ملة الإسلام

السورة 69 · 52 آية · Ali Muhsin Al Barwani

سورة الحاقة باللغة السواحلية

السورة بالعربية مع التفسير استمع إلى سورة الحاقة (1,346 قارئاً)
مكيةسورة الحاقة٥٢ آية

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

ٱلۡحَآقَّةُ ١Tukio la haki مَا ٱلۡحَآقَّةُ ٢Nini hilo Tukio la haki وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡحَآقَّةُ ٣Na nini kitakujuulisha nini hilo Tukio la haki كَذَّبَتۡ ثَمُودُ وَعَادُۢ بِٱلۡقَارِعَةِ ٤Thamudi na A'di waliukadhibisha Msiba unao situsha فَأَمَّا ثَمُودُ فَأُهۡلِكُواْ بِٱلطَّاغِيَةِ ٥Basi Thamudi waliangamizwa kwa balaa kubwa mno وَأَمَّا عَادٌ فَأُهۡلِكُواْ بِرِيحٍ صَرۡصَرٍ عَاتِيَةٍ ٦Na ama A'di waliangamizwa kwa upepo mkali usio zuilika سَخَّرَهَا عَلَيۡهِمۡ سَبۡعَ لَيَالٍ وَثَمَٰنِيَةَ أَيَّامٍ حُسُومًاۖ فَتَرَى ٱلۡقَوۡمَ فِيهَا صَرۡعَىٰ كَأَنَّهُمۡ أَعۡجَازُ نَخۡلٍ خَاوِيَةٍ ٧Alio wapelekea masiku saba, na siku nane, mfululizo bila ya kusita. Utaona watu wamepinduka kama kwamba ni magongo ya mitende yalio wazi ndani فَهَلۡ تَرَىٰ لَهُم مِّنۢ بَاقِيَةٍ ٨Basi je! Unamwona mmoja wao aliye baki وَجَآءَ فِرۡعَوۡنُ وَمَن قَبۡلَهُۥ وَٱلۡمُؤۡتَفِكَٰتُ بِٱلۡخَاطِئَةِ ٩Na Firauni na walio mtangulia, na miji iliyo pinduliwa chini juu, walileta khatia فَعَصَوۡاْ رَسُولَ رَبِّهِمۡ فَأَخَذَهُمۡ أَخۡذَةً رَّابِيَةً ١٠Wakamuasi Mtume wa Mola wao Mlezi, ndipo Yeye Mola akawakamata kwa mkamato ulio zidi nguvu إِنَّا لَمَّا طَغَا ٱلۡمَآءُ حَمَلۡنَٰكُمۡ فِي ٱلۡجَارِيَةِ ١١Maji yalipo furika Sisi tulikupandisheni katika safina لِنَجۡعَلَهَا لَكُمۡ تَذۡكِرَةً وَتَعِيَهَآ أُذُنٌ وَٰعِيَةٌ ١٢Ili tuyafanye hayo kuwa ni waadhi kwenu na kila sikio linalo sikia liyahifadhi فَإِذَا نُفِخَ فِي ٱلصُّورِ نَفۡخَةٌ وَٰحِدَةٌ ١٣Na litapo pulizwa barugumu mpulizo mmoja tu وَحُمِلَتِ ٱلۡأَرۡضُ وَٱلۡجِبَالُ فَدُكَّتَا دَكَّةً وَٰحِدَةً ١٤Na ardhi na milima ikaondolewa, na ikavunjwa kwa mvunjo mmoja فَيَوۡمَئِذٍ وَقَعَتِ ٱلۡوَاقِعَةُ ١٥Siku hiyo ndio Tukio litatukia وَٱنشَقَّتِ ٱلسَّمَآءُ فَهِيَ يَوۡمَئِذٍ وَاهِيَةٌ ١٦Na mbingu zitapasuka, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu kabisa وَٱلۡمَلَكُ عَلَىٰٓ أَرۡجَآئِهَاۚ وَيَحۡمِلُ عَرۡشَ رَبِّكَ فَوۡقَهُمۡ يَوۡمَئِذٍ ثَمَٰنِيَةٌ ١٧Na Malaika watakuwa pembezoni mwa mbingu; na wanane juu ya hawa watakuwa wamebeba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi يَوۡمَئِذٍ تُعۡرَضُونَ لَا تَخۡفَىٰ مِنكُمۡ خَافِيَةٌ ١٨Siku hiyo mtahudhurishwa - haitafichika siri yoyote yenu فَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ فَيَقُولُ هَآؤُمُ ٱقۡرَءُواْ كِتَٰبِيَهۡ ١٩Basi ama atakaye pewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema: Haya someni kitabu changu إِنِّي ظَنَنتُ أَنِّي مُلَٰقٍ حِسَابِيَهۡ ٢٠Hakika nalijua ya kuwa nitapokea hisabu yangu فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ ٢١Basi yeye atakuwa katika maisha ya kupendeza فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٍ ٢٢Katika Bustani ya juu قُطُوفُهَا دَانِيَةٌ ٢٣Matunda yake yakaribu كُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ هَنِيٓـَٔۢا بِمَآ أَسۡلَفۡتُمۡ فِي ٱلۡأَيَّامِ ٱلۡخَالِيَةِ ٢٤Waambiwe: Kuleni na mnywe kwa furaha kwa sababu ya mlivyo tanguliza katika siku zilizo pita وَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ بِشِمَالِهِۦ فَيَقُولُ يَٰلَيۡتَنِي لَمۡ أُوتَ كِتَٰبِيَهۡ ٢٥Na ama atakaye pewa kitabu chake katika mkono wake wa kushoto, basi yeye atasema: Laiti nisingeli pewa kitabu changu وَلَمۡ أَدۡرِ مَا حِسَابِيَهۡ ٢٦Wala nisingeli jua nini hisabu yangu يَٰلَيۡتَهَا كَانَتِ ٱلۡقَاضِيَةَ ٢٧Laiti mauti ndiyo yangeli kuwa ya kunimaliza kabisa مَآ أَغۡنَىٰ عَنِّي مَالِيَهۡۜ ٢٨Mali yangu hayakunifaa kitu هَلَكَ عَنِّي سُلۡطَٰنِيَهۡ ٢٩Madaraka yangu yamenipotea خُذُوهُ فَغُلُّوهُ ٣٠(Pasemwe): Mshikeni! Mtieni pingu ثُمَّ ٱلۡجَحِيمَ صَلُّوهُ ٣١Kisha mtupeni Motoni ثُمَّ فِي سِلۡسِلَةٍ ذَرۡعُهَا سَبۡعُونَ ذِرَاعًا فَٱسۡلُكُوهُ ٣٢Tena mtatizeni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabiini إِنَّهُۥ كَانَ لَا يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ ٱلۡعَظِيمِ ٣٣Kwani huyo hakika alikuwa hamuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ ٣٤Wala hahimizi kulisha masikini فَلَيۡسَ لَهُ ٱلۡيَوۡمَ هَٰهُنَا حَمِيمٌ ٣٥Basi leo hapa hana jamaa wa kumwonea uchungu وَلَا طَعَامٌ إِلَّا مِنۡ غِسۡلِينٍ ٣٦Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni لَّا يَأۡكُلُهُۥٓ إِلَّا ٱلۡخَٰطِـُٔونَ ٣٧Chakula hicho hawakili ila wakosefu فَلَآ أُقۡسِمُ بِمَا تُبۡصِرُونَ ٣٨Basi naapa kwa mnavyo viona وَمَا لَا تُبۡصِرُونَ ٣٩Na msivyo viona إِنَّهُۥ لَقَوۡلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ ٤٠Kwa hakika hii ni kauli iliyo letwa na Mjumbe mwenye hishima وَمَا هُوَ بِقَوۡلِ شَاعِرٍۚ قَلِيلًا مَّا تُؤۡمِنُونَ ٤١Wala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machache sana mnayo yaamini وَلَا بِقَوۡلِ كَاهِنٍۚ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ ٤٢Wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayo yakumbuka تَنزِيلٌ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ٤٣Ni uteremsho utokao kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote وَلَوۡ تَقَوَّلَ عَلَيۡنَا بَعۡضَ ٱلۡأَقَاوِيلِ ٤٤Na lau kama angeli tuzulia baadhi ya maneno tu لَأَخَذۡنَا مِنۡهُ بِٱلۡيَمِينِ ٤٥Bila ya shaka tungeli mshika kwa mkono wa kulia ثُمَّ لَقَطَعۡنَا مِنۡهُ ٱلۡوَتِينَ ٤٦Kisha kwa hakika tungeli mkata mshipa mkubwa wa moyo فَمَا مِنكُم مِّنۡ أَحَدٍ عَنۡهُ حَٰجِزِينَ ٤٧Na hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeli weza kutuzuia وَإِنَّهُۥ لَتَذۡكِرَةٌ لِّلۡمُتَّقِينَ ٤٨Kwa hakika hii ni mawaidha kwa wachamngu وَإِنَّا لَنَعۡلَمُ أَنَّ مِنكُم مُّكَذِّبِينَ ٤٩Na hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba miongoni mwenu wapo wanao kadhibisha وَإِنَّهُۥ لَحَسۡرَةٌ عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ ٥٠Na hakika bila ya shaka itakuwa ni majuto kwa wanao kataa وَإِنَّهُۥ لَحَقُّ ٱلۡيَقِينِ ٥١Na hakika hii bila ya shaka ni haki ya yakini فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ ٥٢Basi litakase jina la Mola wako Mlezi Mtukufu

الترجمة: Ali Muhsin Al Barwani.