ملة الإسلام

السورة 77 · 50 آية · Ali Muhsin Al Barwani

سورة المرسلات باللغة السواحلية

السورة بالعربية مع التفسير استمع إلى سورة المرسلات (1,226 قارئاً)
مكيةسورة المرسلات٥٠ آية

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلۡمُرۡسَلَٰتِ عُرۡفًا ١Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole فَٱلۡعَٰصِفَٰتِ عَصۡفًا ٢Na zinazo vuma kwa kasi وَٱلنَّٰشِرَٰتِ نَشۡرًا ٣Na zikaeneza maeneo yote فَٱلۡفَٰرِقَٰتِ فَرۡقًا ٤Na zinazo farikisha zikatawanya فَٱلۡمُلۡقِيَٰتِ ذِكۡرًا ٥Na zinazo peleka mawaidha عُذۡرًا أَوۡ نُذۡرًا ٦Kwa kuudhuru au kuonya إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَوَٰقِعٌ ٧Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka yatakuwa فَإِذَا ٱلنُّجُومُ طُمِسَتۡ ٨Wakati nyota zitakapo futwa وَإِذَا ٱلسَّمَآءُ فُرِجَتۡ ٩Na mbingu zitakapo pasuliwa وَإِذَا ٱلۡجِبَالُ نُسِفَتۡ ١٠Na milima itakapo peperushwa وَإِذَا ٱلرُّسُلُ أُقِّتَتۡ ١١Na Mitume watakapo wekewa wakati wao لِأَيِّ يَوۡمٍ أُجِّلَتۡ ١٢Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo لِيَوۡمِ ٱلۡفَصۡلِ ١٣Kwa siku ya kupambanua وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلۡفَصۡلِ ١٤Na nini kitakacho kujuulisha siku ya kupambanua ni nini وَيۡلٌ يَوۡمَئِذٍ لِّلۡمُكَذِّبِينَ ١٥Ole wao, siku hiyo hao wanao kanusha أَلَمۡ نُهۡلِكِ ٱلۡأَوَّلِينَ ١٦Kwani hatukuwaangamiza walio tangulia ثُمَّ نُتۡبِعُهُمُ ٱلۡأٓخِرِينَ ١٧Kisha tukawafuatilizia walio fuatia كَذَٰلِكَ نَفۡعَلُ بِٱلۡمُجۡرِمِينَ ١٨Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu وَيۡلٌ يَوۡمَئِذٍ لِّلۡمُكَذِّبِينَ ١٩Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha أَلَمۡ نَخۡلُقكُّم مِّن مَّآءٍ مَّهِينٍ ٢٠Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa فَجَعَلۡنَٰهُ فِي قَرَارٍ مَّكِينٍ ٢١Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti إِلَىٰ قَدَرٍ مَّعۡلُومٍ ٢٢Mpaka muda maalumu فَقَدَرۡنَا فَنِعۡمَ ٱلۡقَٰدِرُونَ ٢٣Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria وَيۡلٌ يَوۡمَئِذٍ لِّلۡمُكَذِّبِينَ ٢٤Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha أَلَمۡ نَجۡعَلِ ٱلۡأَرۡضَ كِفَاتًا ٢٥Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya أَحۡيَآءً وَأَمۡوَٰتًا ٢٦Walio hai na maiti وَجَعَلۡنَا فِيهَا رَوَٰسِيَ شَٰمِخَٰتٍ وَأَسۡقَيۡنَٰكُم مَّآءً فُرَاتًا ٢٧Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu وَيۡلٌ يَوۡمَئِذٍ لِّلۡمُكَذِّبِينَ ٢٨Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha ٱنطَلِقُوٓاْ إِلَىٰ مَا كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ ٢٩Nendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha ٱنطَلِقُوٓاْ إِلَىٰ ظِلٍّ ذِي ثَلَٰثِ شُعَبٍ ٣٠Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu لَّا ظَلِيلٍ وَلَا يُغۡنِي مِنَ ٱللَّهَبِ ٣١Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako إِنَّهَا تَرۡمِي بِشَرَرٍ كَٱلۡقَصۡرِ ٣٢Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba كَأَنَّهُۥ جِمَٰلَتٌ صُفۡرٌ ٣٣Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano وَيۡلٌ يَوۡمَئِذٍ لِّلۡمُكَذِّبِينَ ٣٤Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha هَٰذَا يَوۡمُ لَا يَنطِقُونَ ٣٥Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu وَلَا يُؤۡذَنُ لَهُمۡ فَيَعۡتَذِرُونَ ٣٦Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru وَيۡلٌ يَوۡمَئِذٍ لِّلۡمُكَذِّبِينَ ٣٧Ole wao siku hiyo hao walio kanusha هَٰذَا يَوۡمُ ٱلۡفَصۡلِۖ جَمَعۡنَٰكُمۡ وَٱلۡأَوَّلِينَ ٣٨Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio tangulia فَإِن كَانَ لَكُمۡ كَيۡدٌ فَكِيدُونِ ٣٩Ikiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi وَيۡلٌ يَوۡمَئِذٍ لِّلۡمُكَذِّبِينَ ٤٠Ole wao siku hiyo hao walio kanusha إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي ظِلَٰلٍ وَعُيُونٍ ٤١Hakika wachamngu watakuwa katika vivuli na chemchem وَفَوَٰكِهَ مِمَّا يَشۡتَهُونَ ٤٢Na matunda wanayo yapenda كُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ هَنِيٓـَٔۢا بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ ٤٣Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ ٤٤Hakika ndio kama hivyo tunavyo walipa watendao mema وَيۡلٌ يَوۡمَئِذٍ لِّلۡمُكَذِّبِينَ ٤٥Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha كُلُواْ وَتَمَتَّعُواْ قَلِيلًا إِنَّكُم مُّجۡرِمُونَ ٤٦Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu وَيۡلٌ يَوۡمَئِذٍ لِّلۡمُكَذِّبِينَ ٤٧Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱرۡكَعُواْ لَا يَرۡكَعُونَ ٤٨Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami وَيۡلٌ يَوۡمَئِذٍ لِّلۡمُكَذِّبِينَ ٤٩Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha فَبِأَيِّ حَدِيثِۭ بَعۡدَهُۥ يُؤۡمِنُونَ ٥٠Basi maneno gani baada ya haya watayaamini

الترجمة: Ali Muhsin Al Barwani.