ملة الإسلام

السورة 85 · 22 آية · Ali Muhsin Al Barwani

سورة البروج باللغة السواحلية

السورة بالعربية مع التفسير استمع إلى سورة البروج (1,332 قارئاً)
مكيةسورة البروج٢٢ آية

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلۡبُرُوجِ ١Naapa kwa mbingu yenye Buruji وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡمَوۡعُودِ ٢Na kwa siku iliyo ahidiwa وَشَاهِدٍ وَمَشۡهُودٍ ٣Na kwa shahidi na kinacho shuhudiwa قُتِلَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡأُخۡدُودِ ٤Wameangamizwa watu wa makhandaki ٱلنَّارِ ذَاتِ ٱلۡوَقُودِ ٥Yenye moto wenye kuni nyingi إِذۡ هُمۡ عَلَيۡهَا قُعُودٌ ٦Walipo kuwa wamekaa hapo وَهُمۡ عَلَىٰ مَا يَفۡعَلُونَ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ شُهُودٌ ٧Na wao ni mashahidi wa yale waliyo kuwa wakiwafanyia Waumini وَمَا نَقَمُواْ مِنۡهُمۡ إِلَّآ أَن يُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَمِيدِ ٨Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٍ شَهِيدٌ ٩Ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi; na Mwenyezi Mungu ni shaahidi wa kila kitu إِنَّ ٱلَّذِينَ فَتَنُواْ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ ثُمَّ لَمۡ يَتُوبُواْ فَلَهُمۡ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمۡ عَذَابُ ٱلۡحَرِيقِ ١٠Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَهُمۡ جَنَّٰتٌ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۚ ذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡكَبِيرُ ١١Hakika walio amini na wakatenda mema watapata Bustani zenye mito ipitayo kati yake. Huko ndiko kufuzu kukubwa إِنَّ بَطۡشَ رَبِّكَ لَشَدِيدٌ ١٢Hakika kutesa kwa Mola wako Mlezi ni kukali إِنَّهُۥ هُوَ يُبۡدِئُ وَيُعِيدُ ١٣Yeye ndiye anaye anzisha na ndiye anaye rejeza tena وَهُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلۡوَدُودُ ١٤Naye ni Mwenye kusamehe, Mwenye mapenzi ذُو ٱلۡعَرۡشِ ٱلۡمَجِيدُ ١٥Mwenye Kiti cha Enzi, Mtukufu فَعَّالٌ لِّمَا يُرِيدُ ١٦Atendaye ayatakayo هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلۡجُنُودِ ١٧Je! Zimekuwasilia khabari za majeshi فِرۡعَوۡنَ وَثَمُودَ ١٨Ya Firauni na Thamudi بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فِي تَكۡذِيبٍ ١٩Lakini walio kufuru wamo katika kukadhibisha وَٱللَّهُ مِن وَرَآئِهِم مُّحِيطُۢ ٢٠Na Mwenyezi Mungu nyuma yao amewazunguka بَلۡ هُوَ قُرۡءَانٌ مَّجِيدٌ ٢١Bali hii ni Qur'ani tukufu فِي لَوۡحٍ مَّحۡفُوظِۭ ٢٢Katika Ubao Ulio Hifadhiwa

الترجمة: Ali Muhsin Al Barwani.