Millat al-Islam

Chapter 105 · 5 verses · Abdullah Muhammad Abu Bakr

Surah Al-Fil in Swahili

Arabic with tafsir Listen to Surah Al-Fil (851 reciters)
Meccanسورة الفيل5 verses

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

أَلَمۡ تَرَ كَيۡفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِأَصۡحَٰبِ ٱلۡفِيلِ ١Je hujui, ewe Mtume, namna Alivyowafanya Mola wako watu wa ndovu: Abraha Mhebeshi na jeshi lake ambalo alikuja nalo ili kuivunja Alkaba tukufu أَلَمۡ يَجۡعَلۡ كَيۡدَهُمۡ فِي تَضۡلِيلٍ ٢Kwani Hakuijaalia mipango yao mibaya waliyoifanya ni yenye kuvunjika na kupita patupu وَأَرۡسَلَ عَلَيۡهِمۡ طَيۡرًا أَبَابِيلَ ٣Na Aliwapelekea makundi yaliyofuatana تَرۡمِيهِم بِحِجَارَةٍ مِّن سِجِّيلٍ ٤ya ndege waliokuwa wakiwatupia wao vijiwe vya udongo mkavu mgumu فَجَعَلَهُمۡ كَعَصۡفٍ مَّأۡكُولِۭ ٥Akawapondaponda, wakawa ni kama majani makavu yaliyoliwa na wanyama na halafu kutupwa

Translation: Abdullah Muhammad Abu Bakr.