Millat al-Islam

Chapter 101 · 11 verses · Ali Muhsin Al Barwani

Surah Al-Qaria in Swahili

Arabic with tafsir Listen to Surah Al-Qaria (1290 reciters)

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

ٱلۡقَارِعَةُ ١Inayo gonga مَا ٱلۡقَارِعَةُ ٢Nini Inayo gonga وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡقَارِعَةُ ٣Na nini kitacho kujuilisha nini Inayo gonga يَوۡمَ يَكُونُ ٱلنَّاسُ كَٱلۡفَرَاشِ ٱلۡمَبۡثُوثِ ٤Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika وَتَكُونُ ٱلۡجِبَالُ كَٱلۡعِهۡنِ ٱلۡمَنفُوشِ ٥Na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa فَأَمَّا مَن ثَقُلَتۡ مَوَٰزِينُهُۥ ٦Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ ٧Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza وَأَمَّا مَنۡ خَفَّتۡ مَوَٰزِينُهُۥ ٨Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu فَأُمُّهُۥ هَاوِيَةٌ ٩Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا هِيَهۡ ١٠Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo نَارٌ حَامِيَةُۢ ١١Ni Moto mkali

Translation: Ali Muhsin Al Barwani.