ملة الإسلام

السورة 100 · 11 آية · Abdullah Muhammad Abu Bakr

سورة العاديات باللغة السواحلية

السورة بالعربية مع التفسير استمع إلى سورة العاديات (1,283 قارئاً)
مكيةسورة العاديات١١ آية

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلۡعَٰدِيَٰتِ ضَبۡحًا ١Mwenyezi Mungu Anaapa kwa farasi wenye kwenda shoti katika njia Yake kumkabili adui, wakitoa sauti kwa kasi ya kukimbia. Haifai kwa kiumbe kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni ushirikina فَٱلۡمُورِيَٰتِ قَدۡحًا ٢Na wenye kutoa cheche za moto kwa kwato zao ngumu wanapokimbia kwa kasi فَٱلۡمُغِيرَٰتِ صُبۡحًا ٣Wenye kushambulia maadui kipindi cha asubuhi فَأَثَرۡنَ بِهِۦ نَقۡعًا ٤Wakarusha vumbi kwa mbio zao فَوَسَطۡنَ بِهِۦ جَمۡعًا ٥Wakautia kati, kwa kuuzunguka kwa vipando vyao, mkusanyiko wa maadui إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ لِرَبِّهِۦ لَكَنُودٌ ٦Hakika binadamu ni mkanushaji sana neema za Mola wake وَإِنَّهُۥ عَلَىٰ ذَٰلِكَ لَشَهِيدٌ ٧Na yeye anakubali ukanushaji wake وَإِنَّهُۥ لِحُبِّ ٱلۡخَيۡرِ لَشَدِيدٌ ٨Na yeye ana pupa sana la mali ۞ أَفَلَا يَعۡلَمُ إِذَا بُعۡثِرَ مَا فِي ٱلۡقُبُورِ ٩Kwani binadamu hajui linalomngojea mbele yake, pindi Mwenyezi Mungu Atakapowatoa wafu makaburini waende kuhesabiwa na kulipwa وَحُصِّلَ مَا فِي ٱلصُّدُورِ ١٠Na (kwani yeye hajui) yakatolewa yaliyo ndani ya vifua: mema au maovu إِنَّ رَبَّهُم بِهِمۡ يَوۡمَئِذٍ لَّخَبِيرُۢ ١١Hakika Mola wao kwao na kwa amali zao, Siku Hiyo, ni Mtambuzi; hakuna chenye kufichamana Kwake

الترجمة: Abdullah Muhammad Abu Bakr.