بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
وَٱلسَّمَآءِ وَٱلطَّارِقِ ١Mwenyezi Mungu Anaapa kwa mbingu na nyota yenye kuchomoza usiku وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلطَّارِقُ ٢Na ni lipi lilokujulisha ni ukubwa gani wa nyota hiyo ٱلنَّجۡمُ ٱلثَّاقِبُ ٣Hiyo ni nyota ing’arao na kuzagaa إِن كُلُّ نَفۡسٍ لَّمَّا عَلَيۡهَا حَافِظٌ ٤Hakuna nafsi yoyote isipokuwa amewakilishwa kwayo Malaika mwenye kuchunguza na kusjili amali zake ili ihesabiwe Siku ya Kiyama فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَٰنُ مِمَّ خُلِقَ ٥Basi aangalie binadamu mwenye kukanusha kufufuliwa ameumbwa kwa kitu gani? Ili ajue kuwa kurudisha umbo lake mara ya pili si vigumu kama kuumbwa mara ya kwanza خُلِقَ مِن مَّآءٍ دَافِقٍ ٦Aliumbwa kwa manii yenye kupenyeza ndani ya uzao kwa haraka يَخۡرُجُ مِنۢ بَيۡنِ ٱلصُّلۡبِ وَٱلتَّرَآئِبِ ٧Yatokayo kwenye mgongo wa mwnamume na kifua cha mwanamke إِنَّهُۥ عَلَىٰ رَجۡعِهِۦ لَقَادِرٌ ٨Hakika yule Aliyemuumba binadamu kwa maji haya ni muweza wa kumrudisha kwenye uhai baada ya kufa يَوۡمَ تُبۡلَى ٱلسَّرَآئِرُ ٩Siku zitakapofunuliwa wazi siri ziliofichwa na nafsi na kupambanuliwa njema na mbovu فَمَا لَهُۥ مِن قُوَّةٍ وَلَا نَاصِرٍ ١٠Binadamu hatakuwa na nguvu ya kuitetea nafsi yake wala hatakuwa na mtetezi wa kumwepushia adhabu ya Mwenyezi Mungu وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلرَّجۡعِ ١١Na Anaapa kwa mbingu yenye mvua ya kukaririka وَٱلۡأَرۡضِ ذَاتِ ٱلصَّدۡعِ ١٢Na ardhi yenye pasuko za kufanya mimea ichipuke إِنَّهُۥ لَقَوۡلٌ فَصۡلٌ ١٣Hakika Qur’ani ni neno lenye kupambanua baina ya haki na batili وَمَا هُوَ بِٱلۡهَزۡلِ ١٤Na si upuuzi. Haifai kiumbe kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Akifanya hivyo atakuwa amemshirikisha Mwenyezi Mungu إِنَّهُمۡ يَكِيدُونَ كَيۡدًا ١٥Hakika wenye kumkanusha Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na Qur’ani wanafanya vitimbi na mipango ili kuipinga haki na kuitilia nguvu batili وَأَكِيدُ كَيۡدًا ١٦Na Mimi nafanya vitimbi kuidhihirisha haki ingawa makafiri wanatukia.Usiwe na haraka nao, ewe Mtume, kutaka wateremshiwe adhabu فَمَهِّلِ ٱلۡكَٰفِرِينَ أَمۡهِلۡهُمۡ رُوَيۡدَۢا ١٧Wape muhula uwangojee muda mchache wala usiwafanyie haraka, utaona adhabu itakayowafikia, mateso na maangamivu