Millat al-Islam

Chapter 104 · 9 verses · Abdullah Muhammad Abu Bakr

Surah Al-Humaza in Swahili

Arabic with tafsir Listen to Surah Al-Humaza (1273 reciters)
Meccanسورة الهمزة9 verses

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَيۡلٌ لِّكُلِّ هُمَزَةٍ لُّمَزَةٍ ١Shari na maangamivu yatampata kila mwenye kusengenya watu na kuwatukana ٱلَّذِي جَمَعَ مَالًا وَعَدَّدَهُۥ ٢Ambaye hamu yake ni kukusanya mali na kuyahesabu يَحۡسَبُ أَنَّ مَالَهُۥٓ أَخۡلَدَهُۥ ٣Akidhani kuwa mali yake ambayo ameyakusanya yatampa dhamana ya kuishi milele duniani na kuhepa kuhesabiwa كـَلَّاۖ لَيُنۢبَذَنَّ فِي ٱلۡحُطَمَةِ ٤Anavyodhania sivyo. Atatiwa ndani ya Moto ambao huvunjavunja kila kinachotiwa وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡحُطَمَةُ ٥Lipi lililokujulisha, ewe Mtume, ni upi huo Moto unaovunjavunja نَارُ ٱللَّهِ ٱلۡمُوقَدَةُ ٦Huo ni Moto wa Mwenyezi Mungu uliowashwa ٱلَّتِي تَطَّلِعُ عَلَى ٱلۡأَفۡـِٔدَةِ ٧Ambao kwa ukali wake hupenyeza miilini ukafikia kwenye nyoyo إِنَّهَا عَلَيۡهِم مُّؤۡصَدَةٌ ٨Moto huo umefungiwa juu yao wakiwa wametiwa minyororo فِي عَمَدٍ مُّمَدَّدَةِۭ ٩na pingu ndefu ili wasitoke

Translation: Abdullah Muhammad Abu Bakr.