ملة الإسلام

السورة 91 · 15 آية · Ali Muhsin Al Barwani

سورة الشمس باللغة السواحلية

السورة بالعربية مع التفسير استمع إلى سورة الشمس (1,360 قارئاً)
مكيةسورة الشمس١٥ آية

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلشَّمۡسِ وَضُحَىٰهَا ١Naapa kwa jua na mwangaza wake وَٱلۡقَمَرِ إِذَا تَلَىٰهَا ٢Na kwa mwezi unapo lifuatia وَٱلنَّهَارِ إِذَا جَلَّىٰهَا ٣Na kwa mchana unapo lidhihirisha وَٱلَّيۡلِ إِذَا يَغۡشَىٰهَا ٤Na kwa usiku unapo lifunika وَٱلسَّمَآءِ وَمَا بَنَىٰهَا ٥Na kwa mbingu na kwa aliye ijenga وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا طَحَىٰهَا ٦Na kwa ardhi na kwa aliye itandaza وَنَفۡسٍ وَمَا سَوَّىٰهَا ٧Na kwa nafsi na kwa aliye itengeneza فَأَلۡهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقۡوَىٰهَا ٨Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake قَدۡ أَفۡلَحَ مَن زَكَّىٰهَا ٩Hakika amefanikiwa aliye itakasa وَقَدۡ خَابَ مَن دَسَّىٰهَا ١٠Na hakika amekhasiri aliye iviza كَذَّبَتۡ ثَمُودُ بِطَغۡوَىٰهَآ ١١Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotofu wao إِذِ ٱنۢبَعَثَ أَشۡقَىٰهَا ١٢Alipo simama mwovu wao mkubwa فَقَالَ لَهُمۡ رَسُولُ ٱللَّهِ نَاقَةَ ٱللَّهِ وَسُقۡيَٰهَا ١٣Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipo waambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمۡدَمَ عَلَيۡهِمۡ رَبُّهُم بِذَنۢبِهِمۡ فَسَوَّىٰهَا ١٤Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa وَلَا يَخَافُ عُقۡبَٰهَا ١٥Wala Yeye haogopi matokeo yake

الترجمة: Ali Muhsin Al Barwani.