ملة الإسلام

السورة 70 · 44 آية · Ali Muhsin Al Barwani

سورة المعارج باللغة السواحلية

السورة بالعربية مع التفسير استمع إلى سورة المعارج (1,289 قارئاً)
مكيةسورة المعارج٤٤ آية

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

سَأَلَ سَآئِلُۢ بِعَذَابٍ وَاقِعٍ ١Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayo tokea لِّلۡكَٰفِرِينَ لَيۡسَ لَهُۥ دَافِعٌ ٢Kwa makafiri - ambayo hapana awezaye kuizuia مِّنَ ٱللَّهِ ذِي ٱلۡمَعَارِجِ ٣Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu za daraja تَعۡرُجُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ وَٱلرُّوحُ إِلَيۡهِ فِي يَوۡمٍ كَانَ مِقۡدَارُهُۥ خَمۡسِينَ أَلۡفَ سَنَةٍ ٤Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo kadiri yake ni miaka khamsini elfu فَٱصۡبِرۡ صَبۡرًا جَمِيلًا ٥Basi subiri kwa subira njema إِنَّهُمۡ يَرَوۡنَهُۥ بَعِيدًا ٦Hakika wao wanaiona iko mbali وَنَرَىٰهُ قَرِيبًا ٧Na Sisi tunaiona iko karibu يَوۡمَ تَكُونُ ٱلسَّمَآءُ كَٱلۡمُهۡلِ ٨Siku ambayo mbingu zitakapo kuwa kama maadeni iliyo yayushwa وَتَكُونُ ٱلۡجِبَالُ كَٱلۡعِهۡنِ ٩Na milima itakuwa kama sufi وَلَا يَسۡـَٔلُ حَمِيمٌ حَمِيمًا ١٠Wala jamaa hatamuuliza jamaa yake يُبَصَّرُونَهُمۡۚ يَوَدُّ ٱلۡمُجۡرِمُ لَوۡ يَفۡتَدِي مِنۡ عَذَابِ يَوۡمِئِذِۭ بِبَنِيهِ ١١Ijapo kuwa wataonyeshwa waonane. Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe وَصَٰحِبَتِهِۦ وَأَخِيهِ ١٢Na mkewe, na nduguye وَفَصِيلَتِهِ ٱلَّتِي تُـٔۡوِيهِ ١٣Na jamaa zake walio kuwa wakimkimu وَمَن فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعًا ثُمَّ يُنجِيهِ ١٤Na wote waliomo duniani, kisha aokoke yeye كـَلَّآۖ إِنَّهَا لَظَىٰ ١٥La, hasha! Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa نَزَّاعَةً لِّلشَّوَىٰ ١٦Unao babua ngozi ya kichwa تَدۡعُواْ مَنۡ أَدۡبَرَ وَتَوَلَّىٰ ١٧Utamwita kila aliye geuza mgongo na akageuka وَجَمَعَ فَأَوۡعَىٰٓ ١٨Na akakusanya mali, kisha akayahifadhi ۞ إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ خُلِقَ هَلُوعًا ١٩Hakika mtu ameumbwa na papara إِذَا مَسَّهُ ٱلشَّرُّ جَزُوعًا ٢٠Inapo mgusa shari hupapatika وَإِذَا مَسَّهُ ٱلۡخَيۡرُ مَنُوعًا ٢١Na inapo mgusa kheri huizuilia إِلَّا ٱلۡمُصَلِّينَ ٢٢Isipo kuwa wanao sali ٱلَّذِينَ هُمۡ عَلَىٰ صَلَاتِهِمۡ دَآئِمُونَ ٢٣Ambao wanadumisha Sala zao وَٱلَّذِينَ فِيٓ أَمۡوَٰلِهِمۡ حَقٌّ مَّعۡلُومٌ ٢٤Na ambao katika mali yao iko haki maalumu لِّلسَّآئِلِ وَٱلۡمَحۡرُومِ ٢٥Kwa mwenye kuomba na anaye jizuilia kuomba وَٱلَّذِينَ يُصَدِّقُونَ بِيَوۡمِ ٱلدِّينِ ٢٦Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo وَٱلَّذِينَ هُم مِّنۡ عَذَابِ رَبِّهِم مُّشۡفِقُونَ ٢٧Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi إِنَّ عَذَابَ رَبِّهِمۡ غَيۡرُ مَأۡمُونٍ ٢٨Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika nayo وَٱلَّذِينَ هُمۡ لِفُرُوجِهِمۡ حَٰفِظُونَ ٢٩Na ambao wanahifadhi tupu zao إِلَّا عَلَىٰٓ أَزۡوَٰجِهِمۡ أَوۡ مَا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُهُمۡ فَإِنَّهُمۡ غَيۡرُ مَلُومِينَ ٣٠Isipo kuwa kwa wake zao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi فَمَنِ ٱبۡتَغَىٰ وَرَآءَ ذَٰلِكَ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡعَادُونَ ٣١Lakini wanao taka kinyume ya haya, basi hao ndio wanao ruka mipaka وَٱلَّذِينَ هُمۡ لِأَمَٰنَٰتِهِمۡ وَعَهۡدِهِمۡ رَٰعُونَ ٣٢Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao وَٱلَّذِينَ هُم بِشَهَٰدَٰتِهِمۡ قَآئِمُونَ ٣٣Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao وَٱلَّذِينَ هُمۡ عَلَىٰ صَلَاتِهِمۡ يُحَافِظُونَ ٣٤Na ambao wanazihifadhi Sala zao أُوْلَٰٓئِكَ فِي جَنَّٰتٍ مُّكۡرَمُونَ ٣٥Hao ndio watakao hishimiwa Peponi فَمَالِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ قِبَلَكَ مُهۡطِعِينَ ٣٦Wana nini wale walio kufuru wanakutumbulia macho tu عَنِ ٱلۡيَمِينِ وَعَنِ ٱلشِّمَالِ عِزِينَ ٣٧Makundi kwa makundi upande wa kulia na upande wa kushoto أَيَطۡمَعُ كُلُّ ٱمۡرِيٍٕ مِّنۡهُمۡ أَن يُدۡخَلَ جَنَّةَ نَعِيمٍ ٣٨Kwani kila mmoja wao anatumai kuingizwa katika Pepo ya neema كـَلَّآۖ إِنَّا خَلَقۡنَٰهُم مِّمَّا يَعۡلَمُونَ ٣٩La, hasha! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na wanacho kijua فَلَآ أُقۡسِمُ بِرَبِّ ٱلۡمَشَٰرِقِ وَٱلۡمَغَٰرِبِ إِنَّا لَقَٰدِرُونَ ٤٠Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mashariki zote na magharibi zote kwamba Sisi tunaweza عَلَىٰٓ أَن نُّبَدِّلَ خَيۡرًا مِّنۡهُمۡ وَمَا نَحۡنُ بِمَسۡبُوقِينَ ٤١Kuwabadili kwa walio bora kuliko wao; na Sisi hatushindwi فَذَرۡهُمۡ يَخُوضُواْ وَيَلۡعَبُواْ حَتَّىٰ يُلَٰقُواْ يَوۡمَهُمُ ٱلَّذِي يُوعَدُونَ ٤٢Basi waache wapige porojo na wacheze, mpaka wakutane na siku yao wanayo ahidiwa يَوۡمَ يَخۡرُجُونَ مِنَ ٱلۡأَجۡدَاثِ سِرَاعًا كَأَنَّهُمۡ إِلَىٰ نُصُبٍ يُوفِضُونَ ٤٣Siku watakapotoka makaburini kwa upesi kama kwamba wanakimbilia mfundo خَٰشِعَةً أَبۡصَٰرُهُمۡ تَرۡهَقُهُمۡ ذِلَّةٌۚ ذَٰلِكَ ٱلۡيَوۡمُ ٱلَّذِي كَانُواْ يُوعَدُونَ ٤٤Macho yao yatainama, fedheha itawafunika. Hiyo ndiyo Siku waliyo kuwa wakiahidiwa

الترجمة: Ali Muhsin Al Barwani.