بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
نٓۚ وَٱلۡقَلَمِ وَمَا يَسۡطُرُونَ ١Nuun. Naapa kwa kalamu na yale wayaandikayo مَآ أَنتَ بِنِعۡمَةِ رَبِّكَ بِمَجۡنُونٍ ٢Kwa neema ya Mola wako Mlezi wewe si mwendawazimu وَإِنَّ لَكَ لَأَجۡرًا غَيۡرَ مَمۡنُونٍ ٣Na kwa hakika wewe una malipo yasiyo katika وَإِنَّكَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِيمٍ ٤Na hakika wewe una tabia tukufu فَسَتُبۡصِرُ وَيُبۡصِرُونَ ٥Karibu utaona, na wao wataona بِأَييِّكُمُ ٱلۡمَفۡتُونُ ٦Ni nani kati yenu aliye pandwa na wazimu إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُهۡتَدِينَ ٧Hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye ajuaye zaidi nani aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anaye wajua zaidi walio ongoka فَلَا تُطِعِ ٱلۡمُكَذِّبِينَ ٨Basi usiwat'ii wanao kadhibisha وَدُّواْ لَوۡ تُدۡهِنُ فَيُدۡهِنُونَ ٩Wanatamani lau unge lainisha ili nao wakulainishie وَلَا تُطِعۡ كُلَّ حَلَّافٍ مَّهِينٍ ١٠Wala usimt'ii kila mwingi wa kuapa wa kudharauliwa هَمَّازٍ مَّشَّآءِۭ بِنَمِيمٍ ١١Mtapitapi, apitaye akifitini مَّنَّاعٍ لِّلۡخَيۡرِ مُعۡتَدٍ أَثِيمٍ ١٢Mwenye kuzuia kheri, dhaalimu, mwingi wa madhambi عُتُلِّۭ بَعۡدَ ذَٰلِكَ زَنِيمٍ ١٣Mkavu, na juu ya hayo, mshari, amejipachika tu أَن كَانَ ذَا مَالٍ وَبَنِينَ ١٤Ati kwa kuwa ana mali na watoto إِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِ ءَايَٰتُنَا قَالَ أَسَٰطِيرُ ٱلۡأَوَّلِينَ ١٥Anapo somewa Aya zetu, husema: Hizi ni simulizi za uwongo za watu wa zamani سَنَسِمُهُۥ عَلَى ٱلۡخُرۡطُومِ ١٦Tutamtia kovu juu ya pua yake إِنَّا بَلَوۡنَٰهُمۡ كَمَا بَلَوۡنَآ أَصۡحَٰبَ ٱلۡجَنَّةِ إِذۡ أَقۡسَمُواْ لَيَصۡرِمُنَّهَا مُصۡبِحِينَ ١٧Hakika tumewajaribu hawa kama tulivyo wajaribu wale wenye shamba, walipo apa kwamba watayavuna mazao yake itakapo kuwa asubuhi وَلَا يَسۡتَثۡنُونَ ١٨Wala hawakusema: Mungu akipenda فَطَافَ عَلَيۡهَا طَآئِفٌ مِّن رَّبِّكَ وَهُمۡ نَآئِمُونَ ١٩Basi lilitokea tukio juu yake kutoka kwa Mola wako Mlezi, nao wamelala فَأَصۡبَحَتۡ كَٱلصَّرِيمِ ٢٠Likawa kama usiku wa giza فَتَنَادَوۡاْ مُصۡبِحِينَ ٢١Asubuhi wakaitana أَنِ ٱغۡدُواْ عَلَىٰ حَرۡثِكُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰرِمِينَ ٢٢Ya kwamba nendeni kondeni mwenu ikiwa mnataka kuvuna فَٱنطَلَقُواْ وَهُمۡ يَتَخَٰفَتُونَ ٢٣Basi walikwenda na huku wakinong'onezana أَن لَّا يَدۡخُلَنَّهَا ٱلۡيَوۡمَ عَلَيۡكُم مِّسۡكِينٌ ٢٤Ya kuwa leo hata masikini mmoja asikuingilieni وَغَدَوۡاْ عَلَىٰ حَرۡدٍ قَٰدِرِينَ ٢٥Na walikwenda asubuhi, nao wameshikilia azimio hilo فَلَمَّا رَأَوۡهَا قَالُوٓاْ إِنَّا لَضَآلُّونَ ٢٦Basi walipo liona, wakasema: Hakika tumepotea بَلۡ نَحۡنُ مَحۡرُومُونَ ٢٧Bali tumenyimwa قَالَ أَوۡسَطُهُمۡ أَلَمۡ أَقُل لَّكُمۡ لَوۡلَا تُسَبِّحُونَ ٢٨Mbora wao akasema: Sikukwambieni, kwa nini hamumtakasi Mwenyezi Mungu قَالُواْ سُبۡحَٰنَ رَبِّنَآ إِنَّا كُنَّا ظَٰلِمِينَ ٢٩Wakasema: Ametakasika Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tulikuwa wenye kudhulumu فَأَقۡبَلَ بَعۡضُهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٍ يَتَلَٰوَمُونَ ٣٠Basi wakakabiliana kulaumiana wao kwa wao قَالُواْ يَٰوَيۡلَنَآ إِنَّا كُنَّا طَٰغِينَ ٣١Wakasema: Ole wetu! Tulikuwa tumeikiuka mipaka عَسَىٰ رَبُّنَآ أَن يُبۡدِلَنَا خَيۡرًا مِّنۡهَآ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا رَٰغِبُونَ ٣٢Asaa Mola wetu Mlezi akatubadilishia lilio bora kuliko hili. Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi كَذَٰلِكَ ٱلۡعَذَابُۖ وَلَعَذَابُ ٱلۡأٓخِرَةِ أَكۡبَرُۚ لَوۡ كَانُواْ يَعۡلَمُونَ ٣٣Namna hivi yanakuwa mateso, na bila ya shaka mateso ya Akhera ni makubwa zaidi, laiti wangeli jua إِنَّ لِلۡمُتَّقِينَ عِندَ رَبِّهِمۡ جَنَّٰتِ ٱلنَّعِيمِ ٣٤Hakika wachamngu watakuwa na Bustani za neema kwa Mola wao Mlezi أَفَنَجۡعَلُ ٱلۡمُسۡلِمِينَ كَٱلۡمُجۡرِمِينَ ٣٥Kwani tutawafanya Waislamu kama wakosefu مَا لَكُمۡ كَيۡفَ تَحۡكُمُونَ ٣٦Mna nini? Mnahukumu vipi أَمۡ لَكُمۡ كِتَٰبٌ فِيهِ تَدۡرُسُونَ ٣٧Au mnacho kitabu ambacho ndani yake mnasoma إِنَّ لَكُمۡ فِيهِ لَمَا تَخَيَّرُونَ ٣٨Kuwa mtapata humo mnayo yapenda أَمۡ لَكُمۡ أَيۡمَٰنٌ عَلَيۡنَا بَٰلِغَةٌ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ إِنَّ لَكُمۡ لَمَا تَحۡكُمُونَ ٣٩Au mnazo ahadi za viapo juu yetu za kufika Siku ya Kiyama ya kuwa hakika mtapata kila mnayo jihukumia سَلۡهُمۡ أَيُّهُم بِذَٰلِكَ زَعِيمٌ ٤٠Waulize: Ni nani miongoni mwao dhamini wa haya أَمۡ لَهُمۡ شُرَكَآءُ فَلۡيَأۡتُواْ بِشُرَكَآئِهِمۡ إِن كَانُواْ صَٰدِقِينَ ٤١Au wanao washirika? Basi wawalete washirika wao wakiwa wanasema kweli يَوۡمَ يُكۡشَفُ عَن سَاقٍ وَيُدۡعَوۡنَ إِلَى ٱلسُّجُودِ فَلَا يَسۡتَطِيعُونَ ٤٢Siku utakapo wekwa wazi mundi, na wataitwa kusujudu, lakini hawataweza خَٰشِعَةً أَبۡصَٰرُهُمۡ تَرۡهَقُهُمۡ ذِلَّةٌۖ وَقَدۡ كَانُواْ يُدۡعَوۡنَ إِلَى ٱلسُّجُودِ وَهُمۡ سَٰلِمُونَ ٤٣Macho yao yatainama chini, fedheha itawafunika. Na hakika walikuwa wakiitwa wasujudu walipo kuwa wazima فَذَرۡنِي وَمَن يُكَذِّبُ بِهَٰذَا ٱلۡحَدِيثِۖ سَنَسۡتَدۡرِجُهُم مِّنۡ حَيۡثُ لَا يَعۡلَمُونَ ٤٤Basi niache na wanao kadhibisha maneno haya! Tutawavutia kidogo kidogo kwa mahali wasipo pajua وَأُمۡلِي لَهُمۡۚ إِنَّ كَيۡدِي مَتِينٌ ٤٥Na ninawapururia muhula; hakika hila zangu ni imara أَمۡ تَسۡـَٔلُهُمۡ أَجۡرًا فَهُم مِّن مَّغۡرَمٍ مُّثۡقَلُونَ ٤٦Au unawaomba ujira, na wao wanaemewa na gharama hiyo أَمۡ عِندَهُمُ ٱلۡغَيۡبُ فَهُمۡ يَكۡتُبُونَ ٤٧Au iko kwao siri, basi wao wanaiandika فَٱصۡبِرۡ لِحُكۡمِ رَبِّكَ وَلَا تَكُن كَصَاحِبِ ٱلۡحُوتِ إِذۡ نَادَىٰ وَهُوَ مَكۡظُومٌ ٤٨Basi ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi, wala usiwe kama mmezwa na samaki, alipo nadi naye kazongwa لَّوۡلَآ أَن تَدَٰرَكَهُۥ نِعۡمَةٌ مِّن رَّبِّهِۦ لَنُبِذَ بِٱلۡعَرَآءِ وَهُوَ مَذۡمُومٌ ٤٩Kama isingeli mfikia neema kutoka kwa Mola wake Mlezi, bila ya shaka angeli tupwa ufukweni naye ni mwenye kulaumiwa فَٱجۡتَبَٰهُ رَبُّهُۥ فَجَعَلَهُۥ مِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ ٥٠Lakini Mola wake Mlezi alimteua na akamfanya miongoni mwa watu wema وَإِن يَكَادُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَيُزۡلِقُونَكَ بِأَبۡصَٰرِهِمۡ لَمَّا سَمِعُواْ ٱلذِّكۡرَ وَيَقُولُونَ إِنَّهُۥ لَمَجۡنُونٌ ٥١Na walio kufuru hukaribia kukutelezesha kwa macho yao, wanapo sikia mawaidha, na wanasema: Hakika yeye ni mwendawazimu وَمَا هُوَ إِلَّا ذِكۡرٌ لِّلۡعَٰلَمِينَ ٥٢Na hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote