إِذَا زُلۡزِلَتِ ٱلۡأَرۡضُ زِلۡزَالَهَا ١Itakapotikiswa ardhi mtikiso wa nguvuوَأَخۡرَجَتِ ٱلۡأَرۡضُ أَثۡقَالَهَا ٢Na ikatoa vilivyomo ndani yake: wafu na makandiوَقَالَ ٱلۡإِنسَٰنُ مَا لَهَا ٣Na akauliza binadamu, kwa babaiko, «Imezukiwa na nini?»يَوۡمَئِذٍ تُحَدِّثُ أَخۡبَارَهَا ٤Siku ya Kiyama ardhi itatoa habari ya mambo iliyofanyiwa ya uzuri na ubayaبِأَنَّ رَبَّكَ أَوۡحَىٰ لَهَا ٥kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Ameiamuru itoe habari ya mambo iliyofanyiwaيَوۡمَئِذٍ يَصۡدُرُ ٱلنَّاسُ أَشۡتَاتًا لِّيُرَوۡاْ أَعۡمَٰلَهُمۡ ٦Siku hiyo wataondoka kutoka kwenye kisimamo cha Hesabu wakiwa makundi, ili Mwenyezi Mungu Awaoneshe waliyoyatenda, mazuri na mabaya, na Awalipe kwayoفَمَن يَعۡمَلۡ مِثۡقَالَ ذَرَّةٍ خَيۡرًا يَرَهُۥ ٧Yoyote mwenye kufanya jema wezani wa chungu mdogo atayaona malipo yake Akheraوَمَن يَعۡمَلۡ مِثۡقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُۥ ٨Na yoyote mwenye kufanya baya wezani wa chungu mdogo atayaona malipo yake Akhera