قُلۡ يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡكَٰفِرُونَ ١Sema, ewe Mtume, kuwaambia waliokufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake: «Enyi wenye kumkanusha Mwenyezi Munguلَآ أَعۡبُدُ مَا تَعۡبُدُونَ ٢«Mimi siabudu mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu na waungu wa urongoوَلَآ أَنتُمۡ عَٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ ٣«Wala nyinyi si wenye kuabudu Mola Mmoja ninayemuabudu Ambaye ndiye Anayestahiki kuabudiwaوَلَآ أَنَا۠ عَابِدٌ مَّا عَبَدتُّمۡ ٤«Wala mimi si mwenye kuabudu mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu na waungu wa urongoوَلَآ أَنتُمۡ عَٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ ٥«Wala nyinyi si wenye kuabudu mbeleni ninayemuabudu.» Aya hii imeteremka juu ya watu makhsusi miongoni mwa washirikina ambao Mwenyezi Mungu Alijua kuwa hawataamini kabisaلَكُمۡ دِينُكُمۡ وَلِيَ دِينِ ٦«Nyinyi mna dini yenu mnayoiamini na mimi nina Dini yangu ambayo sitaki nyingine.»