بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
لَآ أُقۡسِمُ بِهَٰذَا ٱلۡبَلَدِ ١Naapa kwa Mji huu وَأَنتَ حِلُّۢ بِهَٰذَا ٱلۡبَلَدِ ٢Nawe unaukaa Mji huu وَوَالِدٍ وَمَا وَلَدَ ٣Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa لَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ فِي كَبَدٍ ٤Hakika tumemuumba mtu katika taabu أَيَحۡسَبُ أَن لَّن يَقۡدِرَ عَلَيۡهِ أَحَدٌ ٥Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza يَقُولُ أَهۡلَكۡتُ مَالًا لُّبَدًا ٦Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali أَيَحۡسَبُ أَن لَّمۡ يَرَهُۥٓ أَحَدٌ ٧Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona أَلَمۡ نَجۡعَل لَّهُۥ عَيۡنَيۡنِ ٨Kwani hatukumpa macho mawili وَلِسَانًا وَشَفَتَيۡنِ ٩Na ulimi, na midomo miwili وَهَدَيۡنَٰهُ ٱلنَّجۡدَيۡنِ ١٠Na tukambainishia zote njia mbili فَلَا ٱقۡتَحَمَ ٱلۡعَقَبَةَ ١١Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡعَقَبَةُ ١٢Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani فَكُّ رَقَبَةٍ ١٣Kumkomboa mtumwa أَوۡ إِطۡعَٰمٌ فِي يَوۡمٍ ذِي مَسۡغَبَةٍ ١٤Au kumlisha siku ya njaa يَتِيمًا ذَا مَقۡرَبَةٍ ١٥Yatima aliye jamaa أَوۡ مِسۡكِينًا ذَا مَتۡرَبَةٍ ١٦Au masikini aliye vumbini ثُمَّ كَانَ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَتَوَاصَوۡاْ بِٱلصَّبۡرِ وَتَوَاصَوۡاْ بِٱلۡمَرۡحَمَةِ ١٧Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ ١٨Hao ndio watu wa kheri wa kuliani وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِنَا هُمۡ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ ١٩Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni عَلَيۡهِمۡ نَارٌ مُّؤۡصَدَةُۢ ٢٠Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande