Millat al-Islam

Chapter 114 · 6 verses · Abdullah Muhammad Abu Bakr

Surah Al-Nas in Swahili

Arabic with tafsir Listen to Surah Al-Nas (1315 reciters)
Meccanسورة الناس6 verses

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلنَّاسِ ١Sema, ewe Mtume, «Ninajilinda na kutaka hifadhi kwa Bwana wa watu, Mwenye uweza, Peke Yake, wa kulirudisha shari lao مَلِكِ ٱلنَّاسِ ٢«Mfalme wa watu, Mwenye kupeleka mambo yao yote Anavyotaka, Aliye Mkwasi kutowahitajia إِلَٰهِ ٱلنَّاسِ ٣«Mola wa watu, Ambaye hapana mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye مِن شَرِّ ٱلۡوَسۡوَاسِ ٱلۡخَنَّاسِ ٤«Kutokana na udhia wa shetani ambaye hutia watu wasiwasi wanapoghafilika na hujificha atajwapo Mwenyezi Mungu ٱلَّذِي يُوَسۡوِسُ فِي صُدُورِ ٱلنَّاسِ ٥«Mwenye kupenyeza shari na shaka kwenye vifua vya watu مِنَ ٱلۡجِنَّةِ وَٱلنَّاسِ ٦«Miongoni mwa mashetani wa kijini na kibinadamu.»

Translation: Abdullah Muhammad Abu Bakr.