا ١٥ili Tutoe kwa maji hayo nafaka inayoliwa na watu وَجَنَّٰتٍ أَلۡفَافًا ١٦nyasi zinazoliwa na wanyama na miti iliyosongamana kwa kutawanyika tagaa zake إِنَّ يَوۡمَ ٱلۡفَصۡلِ كَانَ مِيقَٰتًا ١٧Hakika Siku ya Uamuzi kati ya viumbe يَوۡمَ يُنفَخُ فِي ٱلصُّورِ فَتَأۡتُونَ أَفۡوَاجًا ١٨nayo ni Siku ya Kiyama, imekuwa ni wakati na ahadi iliyowekewa muda maalimu kwa watu wa mwanzo na wa mwisho وَفُتِحَتِ ٱلسَّمَآءُ فَكَانَتۡ أَبۡوَٰبًا ١٩Na zikafunguliwa mbingu zikawa ni zenye milango mingi kwa ajili ya kuteremka Malaika وَسُيِّرَتِ ٱلۡجِبَالُ فَكَانَتۡ سَرَابًا ٢٠Na yakalipuliwa majabali baada ya kuwa yamekita, yakawa ni kama mangati إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتۡ مِرۡصَادًا ٢١Hakika Jahanamu, Siku Hiyo, itawalindiza wenye ukafiri ambao Moto huo umeandaliwa wao لِّلطَّٰغِينَ مَـَٔابًا ٢٢Kwa makafiri ndio marejeo لَّٰبِثِينَ فِيهَآ أَحۡقَابًا ٢٣Watabakia humo muda mrefu ufuatanao, usiokoma لَّا يَذُوقُونَ فِيهَا بَرۡدًا وَلَا شَرَابًا ٢٤Hawatakula humo chochote kitakachozizimisha joto la moto kwao إِلَّا حَمِيمًا وَغَسَّاقًا ٢٥Wala kinywaji kitakachowaondolea kiu yao. Isipokuwa maji moto na usaha wa watu wa motoni جَزَآءً وِفَاقًا ٢٦Watakuwa wanalipwa kwa hilo malipo ya sawa yanayolingana na vitendo vyao walivyovitenda duniani إِنَّهُمۡ كَانُواْ لَا يَرۡجُونَ حِسَابًا ٢٧Hakika wao walikuwa hawaiyogopi Siku ya Hesabu, na kwa hivyo hawakujitayarisha nayo kwa kufanya matendo ya kuwafaa وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا كِذَّابًا ٢٨Na waliyakanusha waziwazi yaliyoletwa na Mitume وَكُلَّ شَيۡءٍ أَحۡصَيۡنَٰهُ كِتَٰبًا ٢٩Na kila kitu Tulikijua na Tukakiandika katika Ubao uliohifadhiwa (Al-Lawḥ Al-Maḥfūd) فَذُوقُواْ فَلَن نَّزِيدَكُمۡ إِلَّا عَذَابًا ٣٠Basi Onjeni, enyi makafiri, hayo yakiwa ni malipo ya vitendo vyenu, Hatutawazidishia isipokuwa adhabu juu ya adhabu yenu إِنَّ لِلۡمُتَّقِينَ مَفَازًا ٣١Hakika kwa wale ambao wanamuogopa Mola wao na huku wanatenda mema kuna kufaulu kwa kuingia Peponi حَدَآئِقَ وَأَعۡنَٰبًا ٣٢Hakika watapata Mabustani makubwa na zabibu وَكَوَاعِبَ أَتۡرَابًا ٣٣Na watapata wanawake wenye umri mdogo, wenye vifua vilivyojaza, marika na waume zao وَكَأۡسًا دِهَاقًا ٣٤Na watapata glasi zlizojaa pombe لَّا يَسۡمَعُونَ فِيهَا لَغۡوًا وَلَا كِذَّٰبًا ٣٥Hawatasikia katika Pepo hiyo maneno ya upotofu wala kudanganyana جَزَآءً مِّن رَّبِّكَ عَطَآءً حِسَابًا ٣٦Watayapata yote hayo yakiwa ni malipo na zawadi na kipewa kingi cha kuwatosha kutoka kwa Mwenyezi Mungu رَّبِّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا ٱلرَّحۡمَٰنِۖ لَا يَمۡلِكُونَ مِنۡهُ خِطَابًا ٣٧Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati ya hizo, Mwenye kuwarehemu duniani na Akhera. Hawataweza kumuomba isipokuwa kile walichopewa ruhusa kumuomba يَوۡمَ يَقُومُ ٱلرُّوحُ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ صَفًّاۖ لَّا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنۡ أَذِنَ لَهُ ٱلرَّحۡمَٰنُ وَقَالَ صَوَابًا ٣٨Siku atakaposimama Jibrili na Malaika wengine hali ya kujipanga mlolongo. Hawatamuombea isipokuwa yule aliyetolewa ruhusa na Mwingi wa Rehema ya kuombewa na akasema maneno ya haki na ya sawa ذَٰلِكَ ٱلۡيَوۡمُ ٱلۡحَقُّۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ مَـَٔابًا ٣٩Hiyo ndiyo siku ya haki isiyokuwa na shaka kuja kwake. Kwa hivyo, yule atakaye kuokoka na vituko vya Siku hiyo, na ajifanyie njia ya marejeo kwa Mola wake kutenda vitendo vyema إِنَّآ أَنذَرۡنَٰكُمۡ عَذَابًا قَرِيبًا يَوۡمَ يَنظُرُ ٱلۡمَرۡءُ مَا قَدَّمَتۡ يَدَاهُ وَيَقُولُ ٱلۡكَافِرُ يَٰلَيۡتَنِي كُنتُ تُرَٰبَۢا ٤٠Sisi Tunawaonya nyinyi adhabu ya Siku ya mwisho iliyo karibu. Siku ambayo atayaona kila mtu aliyoyatenda katika kheri au aliyoyachuma miongoni mwa madhambi. Na kafiri atasema, kwa kitisho cha Hesabu, «Laiti mimi nilikuwa mchanga na sikufufuliwa.»