Arabic with tafsir
Listen to Surah Al-Humaza (1273 reciters)
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
وَيۡلٌ لِّكُلِّ هُمَزَةٍ لُّمَزَةٍ ١Ole wake kila safihi, msengenyaji ٱلَّذِي جَمَعَ مَالًا وَعَدَّدَهُۥ ٢Aliye kusanya mali na kuyahisabu يَحۡسَبُ أَنَّ مَالَهُۥٓ أَخۡلَدَهُۥ ٣Anadhani ya kuwa mali yake yatambakisha milele كـَلَّاۖ لَيُنۢبَذَنَّ فِي ٱلۡحُطَمَةِ ٤Hasha! Atavurumishwa katika H'ut'ama وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡحُطَمَةُ ٥Na nani atakujuvya ni nini H'ut'ama نَارُ ٱللَّهِ ٱلۡمُوقَدَةُ ٦Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa ٱلَّتِي تَطَّلِعُ عَلَى ٱلۡأَفۡـِٔدَةِ ٧Ambao unapanda nyoyoni إِنَّهَا عَلَيۡهِم مُّؤۡصَدَةٌ ٨Hakika huo utafungiwa nao فِي عَمَدٍ مُّمَدَّدَةِۭ ٩Kwenye nguzo zilio nyooshwa
Translation: Ali Muhsin Al Barwani.