بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
عَمَّ يَتَسَآءَلُونَ ١WANAULIZANA nini عَنِ ٱلنَّبَإِ ٱلۡعَظِيمِ ٢Ile khabari kuu ٱلَّذِي هُمۡ فِيهِ مُخۡتَلِفُونَ ٣Ambayo kwayo wanakhitalifiana كـَلَّا سَيَعۡلَمُونَ ٤La! Karibu watakuja jua ثُمَّ كـَلَّا سَيَعۡلَمُونَ ٥Tena la! Karibu watakuja jua أَلَمۡ نَجۡعَلِ ٱلۡأَرۡضَ مِهَٰدًا ٦Kwani hatukuifanya ardhi kama tandiko وَٱلۡجِبَالَ أَوۡتَادًا ٧Na milima kama vigingi وَخَلَقۡنَٰكُمۡ أَزۡوَٰجًا ٨Na tukakuumbeni kwa jozi وَجَعَلۡنَا نَوۡمَكُمۡ سُبَاتًا ٩Na tukakufanya kulala kwenu ni mapumziko وَجَعَلۡنَا ٱلَّيۡلَ لِبَاسًا ١٠Na tukaufanya usiku ni nguo وَجَعَلۡنَا ٱلنَّهَارَ مَعَاشًا ١١Na tukaufanya mchana ni wa kuchumia maisha وَبَنَيۡنَا فَوۡقَكُمۡ سَبۡعًا شِدَادًا ١٢Na tukajenga juu yenu saba zenye nguvu وَجَعَلۡنَا سِرَاجًا وَهَّاجًا ١٣Na tukaifanya taa yenye mwanga na joto وَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلۡمُعۡصِرَٰتِ مَآءً ثَجَّاجًا ١٤Na tukateremsha maji yanayo anguka kwa kasi kutoka mawinguni لِّنُخۡرِجَ بِهِۦ حَبًّا وَنَبَاتًا ١٥Ili tutoe kwayo nafaka na mimea وَجَنَّٰتٍ أَلۡفَافًا ١٦Na mabustani yenye miti iliyo kamatana إِنَّ يَوۡمَ ٱلۡفَصۡلِ كَانَ مِيقَٰتًا ١٧Hakika siku ya uamuzi imewekewa wakati wake يَوۡمَ يُنفَخُ فِي ٱلصُّورِ فَتَأۡتُونَ أَفۡوَاجًا ١٨Siku litapo pulizwa barugumu, nanyi mtakuja kwa makundi وَفُتِحَتِ ٱلسَّمَآءُ فَكَانَتۡ أَبۡوَٰبًا ١٩Na mbingu zitafunguliwa, ziwe milango وَسُيِّرَتِ ٱلۡجِبَالُ فَكَانَتۡ سَرَابًا ٢٠Na milima itaondolewa na itakuwa kama sarabi إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتۡ مِرۡصَادًا ٢١Hakika Jahannamu inangojea لِّلطَّٰغِينَ مَـَٔابًا ٢٢Kwa walio asi ndio makaazi yao لَّٰبِثِينَ فِيهَآ أَحۡقَابًا ٢٣Wakae humo karne baada ya karne لَّا يَذُوقُونَ فِيهَا بَرۡدًا وَلَا شَرَابًا ٢٤Hawataonja humo chochote kibaridi wala kinywaji إِلَّا حَمِيمًا وَغَسَّاقًا ٢٥Ila maji yamoto sana na usaha جَزَآءً وِفَاقًا ٢٦Ndio jaza muwafaka إِنَّهُمۡ كَانُواْ لَا يَرۡجُونَ حِسَابًا ٢٧Hakika hao hawakuwa wakitaraji kuwa kuna hisabu وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا كِذَّابًا ٢٨Na wakikanusha Aya zetu kwa nguvu وَكُلَّ شَيۡءٍ أَحۡصَيۡنَٰهُ كِتَٰبًا ٢٩Na kila kitu Sisi tumekidhibiti kwa kukiandika فَذُوقُواْ فَلَن نَّزِيدَكُمۡ إِلَّا عَذَابًا ٣٠Basi onjeni! Nasi hatutakuzidishieni ila adhabu إِنَّ لِلۡمُتَّقِينَ مَفَازًا ٣١Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu حَدَآئِقَ وَأَعۡنَٰبًا ٣٢Mabustani na mizabibu وَكَوَاعِبَ أَتۡرَابًا ٣٣Na wake walio lingana nao وَكَأۡسًا دِهَاقًا ٣٤Na bilauri zilizo jaa لَّا يَسۡمَعُونَ فِيهَا لَغۡوًا وَلَا كِذَّٰبًا ٣٥Hawatasikia humo upuuzi wala uwongo جَزَآءً مِّن رَّبِّكَ عَطَآءً حِسَابًا ٣٦Malipo kutoka kwa Mola wako Mlezi, kipawa cha kutosha رَّبِّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا ٱلرَّحۡمَٰنِۖ لَا يَمۡلِكُونَ مِنۡهُ خِطَابًا ٣٧Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, Arrahman, Mwingi wa rehema; hawamiliki usemi mbele yake يَوۡمَ يَقُومُ ٱلرُّوحُ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ صَفًّاۖ لَّا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنۡ أَذِنَ لَهُ ٱلرَّحۡمَٰنُ وَقَالَ صَوَابًا ٣٨Siku atakapo simama Roho na Malaika kwa safu. Hawatasema ila Mwingi wa rehema aliye mruhusu, na atasema yaliyo sawa tu ذَٰلِكَ ٱلۡيَوۡمُ ٱلۡحَقُّۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ مَـَٔابًا ٣٩Hiyo ndiyo Siku ya haki. Basi anaye taka na ashike njia arejee kwa Mola wake Mlezi إِنَّآ أَنذَرۡنَٰكُمۡ عَذَابًا قَرِيبًا يَوۡمَ يَنظُرُ ٱلۡمَرۡءُ مَا قَدَّمَتۡ يَدَاهُ وَيَقُولُ ٱلۡكَافِرُ يَٰلَيۡتَنِي كُنتُ تُرَٰبَۢا ٤٠Hakika tumekuhadharisheni adhabu iliyo karibu kufika; Siku ambayo mtu atakapo ona yaliyo tangulizwa na mikono yake; na kafiri atasema: Laiti ningeli kuwa udongo